Mtaalamu wa anga kapteni rubani wa ndege anatoa maoni yake :
Boeing 737 : Hakuna magurudumu yaliyotoka iweze kutua salama | Yagonga Ukuta wa zege
View: https://m.youtube.com/watch?v=w1r8dl4RqMw
Hapa ninafahamu taarifa za awali tu na haya ni maoni yangu tu kuhusu Ajali anasema rubani mbobevu katika kuchambua ajali hii.
Kuna maswali mengi ambayo hayawezi kujibiwa kwa wakati huu kwa hivyo tunahitaji data zaidi na timu ya uchunguzi wa ajali za ndege itajua kilichotokea.
Ndege ya shiriksa la ndege la
Jeju aina ya muundo wa
Boeing 737-800, yenye usajili
HL8088 ikifanya safari ya
7C-2216 kutoka Bangkok (
Thailand) hadi Muan (
Korea Kusini) ikiwa na abiria
175 na wafanyakazi
6, ilitua kwenye barabara ya uwanja wa ndege wa
Muan 19 saa 09:03L (00:03Z) ikiwa na inaonekana gia zote za magurudumu ya ndege
hazijateremshwa, ilitua katika njia ya kurukia ndege kisha kuteleza kwa kutumia
tumbo la ndege (kwenye fuselage) na
injini bila magurudum,u kisha kuparamia uzio wa zege
Mita 300 (futi 1000) baada ya kupitiliza sehemu ya mwisho ya barabara ya ndege na kupasuka kisha kulipuka moto mkubwa.
Watu wawili wameokolewa wakiwa hai, miili 120 imeopolewa, hakuna matumaini kwa walionusurika zaidi
Kikosi cha uokoaji cha Zimamoto cha uwanja wa ndege wa
Muan kiliripoti hitilafu ya gia ya kutoa magurudumu ya kutua, ambayo huenda ilisababishwa na kugonga mnyama ndege angani, hivyo ilisababisha ndege kuhairisha kutua na kuamua kuzunguka.
Kisha baada ya mzunguko ndege hiyo ilijaribu kutua tena katika hali mbaya ya hewa. Hata hivyo, sababu halisi inahitaji kuamuliwa na uchunguzi wa pamoja unaofuata.
Mamlaka iliripoti manusura wawili, wa kiume na wa kike, wote wafanyakazi wa ndani ya ndege , waliokolewa wakiwa hai na majeraha makubwa kutoka kwenye sehemu ya nyuma iliyopo katika mkia wa ndege hiyo.
Wizara ya Uchukuzi ya
Korea Kusini iliripoti kuwa kulikuwa na maswala kadhaa ikiwa ni pamoja na kuahirisha kutua na kuzungika angani kwa ndege hiyo na kuripotiwa hitilafu za zana za kutua, itachunguza kwa kina ili kujua sababu.
Wizara iliongeza baadaye, onyo la rubani kuahirisha kutua ndege lilitolewa saa
08:57L takriban dakika 6 kabla ya ajali, kama dakika moja baada ya mzunguko wa dharura wa ndege angani na kuonya wafanyakazi kutangaza
Meiday MeiDay saa
08:58L wakati wakikaribia mwisho wa kujaribu kutumia barabara ya
01, mnara ulitolewa kuruhusu ndege kutua kwenye njia ya kurukia mbadala jirani (19), hata hivyo ndege
Boeing 737 ilitua na kupata ajali dakika 5 baada ya kutangaza
kauli ya lugha ya dharura ya sekta ya
anga maaru
Mayday.
Kinasa sauti cha safari ya ndege kimepatikana, kinasa sauti kilichopo katika chumba cha marubani bado hakijapatikana.
Shuhuda mtazamaji mmoja akiwa ardhini aliripoti kwamba ndege iliruka kati ya kundi la ndege wanyama, sauti mbili au tatu za pop kama kizibo cha soda ya gesi kufunguliwa zilisikika kana kwamba ndege wanyama hao angani kuvyonzwa, walimezwa kwenye injini ya ndege Boeing 737 , moto ulionekana kutoka kwa injini ya mkono wa kulia.
Ndege hiyo Boeing 737 ilipanda kidogo lakini ilionekana kushindwa kupanda zaidi na kuelekea kupoteza mwinuko. Wakati ndege ilimshinda rubani, ilikuwa na vifaa vya kutua yaani magurudumu chini.
Hospitali iliripoti mmoja wa wahudumu wa ndege hiyo alijeruhiwa bega na kichwa, lakini alikuwa na fahamu na aliweza kutembea. Data ya ADS-B iliyopokelewa kutoka kwa ndege ilikoma ikiwa futi 900 angani saa 08:58L (23:58Z Des 28th) ilipokuwa inakaribia njia ya 01 - safari za awali za ndege zilipokelewa hadi transponder ilipozimwa kwenye
aproni.
Video hizo ikiwemo hapo juu zinaonyesha ndege hiyo ilikuwa ikiteleza kwenye barabara ya namba 19 ya kutua ndege kabla ya kujibamiza katika uzio wa zege