Kanisa ka Kiinjili, la Kilutheri Tanzania, KKKT ina hstoria na ni taasisi ya muda mrefu.
Ina taratibu na kanuni zake , mchungaji au mtumishi atafanya mbwembwe zake zoote lakini lazima awe ndani ya utaratibu wa Kanisa.
Mtumishi akiwa na Karama au upako lazima aongozwe na hekima na siyo jeuri na kiburi cha kufanya na kusema atakavyo kwa kujiona yuko juu ya taratibu zilizowekwa .
Hakuna Mtumishi aliye juu ya KKKT kama taasisi , KKKT ni kubwa kiasi kwamba hata askofu hayupo juu ya KKKT.
Sasa hivi tunsona watumishi wanao lipatia kanisa au usharika mafanikio, cha kushangaza mafanikii yao yanawapanda kichwani na kuanza jeuri, dharau na kiburi.
Sbabu kubwa ni ukubwa wa wafuasi binafsi walionao.
Mwaka jana Dayosisi ya Konde Askofu wake Dr Mwaikali alivuliwa uaskofu.
Wengi wa tulioifuatilia ile ibada ya kumvua Uaskofu tulisononeshwa na uksidi wa Askofu Mwaikali.
Leo, Dayosisi ya KKKT Konde na kanisa linaendelea.
Kama mtumishi anajiona ana karama na unapendwa na watu wengi, bado una wiwa kufuata taratibu za Kanisa.
Kinyume na hapo kwa karama zako anzisha taasisi yako,
Jeuri na kiburi alichoanza kuonyesha hadharani huyu Dr Rev I Kimaro ni upungufu wa maono ya kutoona mbali.
Kuna fununubkuwa Kimaro alionywa mara kadhaa juu ya tabia yake binafsi kujiona yuko juu ya utaratubu, akakaidi, na wakati mwingine anajibu hadharani, na clips zipo.
Sasa inaelekea anavuna alichopanda.