King of software usifananishe na vioo vya kijani ,samsung zina teknolojia ya zamani ,kawekeza kwenye hardwares.
Samsung cha ajabu ana custom software nzuri kuliko clean Android ya Pixel. Anachokosea Google ni kutoa software update ya mapema kabla Androids nyingine zote hazijapata. Huwa anamcheleweshea Samsung, na pia Pixel zina software support ya miaka mingi zaidi.
Samsung ana AI nzuri sana inaizidi mbali ya Google Pixel.
Kwenye vioo, Samsung anatengenezea hadi Apple wakati Google hajui kutengeneza vioo na hajawahi kuwa na vioo vizuri kumzidi Samsung iwe kwenye nits, peak, resolution, colour. Oppo mwenyewe anamzidi mbali Pixel.
Ili huyo Samsung afanye kazi lazima apate huduma za Google , Google pixel ni level nyingine ... Google teknolojia yake ya IA ni level nyingine ,inafunika takataka zote za Samsung.
Google Pixel na Google ni vitu tofauti vya Alphabet Inc. Unachofanya hapa ni sawa na kusema Apple ni sawasawa na iPhone.
AI ya Google haijaribu hata kuikaribia ya Samsung.
Samsung ana foldables na flip phones hazishikiki na yeyote sasa hivi sokoni. Samsung Galaxy Z Fold 7 hamna kenge yeyote kwenye soko anamkaribia. Ukijumlisha kwenye wembamba, processor, charge, camera, wepesi, kudumu, ubora wa kioo, uimara na ubora wa hinges, mikunjo ya kioo, build quality na materials. Hamna mpuuzi kwenye soko la simu duniani anakaribia Galaxy Z Fold 7. Sasa Google Pixel 9 Pro Fold ndio ya kulinganisha na Z Fold 6, mbingu na ardhi!
Google hawajawahi toa simu yenye pen. Tafuta S25 Ultra uone pen yake ilivyo. Simu kwanza nyepesi sio nzito kama li Pixel 9 Pro XL liilivyo.
Google chip yao ya Tensor ni less powerful na ina matumizi mabaya ya umeme. Na haifanyi task nzito sana simu inachemka na hata kwenye AI inapwaya. Samsung wanatumia latest Snapdragons kwenye flagships zao.
Pixel zina camera nzuri ukipiga, sasa share kwenye simu nyingine au share na social network au piga picha za biashara post mtandaoni uone. Hapo ndio watu wanakuja kutumia iPhones.
Kumbuka Google pixel zinauzwa kuputia thirdy party companies na vendors ,hawana promote ila uwezo unajieleza.
Mtu yeyote anayejua simu hawezi linganisha flagship ya Samsung na ya Pixel, Samsung kwa sasa hashikiki na yeyote. Hata wearables za Samsung zinazidi mbali za Pixel.
Pixel kwenye simu ashindane na kina Huawei, Oppo, Xiaomi. Kwa Samsung anashindwa pambano.