Lee
JF-Expert Member
- Jul 31, 2013
- 43,973
- 150,463
Mkuu naenjoy kitu hd muhim tusifungweMzee baba unakula mema ya nchi tartiiibu kabisa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu naenjoy kitu hd muhim tusifungweMzee baba unakula mema ya nchi tartiiibu kabisa.
Kweli kabisa.Mkuu naenjoy kitu hd muhim tusifungwe
Hahahahahaha mkuu muhim kitu HD mengine mbele kwa mbeleNaona mko na Canal hapo mnakula tu kifaransa
Dk ta 25 kitu bila bilaJoseverest leta apdates,mbona kimya sana mzee baba?
Naipataje canal + mkuu?Hahahahahaha mkuu muhim kitu HD mengine mbele kwa mbele
Mpira naupata kwa uzuri kupitia maandishi ya Joseverest hapahapa JamiiForumsNaaaaam Barabara kabisa,
Ndugu wadau wa Michezo wa hapa Jamiiforums na kwingineko karibuni katika Live updates(Matukio Mubashara) kutokea hapa Kinshasa katika Dimba la Stade De Martyrs, uwanja wa nyumbani wa Timu ya AS VITA CLUB ambapo kuna "patashika nguo kuchanika" au unaweza kusema kipute cha ligi ya mabingwa hatua ya makundi katika Kundi A baina ya Wenyeji AS VITA ya hapa Congo na Simba Sports Ckub kutokea Tanzania.. Mechi hii itachezwa Saa Mbili usiku ( Kwa saa za hapa DR Congo na Saa 4 usiku kwa saa za Tanzania)
Kikosi cha Simba kilisafiri kutoka Tanzania jumanne kuja hapa DR Congo na kilitua salama, kikipokelewa salama na wenyeji na jopo la viongozi. Walikaribishwa na wakaendelea na mazoezi siku inayofuata.. Wapinzani wengine kwenye kundi hili A, ni Al Ahly ya Misri na El Mereikh ya Sudan ambao nao watapapatuana keshokutwa 16/2/2021
Kuelekea Mchezo huu Muhimu kwa timu zote, Timu ya Simba itawakosa nyota wake wanne kwa sababu mbalimbali ambao ni Erasto Nyoni/John Bocco (Majeruhi) David Kameta (Timu ya taifa U-20) Pamoja na Perfect Chikwende(Sheria za CAF hazimruhusu). Kocha wao Didier Gomes amesema kuwa wanahitaji kushinda magoli mengi kadiri wawezavyo kulingana na nafasi wapatazo ili kujiweka salama kwa mchezo ujao (Japo anajua Kutoka pale ni ngumu)
Kwa upande wa AS VITA kocha wao Florent Ibenge amesema kuwa itakuwa ni mechi ngumu baina ya timu hizo na amesema chochote kinaweza kutokea, ila amejizatiti kimbinu kushinda mechi hiyo muhimu
Kikosi cha As Vita kilichoibugiza Simba mabao matano kwa sufuri sio hiki kinachocheza leo kwa kuwa wachezaji wengi wameuzwa akiwemo Makusu, Tinombe Mukoko, Tuisila Kisinda, Ngoma n.k na Kile cha Simba sio hiki japo kuna baaadhi ya wachezaji walikuwepo wakiwemo Aishi Manula, Chama Cleotus, Kagere, Mkude, Wawa, Dilunga na wengineo
Kumbukumbu za Head to Head
Hii sio mara ya kwanza kwa timu hizo kucheza, huku Simba ikienda na 'kumbukumbu mbaya' ya kuchabangwa "Hamsa" yaani goli 5 bila majibu mnamo mwaka 2019.
2012 : Simba 1 : 1 As Vita Club
January 19 2019 AS VITA 5 : SIMBA 0
Machi 16, 2019 SIMBA 2 : AS VITA 1
Kwenye kundi lao Simba alifanikiwa kupita ila alitolewa hatua ya Robo fainali
Vikosi vya Timu zote mbili vitawekwa hapa kadiri muda utakavyokwenda......
--------------‐---‐-----------------------
Updates on starting XI (Huenda ikawa/Sio Rasmi)
AS VITA CLUB; Assie Koua, Ebunga Simbi, Makabi Lilepo, Masasi, Fiston Mayele, Medjo Simon Loti, Ouattara, Shabani Djuma, Tulengi Sindani, Wamba Merveille, Yacouba Sidi
SIMBA SPORTS CLUB; Manula, Kapombe, Zimbwe, Wawa, Mkude,Lwanga, Chama, Bwalya, Miquissone,
Mugalu, Kagere
Vikosi rasmi vitawekwa vikishatangazwa hapo baadae
----------------------------------------
Confirmed Mechi kwa watakaotizama itaoneshwa saa 4 usiku kupitia Channel ya ZBC2 inayopatikana kupitia Kisimbuzi cha Azam Tv
View attachment 1700848
Wale wa DSTV CHANNEL NAMBA 270 KBC 1
--------------------‐---------------------
Vikosi Rasmi ( CINFIRMED)
Simba XI: Manula Aishi, Kapombe Shomari, Mohamed Hussein (Nahodha), Onyango, Wawa Sergi, Lwanga Thadeo, Chama Cleotus, Mzamiru Yassin, Mugalu Kopa, Bwalya Larry na Miquissone Luis
Substitutes: Kakolanya, Gadiel, Kennedy, Ndemla, Kagere, Morisson, Kahata
AS VITA XI:
AS Vita Club [emoji1078] lineup:
Simon Omossola (GK) [emoji1062]
Djuma Shabani [emoji1078] (Captain)
Ousmane Ouattara [emoji1081]
Vivien Assié Koua [emoji1081]
Ernest Luzolo Sita [emoji1078]
Papy Tshishimbi [emoji1078]
Amedé Masasi [emoji1078]
Sidi Yacoub [emoji1163]
Jéremie Mbuyi [emoji1078]
Glody Mokabi Lilepo [emoji1078]
Fiston Mayele Kalala [emoji1078]
#TotalCAFCL #ASVSSC
_______________________________________
Mpira utaanza muda wowote kuanzia sasa, vikosi rasmi vinaingia dimbani, wanajipanga kwa picha na matukio mengine
Kickoff
00 + 1' Mpira umeanza rasmi na Simba ndio wanasukuma 'gozi la ng'ombe' kutokea kusini kuelekea Vita club waliopo lango la kaskazini
3' Simba wanalisakama lango la Vita ila mipango inakwama.. Vita wanarudi mchezoni... wanapata faulo inapigwa inaokolewa
7' Simba wanacheza vizuri, wanaonana vyema ila mipango yao inatibuliwa pale..aiseee
8' Vita wanapata faulo....inapigwa inaenda nje pale daaah
10' Kona fupi kwa Vita.. wanacheza vizuri ila inatoka nje Papy Tshishimbi anaitoa nje
13' Timu zote zashambuliana kwa Zamu kwa mashambulizi ya kushtukiza, Simba bado beki hazijatulia wakati huohuo Lwanga anafanyiwa faulo na Papy Kabamba, Papy anaonywa
17' Simva wanapata kona ya kwanza, wanaanzishiana fupi..inatolewa nje
20' luis Miquissone anashambulia lango la Vita, bahati mbaya anaushika mwamuzi anapuliza kipyenga..faulo
22' Miquison anatoa mpira inakuwa ni kona kwa Vita, mchezaji wa Vita anapiga kichwa mpira unatoka sentimeta chache langoni
25' Mpira umesimama Lwanga amechezewa faulu, anagangwa kidogo mpira unaendelea
Vp game imebalance au tumezidiwa,Dk ta 25 kitu bila bila
Asante sana, ninaona sasa.
Mda wote wanacheza nyuma kwao wanakabiwa kwao hawawezi kutengeneza nafasi hata wakiwa na mpiraPasi nyingi za Simba hazifiki kwa walengwa.. hii itaicost Simba
Mkuu kingamuz chao kinapatikanaNaipataje canal + mkuu?
Vitoto kama Messi au Mo Salah?Nilichogundua, wachezaji wa AS Vita wana miili mikubwa kiasi kwamba Simba wanaonekana kama vitoto uwanjani[emoji4]