Klabu bingwa Afrika: As vita club 0-1 Simba dimba la Stade de Martyrs 12/2/2021

Klabu bingwa Afrika: As vita club 0-1 Simba dimba la Stade de Martyrs 12/2/2021

Naaaaam Barabara kabisa,

Ndugu wadau wa Michezo wa hapa Jamiiforums na kwingineko karibuni katika Live updates(Matukio Mubashara) kutokea hapa Kinshasa katika Dimba la Stade De Martyrs, uwanja wa nyumbani wa Timu ya AS VITA CLUB ambapo kuna "patashika nguo kuchanika" au unaweza kusema kipute cha ligi ya mabingwa hatua ya makundi katika Kundi A baina ya Wenyeji AS VITA ya hapa Congo na Simba Sports Ckub kutokea Tanzania.. Mechi hii itachezwa Saa Mbili usiku ( Kwa saa za hapa DR Congo na Saa 4 usiku kwa saa za Tanzania)

Kikosi cha Simba kilisafiri kutoka Tanzania jumanne kuja hapa DR Congo na kilitua salama, kikipokelewa salama na wenyeji na jopo la viongozi. Walikaribishwa na wakaendelea na mazoezi siku inayofuata.. Wapinzani wengine kwenye kundi hili A, ni Al Ahly ya Misri na El Mereikh ya Sudan ambao nao watapapatuana keshokutwa 16/2/2021

Kuelekea Mchezo huu Muhimu kwa timu zote, Timu ya Simba itawakosa nyota wake wanne kwa sababu mbalimbali ambao ni Erasto Nyoni/John Bocco (Majeruhi) David Kameta (Timu ya taifa U-20) Pamoja na Perfect Chikwende(Sheria za CAF hazimruhusu). Kocha wao Didier Gomes amesema kuwa wanahitaji kushinda magoli mengi kadiri wawezavyo kulingana na nafasi wapatazo ili kujiweka salama kwa mchezo ujao (Japo anajua Kutoka pale ni ngumu)

Kwa upande wa AS VITA kocha wao Florent Ibenge amesema kuwa itakuwa ni mechi ngumu baina ya timu hizo na amesema chochote kinaweza kutokea, ila amejizatiti kimbinu kushinda mechi hiyo muhimu

Kikosi cha As Vita kilichoibugiza Simba mabao matano kwa sufuri sio hiki kinachocheza leo kwa kuwa wachezaji wengi wameuzwa akiwemo Makusu, Tinombe Mukoko, Tuisila Kisinda, Ngoma n.k na Kile cha Simba sio hiki japo kuna baaadhi ya wachezaji walikuwepo wakiwemo Aishi Manula, Chama Cleotus, Kagere, Mkude, Wawa, Dilunga na wengineo


Kumbukumbu za Head to Head

Hii sio mara ya kwanza kwa timu hizo kucheza, huku Simba ikienda na 'kumbukumbu mbaya' ya kuchabangwa "Hamsa" yaani goli 5 bila majibu mnamo mwaka 2019.

2012 : Simba 1 : 1 As Vita Club

January 19 2019 AS VITA 5 : SIMBA 0
Machi 16, 2019 SIMBA 2 : AS VITA 1

Kwenye kundi lao Simba alifanikiwa kupita ila alitolewa hatua ya Robo fainali

Vikosi vya Timu zote mbili vitawekwa hapa kadiri muda utakavyokwenda......

--------------‐---‐-----------------------

Updates on starting XI (Huenda ikawa/Sio Rasmi)

AS VITA CLUB; Assie Koua, Ebunga Simbi, Makabi Lilepo, Masasi, Fiston Mayele, Medjo Simon Loti, Ouattara, Shabani Djuma, Tulengi Sindani, Wamba Merveille, Yacouba Sidi

SIMBA SPORTS CLUB; Manula, Kapombe, Zimbwe, Wawa, Mkude,Lwanga, Chama, Bwalya, Miquissone,
Mugalu, Kagere

Vikosi rasmi vitawekwa vikishatangazwa hapo baadae
----------------------------------------
Confirmed Mechi kwa watakaotizama itaoneshwa saa 4 usiku kupitia Channel ya ZBC2 inayopatikana kupitia Kisimbuzi cha Azam Tv
View attachment 1700848

Wale wa DSTV CHANNEL NAMBA 270 KBC 1
Simba nguvu moja
 
Kikosi cha Simba
simbasctanzania-20210212-0001.jpg
 
Àikiwemo huyu Dada Jove ...aliyeanzisha Uzi hiu
Ajabu ni kwamba deportivo de la utopolo a.k.a Nyani a. k. Vyura wa jangwani ndo wenye presha na hii mechi kuliko Mfalme wa nyika SIMBA ....

Simba nguvu moja....ushindi upo wala sina hofu na kikosi chet
 
Kikosi cha AS VITA vs SIMBA
AS Vita Club [emoji1078] lineup:

Simon Omossola (GK) [emoji1062]
Djuma Shabani [emoji1078]
Ousmane Ouattara [emoji1081]
Vivien Assié Koua [emoji1081]
Ernest Luzolo Sita [emoji1078]
Papy Tshishimbi [emoji1078]
Amedé Masasi [emoji1078]
Sidi Yacoub [emoji1163]
Jéremie Mbuyi [emoji1078]
Glody Mokabi Lilepo [emoji1078]
Fiston Mayele Kalala [emoji1078]

#TotalCAFCL #ASVSSC
 
Bado takribani nusu saa kipute kianze,

Vikosi vimeshatoka, je nini utabiri wako? SIMBA ANASHINDA, AS VITA ANASHINDA AU WATAGAWANA POINT?
 
Back
Top Bottom