Google wanatumia approach ya Apple hawakimbizani na namba, wanajenga ecosystem inayoshikana/inayoendana..
kama mtu anatafuta gaming powerhouse , pixel huenda si chaguo bora. Lakini kama unatafuta simu iliyo focus na AI driven features na integrated AI experience iliyo bora, usability ya hali ya juu, simu iliyo optimized vizuri, na yenye kamera kali basi chukua pixel...
Hivyo, google hawakulenga raw power bali kwa matumizi waliyoazimia ambapo hawakuhitaji processor yenye cores nyingi au yenye specs za juu kuliko nyingine zilizopo sokoni...
Kumbuka pia Tensor haikutengenezwa kama bidhaa ya kibiashara kama Snapdragon. Qualcomm wanatengeneza Snapdragon kwa ajili ya watengenezaji mbalimbali kama Samsung, Xiaomi, OnePlus, n.k. kwa hiyo lazima iwe chip ya matumizi ya kila mtu, yenye raw power kubwa, specs kubwa na scalability, kwa sababu inahitajika kwenye simu za bei ya chini hadi za flagship...
Lakini Google hawakutengeneza Tensor kwa ajili ya kuwauzia wengine. Tensor ni tailor made kwa Pixel kwa mahitaji ya Google wenyewe, kwenye ecosystem yao. Hii inawapa uhuru wa ku prioritize mambo wanayohitaji zaidi kama on device AI, security , camera processing n.k badala ya kukimbizana na namba za benchmark au gaming fps....
Qualcomm lazima watengeneze chip itakayo hudumia vifaa tofauti kama Pixel, Samsung, Xiaomi n.k kwa hiyo lazima iwe na kwa matumizi yote. Lakini Tensor ni ya Pixel tu, na imetengenezwa mahsusi kwa kile Google wanataka , niseme ni kama CPU iliyokuwa customized kwa ajili ya ecosystem yake, si bidhaa ya soko huria...
Ni kweli samsung wanatengeneza tensor lakini wao ni manufacturer na sio designers, kumbuka hata Android OS ambayo Samsung hutumia kwenye kila simu yao inatengenezwa na Google...