KKKT ni kubwa kuliko Mch. Kimaro, msihuzunike kuna jambo hamlijui, viongozi wake hawajakurupuka

Kkkt viongozi wengi Ni wachawi
Fafanua mkuu, maana tangu enzi za manabii ukisoma Yeremia na Ezekiel kulikuwa na makuhani wachawi au waabudu shetani ambao kwa siri wanalipa hekalu kisogo na kuabudu jua, hili jambo alionyeshwa nabii akapigwa na mshangao muda wa siku saba, ndo ujue shetani alivyo na hila....
 
Siasa zinataka ingizwa kwenye hili jambo
 
Na wengi hawataki hivyo anataka ifuatwe litrujia kama sikosei
 
Sioni kama kuna ajabu kwa mchungaji kuhamishwa, mimi nimekulia KKKT, Nimesoma shule za KKKT na wachungaji walikuwa wanahamishwa kama kawaida tu.
 
Yote hayo uliyoandika umeyajuaje mkuu ilhali umesema wewe siyo muumini? Kwa uandishi wako unaonekana nawe ni mdau.

Vyovyote iwavyo KKKT kuna shida kubwa, wachungaji wengi na viongozi shida kubwa ni maslahi.
Mbona nimeeleza kwenye Uzi hapo mkuu!
Mbona Siku ile kabla ya kombe la dunia nilipoaandika ufaransa watafungwa na Argentina mbona hukuniuliza kwamba naichezea ARGENTINA?
 
ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA SUALA LA KUSIMAMISHWA KWA MCH. DKT. KIMARO

Taarifa za kupewa likizo na kusimamishwa kwa muda kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dkt. Eliona Kimaro zimeanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kuzua hisia nzito miongoni mwa waumini na wasio waumini wa KKKT. Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi.

Hapa tumeweka tazamo wetu wa kitheologia ili kutoa mchango wetu katika hoja hii. Ni dhahiri kuwa misimamo binafsi ya Mch. Dkt. Kimaro imemtia katika misuguano mingi na uongozi wa KKKT kwa kipindi kirefu. Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Tumefuatilia kutoka kwa baadhi ya viongozi ndani ya Dayosisi ya Mashariki na kuelezwa kuwa matamshi ya Mch. Dkt. Kimaro aliyoyatoa hivi karibuni baada ya kutoka Marekani ndiyo yaliyopelekea uongozi wa Dayosisi kumuita na kumpa likizo ambayo imeibua hisia na mjadala mzito baada ya yeye Mch. Dkt. Kimaro kutoa hadharani jambo ambalo lilikuwa ni karipio la Kichungaji.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu bali vijana wa Kiislamu ndio waaminifu kuliko vijana wa Kikristo. Mch. Dkt. Kimaro amesikika pia akisema kuwa watu wote wanaosimama madhabahuni [Wainjilisti, Wachungaji na Maaskofu] ni matapeli na watu wote waliokaa kwenye viti [vya ibadani - Wazee wa Kanisa na waumini] ni matapeli pia. Mch. Dkt. Kimaro amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa takwimu [hajataja ni takwimu gani na taasisi iliyotoa takwimu hizo] zinaeleza hayo aliyosema.

Kitheologia tunapata tafsiri kuwa Mch. Dkt. Kimaro hana imani na maadili ya Kikristo, hana imani na mafundisho ya Kikristo na pia hana imani hata na watumishi wenzake wote wa Kikristo kutoka madhehebu yote nchini Tanzania. Tafsiri hapa ni kuwa Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa ana imani na maadili ya Kiislamu, mafundisho ya Kiislamu na hata Mashehe wa Kiislamu. Pia, Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa hana imani pia na hata vijana wake wa Kikristo ndani ya KKKT na nje ya KKKT ambao siku zote yeye mwenyewe amekuwa akiwafundisha katika ibada, mikesha, semina, morning glory, bali ana imani kubwa na vijana wa Kiislamu ndio maana akawaajiri hao katika miradi yake.

Mtumishi ye yote (Mwinjilisti, Mchungaji/Padre au Askofu) kutoka katika madhehebu yetu ya Katholiko (RC, Moravian, Lutheran, Anglikana na Orthodox) akitoa kauli kama hizo, ni lazima aitwe na uongozi wake, ahojiwe na hata ikibidi achunguzwe. Hicho ndicho kilichotokea kwake Mch. Dkt. Kimaro kuitwa na uongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kuhojiwa na kuchunguzwa. Kauli zake alizotoa zimepingana na imani, mafundisho na maadili ya Kikristo! Kauli ya Mch. Dkt. Kimaro hayakushambulia Ulutheri tu, bali kwa kujua au hata kutokujua, kauli yake ilishambuliwa Ukristo wote kwa ujumla katika nchi hii.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu tunatoa wito kwa waumini wote wa Kikristo nchini kuwa watulivu wakati KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani inashughulikia jambo la Mch. Dkt. Kimaro. Sisi tumelazimika kuandika baada ya kuona kuwa jambo hili limeanza kusambaa mitandaoni na kubeba hisia zaidi kuliko uhalisia na pengine kubeba upotofu mwingi zaidi kuliko ukweli.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
 
Tuseme ukweli waafrika sie hutupendagi mtu aanzishe kitu halafu kionekane naye apate sifa au kusifiwa hakuna kabisa, hapa duniani hakuna aliye mkamilifu bali tunaonyana na kuvumiliana.


Mwisho wa yote wao ndiyo wanafahamiana zaidi na kujuana watayamaliza tu, nuru na giza havitangamani njia itapatikana tu.
 
Mbona nimeeleza kwenye Uzi hapo mkuu!
Mbona Siku ile kabla ya kombe la dunia nilipoaandika ufaransa watafungwa na Argentina mbona hukuniuliza kwamba naichezea ARGENTINA?
Huwezi kudhania kuwa kila aliyesoma hapa basi amesoma post zako zote siyo?! OK, bye.
 
Kwahiyo unamaanisha maombi yake na mafundisho yake yanawaumiza wachawi hao?
Ndio maana yake mi Babu yangu alikuwa mchungaji kkkt, najua kwenye nafasi za juu dayosisi Ni watu wa namna gani
 
Mungu anayehubiriwa na Mch. Kimaro ni mkubwa kuliko KKKT.
πŸ˜¬πŸ˜¬πŸ˜¬πŸ˜¬πŸ˜‚, roho ni mali ya Mungu, kanisa ni la Mungu, ile watu kuja na kuabudu kwenye KKKT haina maana wale zile roho za wale watu ni za KKKT.Shetani hana shida unaabudu wapi au dini yako gani yeye shida yake ipo hapa "U must believe in Supreme being". Sasa akiona mahali kabanwa, na mioyo ya watu inamwelekea Mungu kwa dhati lazima vurugu zianze. Kanisa likimwabudu Mungu kwa roho na kweli, taratibu nyingi sana za kimapokeo zinavunjika automatically na hiko ndio Mafarisayo wa kkkt hawataki kuona.
 
Kila mchungaji nayemjua wa kkkt ni mchaga
 
Haya makanisa makubwa yana misingi imara sana! Usifikili ni rahisi kutoka ukabakia na makali yaleyale!

Sakata lake halitakuwa tofauti na Feisal!

Inside the box mentality...
Hii sio football kwamba lazima muwe 11... this is something else

Wangapi wametoka na wakafanya establisment bhna...

Hao Protestant wenyewe ni wapinga namna Papa alivokuwa anaendesha Kanisa... yani wametoka..... na wapo dunia nzima.

Kimaro ni mkubwa mnoooo tena kuliko 95% ya maaskofu wa hapo.
 
Mimi ni Mlutheri, kune mengi hatuyajui
KUhusu Kimaro, nakumbuka vuguvugu la ubadhirifu wa fedha pale kariakoo ndio lilimuonfoa akaletwa kijitonyama
 
Sioni kama kuna ajabu kwa mchungaji kuhamishwa, mimi nimekulia KKKT, Nimesoma shule za KKKT na wachungaji walikuwa wanahamishwa kama kawaida tu.
Hadi leo wanahamishwa, kuna usharika fulani niliwahi kuabudu wakati fulani, mchungaji alikaa pale kama mwaka na nusu hivi akapewa uhamisho, siku ya kuaga akasema ndio kwanza nilikuwa nimeanza kuwazoea lkn nimepata uhamisho kwenda usharika mwingine na ndio wito nilioitiwa, mbaki na amani ya Bwana, tukasema Amen! Baada ya miezi miwili akaja tukamuaga na bonge la sherehe na zawadi kama zote.....

kwahiyo kimaro siku atakayoenda kuagwa kijito ataondoka na mazawadi kibao ukizingatia waumini wanampenda πŸ˜… πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Endeleeni kusubiri lakini msifadhaike
Unatuchanganya sasa, kwenye post yako umesema tusubiri, tumekubali ngoja tusubiri. Mara unasema tena tusifadhaike[emoji849][emoji849]
 
Ati wewe ni muumini wa Eliona Kimaro? [emoji848][emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…