KKKT ni kubwa kuliko Mch. Kimaro, msihuzunike kuna jambo hamlijui, viongozi wake hawajakurupuka

KKKT ni kubwa kuliko Mch. Kimaro, msihuzunike kuna jambo hamlijui, viongozi wake hawajakurupuka

Taasisi maanayake ni utaratibu!

Wewe kwanini uwe kinyume na utaratibu?

Mnataka tusali mfumo wa kukremisha ili muendelee kututawala kiroho? Soma vizuri na uelewe huo uzi.
 
Tatizo ni kwamba. dhehebu linalazimisha mtu usali kitu kilichopo kwenye kitabu. Yaani mfano keo tarehe 18/January ila sala ya tarehe 31/12 imeshaandikwa. Ukianza kusali tofauti tayari unaitwa mlokole. Dini zina changamoto na hapa tunawafaidisha tu waislam wanapata cha kusema

Kalenda ya kanisa ipo katika utaratibu rasmi, waumini na wachungaji wote tunelekezwa kuifuata kwa sababu tumekubaliana nayo. Kama mtu anahsi amepata uelewa wa dini na ahitaji kufuata tena utaratibu aliokubali wakati anapata kipaimara au uchungaji, nadhani hana haja ya kufanya malumbano ispokuwa kwenda kule moyo wake unapomtuma.
 

Mnataka tusali mfumo wa kukremisha ili muendelee kututawala kiroho? Soma vizuri na uelewe huo uzi.
Ulivyobatizwa komunio na kujiunga KKKT Hukufundishwa kushika amri za kanisa?
Kama unaona hazifai si uhame tu?
 
Ulivyobatizwa komunio na kujiunga KKKT Hukufundishwa kushika amri za kanisa?
Kama unaona hazifai si uhame tu?
Kwahiyo Amri za kanisa ndo zitakufikisha mbinguni na kukukuza kiimani? Think outside the box. Nyie ndo mnaoabudu viongozi wa dini instead of kuabudu Yule aliekupa uhai.
 
Kwahiyo Amri za kanisa ndo zitakufikisha mbinguni na kukukuza kiimani? Think outside the box. Nyie ndo mnaoabudu viongozi wa dini instead of kuabudu Yule aliekupa uhai.
Kutii mamlaka ni moja ya maelekezo ya KiMungu!
Hajazuiwa kuhubili, Viongozi wake wameona ni bora zaidi akienda kutumika na kwingine kunahitaji zaidi nguvu yake!

Hata kama ni mchezaji mzuri huwezi kubishana na kocha kufanyiwa sub!

Mungu yupo popote!
Wito wa kichungaji wa kimaro HAKUITWA ILI ATUMIKE kijitonyama peke yake!

Kuna waumini wengine inje ya hapo akubali kwenda kutumika!
Kiburi hakimsaidii!
 
Tusifike humu! Yule kahamishwa akatumike na kwingine!
Kwa mujibu wa barua kastopishwa na kapewa likizo ya lazima na akirudi aripoti jimboni tofautisha na kuhamishwa Chief.
 
Ni rahisi sana kufanya jambo na kuona uko sahihi lakini ni ngumu sana kukichunguza ulichokifanya na kuona kuwa umekosea. Kuna mmoja inabidi ajirudi, na sisi waumini tulivyo wanafiki hatuishi kuandika nyuzi kwenye mitandao lengo letu apatikane mshindi badala ya kupatikana suluhu [emoji3166][emoji3166][emoji848]
 
Mimi ni Muumini wake mzuri sana pale Kitonyama Mkesha wa Mwaka Mpya nilikuwa hapo na Mch.Kimaro ana Mafundisho mazuri sana hasa ya Ki Imani.

Ila kwenye hili...

Mch.Kimaro anapaswa kuwa na hekima ya ki Mungu sana kwenye hili lililotokea...

Ingewezekana hata ile kuaga angeaga kawaida tu kama Wachungaji wengine wanavyoaga kwenye Sharika zao wakipata Uhamisho ila ile kuaga ameonesha kuna uonevu kafanyiwa.(Ni Mtazamo wangu)

But yote kwa yote sijui nini kimetokea hadi kupelekea hayo..Nimuombee tu yamalizike salama na arejee kwenye kulisha Kondoo wake.
Nae Ni binadamu jmn Kuna kuteleza

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Haya mambo ya Vyeo yanaleta kutukuzwa watu badala ya Mungu. Kiasi kwamba mtu anajiona yeye Yuko juu ya wengine

Bora Mashahidi wa Yehova(JEVOVA's WITNESS) hawana upuuzi huu. Wote mnakuwa wanafunzi wa Biblia.
 
Naomba nianze kwa kuwapa pole waumini ambao walibarikiwa na mchungaji kimaro!

Kazi ya kitume ni kama mvua, inanyesha kwa wakati wake na kupisha kwa muda ili shughuli zingine zifanyike, mpate muda wa kupanda, kuvuna, na hata kuezeka panapovuja.

Yamkini mvua ya mahubiri ya mchungaji kimaro ilipendwa na wengi, ili stawisha imani za watu wengi, ili punguza joto kali la mizigo.

LAKINI Tusisahau mvua za namna hii kwa upande mwingine zina majanga yasiyoonekana bayana!

Yamkini kupitia mvua hii watu walizibua mitaro yao, yamkini mvua hii ilileta limonia,yamkini kuna mahali palivuja sana.

Hivyo mambo kama hayo huwezi kuyaelewea kama ukiitazama mvua kwa lengo la masika!

Mchungaji ELIONA KIMARO ANAWEZA KUWA NA SHIDA GANI?
Mimi siyo kiongozi wala muumini wa KKKT! Mimi bado natafta kanisa zuri hata humu jf niliwahi kuuliza kanisa gani zuri ili nikajiunge.

Hivyo Kwa uzoefu wangu na elimu yangu ndogo ya kuchunguza matukio kama haya ikiwemo migogoro ya kiimani, kijamii, mauaji, siasa na uchumi n.k

Naweza kusema mchungaji ELIONA KIMARO Ana sifa zifuatazo
  • Mchungaji kimaro analijua andiko analolihubiri
  • Mchungaji kimaro anawajua waumini anaowahubiri na shida zao
  • Mchungaji kimaro anaijua vyema jamii anayo ihubiri
  • Mchungaji kimaro hayumbishwi hasa pale anapokuwa kapanga jambo lake!
  • Mchungaji kimaro siyo msimamizi mzuri wa rasilimali na fedha za kanisa ( fedha ni rahisi kupotea mikononi mwake)
  • Mchungaji kimaro kwa kutambua karama yake anaitumia kuficha madhaifu mengine hasa kwenye matumizi ya fedha!
  • Kuna uwezekano mkubwa wa wa kuonywa lakini kwa kiburi cha kupendwa na waumini aliamini hagusiki!
  • Kwa karama yake ya kichungaji alipogundua viongozi wakuu wake wana jambo naye! Alianzisha semina nyingi za mafunzo ili atakapoitwa WAUMINI Waone kama kuna shida!
ELIONA KIMARO ni mchungaji mzuri sana! Na hili ndilo lengo la makanisa mengi ikiwemo kanisa hili la KKKT!

Lakini kwasababu kanisa lina hitaji uponyaji wa kiroho, kimwili na kiuchumi! Ni lazima VIONGOZI wake wafanye hivyo walivyofanya! Kumuhamisha kwasababu za ndani za kiuchumi! HAWAJAKURUPUKA

Hata viongozi wanaweza kuwa wanampenda sana ELIONA KIMARO Lakini haina budi kupisha eneo hilo linalohitaji usimamizi bora wa kiroho, kimwili na kiuchumi kwa mstakabali wa kanisa zima!

Ikiwapendeza viongozi wanaweza kumrudisha lakini awe chini ya usimamizi wa mchungaji mwingine!
Lakini kwa kutambua nguvu aliyonayo kimaro kuwa chini ya mtu palepale Kijitonyama ni changamoto!

Huenda viongozi wameona ni bora sasa akatumike na kwingine.

Kama lengo lingekuwa moja tu kuinjilisha huenda wangemuacha.

Lakini kwasababu linahitaji kukua zaidi kiroho na kiuchumi, ndiyo maana VIONGOZI WAMEFIKIA UAMUZI HUU.

Endeeleeni kusubiri taarifa ya KKKT lakini nauhakika haiwezi kuwa mbali na maoni yangu.

Wewe unampenda kimaro, Viongozi wanampenda kimaro lakini tusisaha Kanisa la KKKT ni kubwa kuliko Kimaro.

Tuliokaribu naye tumsihi asiwaone wabaya viongozi, alipokee hili kwa wema na akatumike popote atakapopangiwa.

Asikuruouke KUHAMA au KIANZISHA KANISA ATAPOTEA, Atambue kwamba mbio zake ni kama samaki baharini,

Kimaro anaonekana kupiga mbizi za kuvutia akiwa ndani ya KKKT, akitoka inje ATAPOTEA!
KKKT ni bahari inayomfanya a-shine!
Asithubutu kutoka Bali atii mamlaka yake ilivyoamua!

Mapadri wa kikatoliki huhamishwa, wachungaji KKKT huhamishwa, Kimaro asione ajabu kuhamishwa.

Yesu alihubiri Galilaya, Yerusalem, Kapenaumu hata kirindini kwa wavuvi kanisa!

Kwanini KIMARO ang'ang'ane pale pale kijitonyama na sio kwingine? HAMJIULIZI HILO?

JF ukweli na uwazi.

View attachment 2484976
wewe ni malaasusa ndo kawaida yako kuta nimonia limonia
 
Sijui kwanini siku hizi wakristo umehamia kwenye kuamini watu badala ya kanisa.

Yani mijitu mizima imeandamana eti inamtaka mchungaji wao.
Amesema muumini wa Kijitonyama si muumini wa Kimaro. Read between the lines
 
Baadhi ya maaskofu wanavuruga kanisa. Angalia kule Rukwa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika Askofu Mwa... alivyovuruga kanisa. Mbeya Askofu Mwa... nae kavuruga. Sasa Dayosisi ya Mashariki na Pwani mwingine tena Askofu Ma... amelianzisha. Nyie akina Mwa... kutoka Mby Mungu anawaona
 
Back
Top Bottom