Korea Kaskazini yatupa makombora 10 ya "Ballistic" kujipima uwezo wakati huu wa vita ya Mashariki ya Kati

Korea Kaskazini yatupa makombora 10 ya "Ballistic" kujipima uwezo wakati huu wa vita ya Mashariki ya Kati

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440
1773616648948.png

Vikosi vya Marekani na Korea Kusini vikiwa katika matayarisho ya mazoezi ya pamoja ya kuvuka mto katika wilaya ya YeonCheon. Picha na Reuters.


Siku ya Jumamosi ilopita Korea Kaskazini ilitupa makombora yapatayo 10 ya Ballistic katika kutunisha musuli khasa katika kipndi hichi cha mgogoro katika eneo la Mashariki ya Kati. Pia kitendo hichi kilikuwa ni kujibu mazoezi ya kila mwaka ya kijeshi yalokuwa yakifanywa kati ya vikosi vya Marekani na vile vya Korea Kusini.

Mazoezi hayo yamepangwa kufanyika kati ya terehe 9 na 19 mwezi huu wa March na Korea Kaskazini yahesabu kuwa hayo ni mazoezi ya kutaka kuivamia. Mazoezi hayo ya siku 11 yaitwa Freedom Shield ambayo ni sehemu ya mazoezi mawili ya kila mwaka.

Korea Kusini ambayo ni nchi hasimu na Korea Kaskazini imesema imehesabu idadi ya makombora hayo na kuthibitisha kuwa yalikuwa 10 na yalitupwa kutokea katika wilaya ya Sunan iliyoko mashariki ya mji mkuu wa Pyongyang kuelekea katika bahari ya Mashariki au East Sea.

Makombora hayo ya Ballistic yalitupwa umbali wa kilomita 350 yakiinukia katika mwinuko wa kilomita 80 na kulala kwenye mteremko wa kilomita 340 kabla ya kuangukia baharini na afisa mwandamizi wa jeshi la Korea Kusini alisema wao walikuwa wamejitayarisha kujibu aina yoyote ile ya uchokonozi.

Ni miaka mitatu imepita sasa tangia mara ya mwisho Korea Kaskazini irushe makombora hayo mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2022 ambapo makombora ya masafa mafupi 7 na mikia (Projectiles) ipatayo 16 pamoja na makombora mengine ya kutokea ardhini kwenda angani (Surface to air missiles).

Wachambuzi wengi waweza kutafsiri hatua hiyo ya Korea Kaskazini ni katika kusoma vita inoendelea kati ya Iran na Marekani ikishirkiana na Israeli. Korea Kaskazini yaangazia katika kujipima uwezo wake na utayari wa kujibu mashambulizi yoyote na kupima uimara wa mitamb yake ya ulinzi wa anga (air defence systems) na namna ya kuhimili mashambulizi ya ghafla (pre-emptive strikes).

Katika miezi ya hivi karibuni Korea Kaskazini imekuwa ikijishughulisha ya uboreshaji wa jeshi lake la majini kwa msaada ya Russia na hivyo baad aya kuona jinsi Marekani ilivyoweza kuzamisha manowari nyingi za Iran, Pyongyang tiyari wamekuwa wakijitayarisha kutupa makombora ya ballistic ya masafa marefu ambayo yataweza kufika zilipo meli za Marekani mahala popote pale endapo manowari za nchi hiyo zitashambuliwa.

Bila kutaja moja kwa moja mgogoro wa Mashariki ya Kati dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Yo Jong amesema mazoezi ya Marekani na Korea Kusini yahatarisha usalama wa eneo zima la rasi ya Korea, katika kipindi hiki ambapo usalama wa kidunia na mifumo yake vyaporomoka kutokana na vitendo vonofanywa na waharibifu wa kimataifa.

Vyanzo: Independent, Reuters na AP.
 
Si wayapeleke iran yakafanye kazi za maana? Hayo makombora yao yanasumbua tu samaki, wanajishtukia tu, marekani hapigani vita ya hasara, hana shida na makaa ya mawe, hata guruneti moja la marekani likidondoka pyongyang itakuwa ni hasara tu, hakuna cha kuchukua huko, wa relax.
 
Back
Top Bottom