KKKT ni kubwa kuliko Mch. Kimaro, msihuzunike kuna jambo hamlijui, viongozi wake hawajakurupuka

ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA SUALA LA KUSIMAMISHWA KWA MCH. DKT. KIMARO

Taarifa za kupewa likizo na kusimamishwa kwa muda kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dkt. Eliona Kimaro zimeanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kuzua hisia nzito miongoni mwa waumini na wasio waumini wa KKKT. Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi.

Hapa tumeweka tazamo wetu wa kitheologia ili kutoa mchango wetu katika hoja hii. Ni dhahiri kuwa misimamo binafsi ya Mch. Dkt. Kimaro imemtia katika misuguano mingi na uongozi wa KKKT kwa kipindi kirefu. Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Tumefuatilia kutoka kwa baadhi ya viongozi ndani ya Dayosisi ya Mashariki na kuelezwa kuwa matamshi ya Mch. Dkt. Kimaro aliyoyatoa hivi karibuni baada ya kutoka Marekani ndiyo yaliyopelekea uongozi wa Dayosisi kumuita na kumpa likizo ambayo imeibua hisia na mjadala mzito baada ya yeye Mch. Dkt. Kimaro kutoa hadharani jambo ambalo lilikuwa ni karipio la Kichungaji.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu bali vijana wa Kiislamu ndio waaminifu kuliko vijana wa Kikristo. Mch. Dkt. Kimaro amesikika pia akisema kuwa watu wote wanaosimama madhabahuni [Wainjilisti, Wachungaji na Maaskofu] ni matapeli na watu wote waliokaa kwenye viti [vya ibadani - Wazee wa Kanisa na waumini] ni matapeli pia. Mch. Dkt. Kimaro amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa takwimu [hajataja ni takwimu gani na taasisi iliyotoa takwimu hizo] zinaeleza hayo aliyosema.

Kitheologia tunapata tafsiri kuwa Mch. Dkt. Kimaro hana imani na maadili ya Kikristo, hana imani na mafundisho ya Kikristo na pia hana imani hata na watumishi wenzake wote wa Kikristo kutoka madhehebu yote nchini Tanzania. Tafsiri hapa ni kuwa Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa ana imani na maadili ya Kiislamu, mafundisho ya Kiislamu na hata Mashehe wa Kiislamu. Pia, Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa hana imani pia na hata vijana wake wa Kikristo ndani ya KKKT na nje ya KKKT ambao siku zote yeye mwenyewe amekuwa akiwafundisha katika ibada, mikesha, semina, morning glory, bali ana imani kubwa na vijana wa Kiislamu ndio maana akawaajiri hao katika miradi yake.

Mtumishi ye yote (Mwinjilisti, Mchungaji/Padre au Askofu) kutoka katika madhehebu yetu ya Katholiko (RC, Moravian, Lutheran, Anglikana na Orthodox) akitoa kauli kama hizo, ni lazima aitwe na uongozi wake, ahojiwe na hata ikibidi achunguzwe. Hicho ndicho kilichotokea kwake Mch. Dkt. Kimaro kuitwa na uongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kuhojiwa na kuchunguzwa. Kauli zake alizotoa zimepingana na imani, mafundisho na maadili ya Kikristo! Kauli ya Mch. Dkt. Kimaro hayakushambulia Ulutheri tu, bali kwa kujua au hata kutokujua, kauli yake ilishambuliwa Ukristo wote kwa ujumla katika nchi hii.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu tunatoa wito kwa waumini wote wa Kikristo nchini kuwa watulivu wakati KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani inashughulikia jambo la Mch. Dkt. Kimaro. Sisi tumelazimika kuandika baada ya kuona kuwa jambo hili limeanza kusambaa mitandaoni na kubeba hisia zaidi kuliko uhalisia na pengine kubeba upotofu mwingi zaidi kuliko ukweli.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
 
Sioni kama kuna ajabu kwa mchungaji kuhamishwa, mimi nimekulia KKKT, Nimesoma shule za KKKT na wachungaji walikuwa wanahamishwa kama kawaida tu.
Hakuna ajabu
 
Jamani munamkumbuka Askofu Dr. Mwaikali?
 
Waumini wanauliza waende wapi! Mimi nawashauri watulie! Ametoka KIMARO ATAKUJA KIMARIO
 
kuna video alikua anawaombea waumini baada ya kuwaaga huku analia, sasa sijui naye alikuwa analia nini Mch kimaro
 
Bwashee anakula mwenyewe hataki kutoa bahasha kwa mkubwa.
Mwenzie kaksai ni mtoto wa mjini anaachia mzigo ndio maana pale hajaamishwa ila kawekewa msaidizi yeye akapewa msimamizi wa miradi
 
Askofu Shoo inawezekana alibanwa alibanwa asipige Hela, akaamua kumuanzishia. Ni sawa na Mwaikali alivyomzuia asiuze Hoteli kule Nyanda za juu kusini
 
NAUNGA MKONO HATUA ZA KANISA KUMSIMAMISHA KAZI.

Mch.Dr Kimaro hivi karibuni alitoa kauli ya kushangaza na ya kusikitisha sana na ilikuwa na madhara makubwa sana Kwa vijana WA Imani yake.

Alisema " Vijana WA Imani ya...........
ni waaminifu sana kuliko vijana WA kikristu,Kijana WA Imani ya ........ ukimpa kazi ataifanya Kwa uaminifu mkubwa sana kuliko vijana wa kikristu,Mimi kwangu nawatumiaga vijana wa Imani ......... kunifanyia kazi zangu"

Kauli hiyo niliandika na kuipinga Kwa ilikuwa na madhara makubwa Kwa vijana WA kikristu hasa Kwenye Ajira.

Kwa kauli hiyo nzito ambayo imetolewa na Mch ,
Tena Mchungaji kiongozi
Tena ni Dr.
Tena ni WA Imani ya kikristu anasema vijana wake WA kikristu siyo waaminifu Kwenye kazi ,Sasa hapo unategemea Serikali itawapa Ajira watu wasio waaminifu Kwenye kazi?

Watu binafsi,Mashirika binafsi wanaposikia kauli hii ya Mchungaji mwenye dhamana kubwa akisema vijana WA Imani yake siyo waaminifu unategemea Kwenye Ajira Hawa watu binafsi inapotokea Kuna Mkristu anasifa na mwislamu anasifa za kuajiliwa,
Kwa suala la uaminifu ambalo hadi kiongozi wao WA kiroho kawakandia kuwa siyo waaminifu unategemea kijana WA kikristu atapata Ajira hapo?

TUMUULIZE MCH KIMARO,
Unasema vijana wako WA kikristu siyo waaminifu,!!! Lakini sadaka zao ambazo zimetokana na uharamia wao unaziruhusu kuingia madhabahuni na unazibariki huku ukijua vijana Hao siyo waaminifu haoni na yeye ni tatizo?

Anaposema siyo waaminifu maana nyingine ni wezi ,wazinzi n.k na yeye anajua kuwa vijana wake siyo waaminifu ni kwanini amekuwa akipokea sadaka zao?

Na anapokiri kwamba vijana wake siyo waaminifu je wasio WA Imani yake unategemea wakiwa Kwenye mamlaka ya kuajiri watawatazama Hao vijana WA kikristu?

Kwanza Kwa utafiti upi alioufanya akagundua hilo?

Kumpa kazi kijana mmoja WA kikristu na kijana huyo Kuharibu kazi Kwenye shamba lake huwezi ukatumia kigezo hicho kujustfy kwamba vijana WA kikristu siyo waaminifu!!!

Hao wanaoandamana kumtaka laiti wangejua madhara makubwa ya kauli ile ya Mchungaji wao Kwa Vijana wao WA kikristu kamwe wangelishukuru kanisa Kwa hatua lilizochukua.

Na kama anaona anaongoza kundi lisilo la waaminifu kwanini asiende Kuungana na kundi hilo la Imani nyingine lenye vijana waaminifu? Kwanini kuendelea kukaa na kundi la vijana WA kikristu ambao ni wezi???.

Sina maneno mbadala ya kutumia Mchungaji huyu amepotoka,Amekengeuka pengine alitoa kauli ile Kwa bahati mbaya ,Au hakujua madhara yake au alitaka umaarufu kutoka Dini ya pili basi. Akatumie likizo ile kubadili mwenendo wake.

Namuombea hekima za kufuta matamshi yake hayo na awaombe radhi vijana WA Imani yake na aliombe radhi Kanisa na Kwa Mungu afanye toba ya kweli.

Naunga mkono Kanisa Kwa hatua lilizochukua.
Na hili Liwe FUNDISHO kwake na Kwa WENGINE wenye kunanga watu WA Imani Yao na kuitukuza watu WA Imani nyingine Kwa kutaka sifa au umaarufu usiyo na tija.

Mtu WA Imani yako akikosea mkanye.

Andiko linasema
" Asiyewapenda WA kwao ni Mchawi"
 
ni waaminifu sana kuliko vijana WA kikristu, Kijana WA Imani ya ........ ukimpa kazi ataifanya Kwa uaminifu mkubwa sana kuliko vijana wa kikristu, Mimi kwangu nawatumiaga vijana wa Imani ......... kunifanyia kazi zangu"

Kauli hiyo niliandika na kuipinga Kwa ilikuwa na madhara makubwa Kwa vijana WA kikristu hasa Kwenye Ajira.

Kwa kauli hiyo nzito ambayo imetolewa na Mch ,
Tena Mchungaji kiongozi
Tena ni Dr.
Tena ni WA Imani ya kikristu anasema vijana wake WA kikristu siyo waaminifu Kwenye kazi ,Sasa hapo unategemea Serikali itawapa Ajira watu wasio waaminifu Kwenye kazi?

Watu binafsi,Mashirika binafsi wanaposikia kauli hii ya Mchungaji mwenye dhamana kubwa akisema vijana WA Imani yake siyo waaminifu unategemea Kwenye Ajira Hawa watu binafsi inapotokea Kuna Mkristu anasifa na mwislamu anasifa za kuajiliwa.

Kwa suala la uaminifu ambalo hadi kiongozi wao WA kiroho kawakandia kuwa siyo waaminifu unategemea kijana WA kikristu atapata Ajira hapo?

TUMUULIZE MCH KIMARO,
Unasema vijana wako WA kikristu siyo waaminifu,!!! Lakini sadaka zao ambazo zimetokana na uharamia wao unaziruhusu kuingia madhabahuni na unazibariki huku ukijua vijana Hao siyo waaminifu haoni na yeye ni tatizo?

Anaposema siyo waaminifu maana nyingine ni wezi ,wazinzi n.k na yeye anajua kuwa vijana wake siyo waaminifu ni kwanini amekuwa akipokea sadaka zao?

Na anapokiri kwamba vijana wake siyo waaminifu je wasio WA Imani yake unategemea wakiwa Kwenye mamlaka ya kuajiri watawatazama Hao vijana WA kikristu?

Kwanza Kwa utafiti upi alioufanya akagundua hilo?

Kumpa kazi kijana mmoja WA kikristu na kijana huyo Kuharibu kazi Kwenye shamba lake huwezi ukatumia kigezo hicho kujustfy kwamba vijana WA kikristu siyo waaminifu!!!

Hao wanaoandamana kumtaka laiti wangejua madhara makubwa ya kauli ile ya Mchungaji wao Kwa Vijana wao WA kikristu kamwe wangelishukuru kanisa Kwa hatua lilizochukua.

Na kama anaona anaongoza kundi lisilo la waaminifu kwanini asiende Kuungana na kundi hilo la Imani nyingine lenye vijana waaminifu? Kwanini kuendelea kukaa na kundi la vijana WA kikristu ambao ni wezi???.

Sina maneno mbadala ya kutumia Mchungaji huyu amepotoka,Amekengeuka pengine alitoa kauli ile Kwa bahati mbaya ,Au hakujua madhara yake au alitaka umaarufu kutoka Dini ya pili basi. Akatumie likizo ile kubadili mwenendo wake.

Namuombea hekima za kufuta matamshi yake hayo na awaombe radhi vijana WA Imani yake na aliombe radhi Kanisa na Kwa Mungu afanye toba ya kweli.

Naunga mkono Kanisa Kwa hatua lilizochukua.
Na hili Liwe FUNDISHO kwake na Kwa WENGINE wenye kunanga watu WA Imani Yao na kuitukuza watu WA Imani nyingine Kwa kutaka sifa au umaarufu usiyo na tija.

Mtu WA Imani yako akikosea mkanye.

Andiko linasema
" Asiyewapenda WA kwao ni Mchawi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…