KKKT ni kubwa kuliko Mch. Kimaro, msihuzunike kuna jambo hamlijui, viongozi wake hawajakurupuka

Naomba nianze kwa kuwapa pole waumini ambao walibarikiwa na mchungaji kimaro!

Kazi ya kitume ni kama mvua, inanyesha kwa wakati wake na kupisha kwa muda ili shughuli zingine zifanyike, mpate muda wa kupanda, kuvuna, na hata kuezeka panapovuja...
Mkuu kama kosa ni tuhuma tukisema tuhuma za Malasusa humu kutakalika? Mi nafikir ni hekima imekosekana tu. Watu hawajakataa kuhamishwa Mzee ila mfumo uliotumika kwanini likizo na kwanini katikati ya semina. Eti ametolea mfano vijana wa kiislam na WA kikristo hilo mbona liko wazi sana.

Kwani Yesu alivyowaambia wanafunz Wake makahaba na watoza ushuru wanawatangulia kwenda mbinguni alikuwa amewapaisha makahaba au alitaka watubu.

Hawa viongoz wa dini wanatumia mfumo wa kanisa kuzuia watu wanaohisi wanakubalika kuliko wao.
 
NAUNGA MKONO HATUA ZA KANISA KUMSIMAMISHA KAZI.

Mch.Dr Kimaro hivi karibuni alitoa kauli ya kushangaza na ya kusikitisha sana na ilikuwa na madhara makubwa sana Kwa vijana WA Imani yake.

Alisema " Vijana WA Imani ya...
Duh unedadavua vyema sana
 
Tusifike humu! Yule kahamishwa akatumike na kwingine!
 
Kimaro akaanzishe kanisa lake KKKT(K), hiyo K ndani ya mabano ni Kimaro.
 
Kwani uamisho si sehemu ya majukum?kanisa alilonalo kimaro ni kanisa la kimfumo si la mtu hivyo ni km serikali anaamishwa mtu kutoka point a kwenda b, anaweza akaja mzuri au mbaya kuliko kimaro..hatupaswi kuwekeza kwenye watu. Tunapaswa kuwekeza kwenye mifumo imara.
KKKT Ina mapokeo yake km yalivyo makanisa mengine,Wana KKKT muishi humo..hayo mambo ya fellowship na vipindi vingine ni ziada Ila kalenda yenu ya mwaka na liturujia muifuate km inavyopaswahuo ndo uluteri.
Km ilivyo kwa Roman Catholic na Anglican ,Lutheran sio kanisa km la kakobe au la mwingila au gwajima nk.
 
Hakika kabisa
 
"kujiamini" sio sifa mbaya,maana yake kiongozi hatayaumbishwa akiawa kwenye mstari sahihi.
Kosa ni kusema Mungu akikupandisha hakuna wa kukushusha?? 🤣 .wana sababu mbovu zaidi ila wanajaribu kutengeneza uhalali wa waliyoyafanya tu. Wangeweza tu kumuhamisha kawaida bila kutengeneza kashfa kama kweli suala n kituo tu,ila hapa kuna Agenda ya kumuondoa kabisa kama mtumishi wa kanisa.Kuna chuki na hila nyingi,sababu sijui anazungumzia wizi na tabia ovu za viongozi??Mungu alitetee kanisa lake
 
Lkini hapa Kimaro HAJAMISHWA!!hata wangekua na ajenda yao wangemuhamisha kimyakimya ingekuwa bora sana.Hajahamishwa na hajawahi gomea uhamisho,hata sasa kasimamishwa hajagomea kusimamishwa. Kuna jambo kubwa zaidi uongozi wa Dayosisi unajariub kuficha
 
Mbona huhamishwa ni kawaida tu
 
Siyo Jambo la Ajabu wala Mchungaji kupewa Likizo na Kuhamishwa kwenye Usharika mmoja kwenda mwingine

Kama Hamfahamu Hakuna Sharika Mchungaji Kimaro aliokaa kwa Mafanikio Makubwa yake Binafsi ya Kanisa na Dayosisi nzima kwa muda mrefu kama Usharika wa Kariakoo! Lakini ilifikia mahali akaondoka; Aliondoka huku akiwa ameshapata misukosuko Mikubwa ya Kusimamishwa kutokana na Kashfa kubwa iliyoikumba Kanisa. Ila mwisho wa siku alirudi na Kuendeleza Injili Pale pale Usharika wa Kariakoo baada ya Hapo ndo alipelekwa Kijitonyama Mpka hapo Jana alipopewa likizo ya Kupumzika kwa siku 60.
 
Wanamtaka Kimaro siyo Kristo!!!! Hapa pana shida kubwa!!! Hayo mafundisho hayajawaingia hao
Wanmtaka Kimaro siyo Kristo!!! Hapa pana shida kubwa. Inaonyesha mafundisho hayajawaingia hawa watu!!!!
 
Ulichosema sio kweli. Mchungaji kimaro ni msimamizi mzuri wa rasilimali za fedha na yuko makini sana eneo hilo. Alipokea usharika ukiwa na deni la mamilioni na jengo na mali za KKKT Kijitonyama kutaka kuuzwa na benki. Mlivumilia sana huduma zake mpaka hivi karibuni alipomaliza kulipa deni. Na sababu ya yeye kuweza kumaliza deni ni kuwa Dayosisi walikuwa wanapangia matumizi mengine fedha za kulipia deni. Kwa hili ulilosema uje na ushahidi wa kutosha.

Baada ya kuvumilia deni limelipwa sasa Njama za kumuondoa zikaanza kupangwa.

Ni mtu mwenye akili, msimamo, asiyetetereka na anayeweza kulifia neno analotamka.

Wengi wetu hatupendi kuambiwa ukweli. Na ukiwa unasema kweli kuwa na hakika wengi watakupinga.
 
Kapewa likizo,yule ni muajiliwa km mwalimu au daktari na Wana viapo vyao,kupewa likizo mwajiri wake,ifahamike muajiri anaweza kukupa likizo au wewe muajiriwa. Kuomba likizo.
Kuna Aina nyingi za likizo,na baada ya likizo ameambiwa akaripoti makao makuu maana watampangia majukum .
KKKT ni kanisa la kimnyororo,leseni yake ya kukaa kuhubili au kufundisha neno la Mungu imedhaminiwa na kanisa na kwayo ana kiapo Chao Cha kueshimu sio mamlaka tu Bali mapokeo ya kanisa yaani uruteli na si vinginevyo.
Kabla ya yeye kulikua na changamoto za askofu Jerry dhidi ya KKKT, na mwisho wake tunaukumbuka wote ,hivyo naona Mimi ni kawaida ndo kukua kwa kanisa na Imani yao,
Pia Kuna yule askofu Mungu dhidi ya Dayosisi yake,
Unaposajili kanisa Kuna taratibu kanuni miongozo na taratibu,ndo maana anapoapishwa anakili kuufuata mafundisho ya Luther na si vinginevyo.
Km Kuna karama zingine unaruhusiwa kuwa na vipindi baada ya ibada .
Kulikua na changamoto km hizo kwa padre Nkwela kuhusu kalama yake na mafundisho ya ukatoliki. Na katoliki walichukua. Hatua stahiki kwa wakati dhidi ya mapokeo yao.
Hivyo tusilichukulie suala personal badala ya kulichukulia km suala.la.kitendaji kwa maana pale kijitonyama sio usharika wa kwanza kuanzisha yeye na. Hata baada ya. Yeye watakuja wengine. Na wengine .
 
Wanamtaka Kimaro siyo Kristo!!!! Hapa pana shida kubwa!!! Hayo mafundisho hayajawaingia hao

Wanmtaka Kimaro siyo Kristo!!! Hapa pana shida kubwa. Inaonyesha mafundisho hayajawaingia hawa watu!!!!
Ndo hapo sasa!
 
KKKT ina utaratibu wake wa kuwahamisha watumishi kutoka kituo A kwenda kituo B.

Huo ukiotumika kwa Kimaro siyo utaratibu wa kawaida ile ni adhabu!

Kina mchungaji mwingine anaitwa Kisanga alikuwa usharika wa Kitunda relini alisimamishwa miezi 2 baada ya kufanya kosa la kimaadili na sasa hivi yupo Usharika wa chanika baada ya kutubu kosa lake.
 
Tatizo ni kwamba. dhehebu linalazimisha mtu usali kitu kilichopo kwenye kitabu. Yaani mfano keo tarehe 18/January ila sala ya tarehe 31/12 imeshaandikwa. Ukianza kusali tofauti tayari unaitwa mlokole. Dini zina changamoto na hapa tunawafaidisha tu waislam wanapata cha kusema
 
Sijui kwanini siku hizi wakristo umehamia kwenye kuamini watu badala ya kanisa.

Yani mijitu mizima imeandamana eti inamtaka mchungaji wao.
 
Taasisi maanayake ni utaratibu!

Wewe kwanini uwe kinyume na utaratibu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…