Komodo dragon ndio mnyama hatari zaidi kuliko Black mamba (koboko), Simba, Mamba, Tiger na wanyama wengine wa aina hiyo

Huyu namwogopa hata kumwangalia kwenye tv yaan anakujeruhi kidogo tu ili mradi meno yake yagusane na dam yako. Anakuwa anakufuatilia kwa mbali hadi hapo utakapomaliza nguvu na kuanguka atakaa hapo anakula hata kwa siku nne mpaka akumalize
Mkuu hili dudu linakula kwa dakika 15 linakuwa lishakumaliza wewe, nguo zako na viatu vyako kwa pamoja. Ndio mnyama anaekula chochote kile kilichopo mbele au karibu yake pale anapokuwa na njaa.
 
Its all about timing hata siafu au kirusi kinaweza kumuondoa myama yoyote yule
 
Lakini ukimiangalia unaweza hata kimbia kabla hajakuuma ukapona sasa kwa black mamba utakimbiaje akisha kuweka kwenye 18 zake?
Yah Ila black mamba ukifuga mangoose nyumbani kwako hatii mguu. Ila hili dubwasha hata ufuge mangoose 20 kwanza ataanza na hao mangoose kuwatafuna kisha atakuja kumalizana na wewe πŸ˜€πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.
 
Mziki wa black mamba huyu hawezi kuukutia hata kidogo.

Kwanza nikimuona naweza kimbia nikapona, je black mamba ukimzingua unaweza kimbia ukapona?
 
Mziki wa black mamba huyu hawezi kuukutia hata kidogo.

Kwanza nikimuona naweza kimbia nikapona, je black mamba ukimzingua unaweza kimbia ukapona?
Mkuu sikatai kwamba black mamba ni rahisi mno kumu attack binadam kuliko hili dubwasha. Ila kinachofanya huyu awe hatari ni kwa sababu ana uwezo wa kuangamiza kiumbe chochote kilichopo mbele yake. Tofauti na black mamba ambae anaweza kudhibitiwa na mnyama mdogo kama mangoose. Yan black mamba hata akifanikiwa kung'ata mangoose bado mangoose ataendelea kufanya kile anachotaka kufanya kw black mamba hadi atamuuwa. Ila hili kwanza anaweza kumtafuna huyo mangoose bila hata kujipa hasara ya kutumia sumu yake.
 
Ili ni lioga tu halafu halina speed wala stamina kinachompaisha ni mabakteria waliopo kwenye mate yake ikitokea limekuuma

Labda likute umelala Mara nyingi ni Lila mizoga na wanyama wadogo wadogo
Yako ma apex predator kama tiger,brown bear

Akipigwa kucha mbili na Tiger kwishaaa iyoooo
 
Wanapatikana wapi hao wanyama kwa sasa kwenye hii dunia?

Vipi binadamu ni kawaida kuwindwa na huyo mnyama au inakuwa kama bahati mbaya tu kupitiwa?
Hakuna kiumbe anayewinda binadamu. Ukikuta binadamu ameshambuliwa ni bahati mbaya tu.

Kiumbe gani anayekula nyama ya binadamu ?
 
Tukiachana na hayo mengine ya speed nk ambayo kila mnyama kapewa namna yake ya kutembea na kukimbia. Tuje kwenye swala la Tiger au Simba kumu attack huyu jamaa.

Hapa kuna mambo mawili tofauti ambayo haukuyafahamu. Mambo hayo ni:
1) Tiger au Simba akimu attack komodo ni lazima atahitaji amfanye kitoweo baada ya attack. Kwahiyo hapo tunaona kabisa attack ya mnyama Tiger au Simba itasababisha vifo vya wote wawili, yani komodo na yeye tiger au simba kwa sababu ya venom (sumu) kali iliyo katika mwili la hili dubwasha.
Ikitokea Tiger au Simba ndo kaliwa timing na komodo basi hapo predator huyo atakuwa hana ujanja wa kukwepa kuwa kitoweo cha hili dudu.
 
Bora uhamishie majeshi humu,kule ulikuwa umepotea njia,Bora umerudi kwenye reliπŸ€”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…