Kosa Hili Liliwagarimu Samsung, Google Pixel Wakawapiga Bao

Hakuna mjinga wa kudamdanya labda atoke kijijini ,huko mimi ni fundi simu ..Hayo Masamsung ni bomu ,simu la mil 2 inatoka mistari kisa update ...Imetoka ile trash ya kwanza niupdatw fresh mapaka pixel 6 ,nyie takataka zenu za kijani zinatoa mistari😂😂🥲
[/QUOTE]Mkuu ukiona Samsung inatoa mistari hiyo fake, Tatizo la Samsung spear zake ni gharama yani kioo kikipasuka tu gharama yake ni bora ununue Google Pixels mpya.
 
Google wanatumia approach ya Apple hawakimbizani na namba, wanajenga ecosystem inayoshikana/inayoendana..

kama mtu anatafuta gaming powerhouse , pixel huenda si chaguo bora. Lakini kama unatafuta simu iliyo focus na AI driven features na integrated AI experience iliyo bora, usability ya hali ya juu, simu iliyo optimized vizuri, na yenye kamera kali basi chukua pixel...

Hivyo, google hawakulenga raw power bali kwa matumizi waliyoazimia ambapo hawakuhitaji processor yenye cores nyingi au yenye specs za juu kuliko nyingine zilizopo sokoni...

Kumbuka pia Tensor haikutengenezwa kama bidhaa ya kibiashara kama Snapdragon. Qualcomm wanatengeneza Snapdragon kwa ajili ya watengenezaji mbalimbali kama Samsung, Xiaomi, OnePlus, n.k. kwa hiyo lazima iwe chip ya matumizi ya kila mtu, yenye raw power kubwa, specs kubwa na scalability, kwa sababu inahitajika kwenye simu za bei ya chini hadi za flagship...

Lakini Google hawakutengeneza Tensor kwa ajili ya kuwauzia wengine. Tensor ni tailor made kwa Pixel kwa mahitaji ya Google wenyewe, kwenye ecosystem yao. Hii inawapa uhuru wa ku prioritize mambo wanayohitaji zaidi kama on device AI, security , camera processing n.k badala ya kukimbizana na namba za benchmark au gaming fps....

Qualcomm lazima watengeneze chip itakayo hudumia vifaa tofauti kama Pixel, Samsung, Xiaomi n.k kwa hiyo lazima iwe na kwa matumizi yote. Lakini Tensor ni ya Pixel tu, na imetengenezwa mahsusi kwa kile Google wanataka , niseme ni kama CPU iliyokuwa customized kwa ajili ya ecosystem yake, si bidhaa ya soko huria...

Ni kweli samsung wanatengeneza tensor lakini wao ni manufacturer na sio designers, kumbuka hata Android OS ambayo Samsung hutumia kwenye kila simu yao inatengenezwa na Google...
 
King of software usifananishe na vioo vya kijani ,samsung zina teknolojia ya zamani ,kawekeza kwenye hardwares.
Samsung cha ajabu ana custom software nzuri kuliko clean Android ya Pixel. Anachokosea Google ni kutoa software update ya mapema kabla Androids nyingine zote hazijapata. Huwa anamcheleweshea Samsung, na pia Pixel zina software support ya miaka mingi zaidi.

Samsung ana AI nzuri sana inaizidi mbali ya Google Pixel.

Kwenye vioo, Samsung anatengenezea hadi Apple wakati Google hajui kutengeneza vioo na hajawahi kuwa na vioo vizuri kumzidi Samsung iwe kwenye nits, peak, resolution, colour. Oppo mwenyewe anamzidi mbali Pixel.
Ili huyo Samsung afanye kazi lazima apate huduma za Google , Google pixel ni level nyingine ... Google teknolojia yake ya IA ni level nyingine ,inafunika takataka zote za Samsung.
Google Pixel na Google ni vitu tofauti vya Alphabet Inc. Unachofanya hapa ni sawa na kusema Apple ni sawasawa na iPhone.

AI ya Google haijaribu hata kuikaribia ya Samsung.

Samsung ana foldables na flip phones hazishikiki na yeyote sasa hivi sokoni. Samsung Galaxy Z Fold 7 hamna kenge yeyote kwenye soko anamkaribia. Ukijumlisha kwenye wembamba, processor, charge, camera, wepesi, kudumu, ubora wa kioo, uimara na ubora wa hinges, mikunjo ya kioo, build quality na materials. Hamna mpuuzi kwenye soko la simu duniani anakaribia Galaxy Z Fold 7. Sasa Google Pixel 9 Pro Fold ndio ya kulinganisha na Z Fold 6, mbingu na ardhi!

Google hawajawahi toa simu yenye pen. Tafuta S25 Ultra uone pen yake ilivyo. Simu kwanza nyepesi sio nzito kama li Pixel 9 Pro XL liilivyo.

Google chip yao ya Tensor ni less powerful na ina matumizi mabaya ya umeme. Na haifanyi task nzito sana simu inachemka na hata kwenye AI inapwaya. Samsung wanatumia latest Snapdragons kwenye flagships zao.

Pixel zina camera nzuri ukipiga, sasa share kwenye simu nyingine au share na social network au piga picha za biashara post mtandaoni uone. Hapo ndio watu wanakuja kutumia iPhones.

Kumbuka Google pixel zinauzwa kuputia thirdy party companies na vendors ,hawana promote ila uwezo unajieleza.
Mtu yeyote anayejua simu hawezi linganisha flagship ya Samsung na ya Pixel, Samsung kwa sasa hashikiki na yeyote. Hata wearables za Samsung zinazidi mbali za Pixel.

Pixel kwenye simu ashindane na kina Huawei, Oppo, Xiaomi. Kwa Samsung anashindwa pambano.
 
Nmetoka kuuza pixel 8pro mwez ulopita sababu hii nkavuta zangu S24 ultra kioo mafuta
S24 ultra sikuielewa kabisa, simu ipo kama tofali sijui imekaaje, yaani design ni hovyo kabisa.. samsung wameishiwa ubunifu..

S24 ultra ukikurupuka utasema ni infinix au tecno...

iPhone kwenye designing nawanyooshea mikono, hata Pixel ameipiga chini Samsung..
 
Shule ni muhimu ,Google pixel zinauzwa kupitia third party na vendors ...Hata Samsung wanaweza kuziuza ..Soma kwanza mzee wa vioo vya kijani
Kulingana na hiyo shule yako, Pixel zikiuzwa kwa third party zinabadilika na kuwa itel au Motorola?

Na ni kampuni gani ambayo simu zake haziwezi uzwa na third party? Itaje.

Na ni outlet gani ya Samsung iwe online shop au physical inaweza uza simu za Google Pixel? Iko nchi gani hapa duniani?
 
Hata Oppo na Xiaomi ni nzuri kuliko Pixel
Xiaomi 15 Ultra is way better than Pixel 9 Pro XL
 
Tensor ni mabaki ya Exynos ya Samsung, in short Bill of material zaidi ya 50% ya Pixel ni Samsung.

Na Tensor is no where near Snapdragon/Mediatek/Exynos linapokuja suala la AI, ni marketing term tu kwamba Tensor ni AI focused. Tensor G4 imepitwa mara 3 na Soc ya mwaka juzi kama snapdragon 8 gen 3, na uki compare na so mpya kama 8 elite utofauti ni mkubwa mno. We UNAFKIRI kwanini Pixel AI zinakuwa processed online? Sababu Tensor NPU yake ni ndogo.

Sphpquantized
Google Pixel 9 Pro XL
Google Tensor G4
TensorFlow Lite NNAPI
37945577239
Samsung Galaxy S25 Ultra
Qualcomm Snapdragon 8 Elite
TensorFlow Lite QNN
6152719960998

Source

Kama unavyoona hapo unaongelea mara 2 mpaka karibia mara 9 Wa nguvu ya NPU baina ya Pixel 9(Tensor G4) na S25U (snapdragon 8 elite)
 
Na mimi naomba nikuulize. S24 Ultra inafanana na Tecno gani hiyo, au Infinix gani????
 
Subiri iPhone 17 series uone design ilivyo mbaya. Hasa iPhone 17 Air. 16 plain yenyewe sikubali camera island yake. Ila design mara nyingi ni upendeleo wa mtu lakini Samsung S25 Ultra na Z Fold 6 zina design nzuri sana.

Kwangu Pixel 9 series zina design nzuri ila 8 sio.
 
Hata Oppo na Xiaomi ni nzuri kuliko Pixel
Xiaomi 15 Ultra is way better than Pixel 9 Pro XL
Pixel 9 Pro XL ni flagship kubwa jinga.

Ina processor ya kawaida, processor yake inashindana na ka Nothing Phone 3 nao wameweka processor ya kipuuzi alafu wanaiita true flagship.
Wakati kina Oppo, Xiaomi, Vivo, Honor, Samsung flaships zao wanaweka Snapdragon 8 Elite yenyewe iko na Tensor mbaya kama Kirin ya Huawei mwenye sanctions.

Battery performance ya kawaida. Na watafiti wamegundua Samsung zinaongoza kudumu battery. iPhones na Pixels zina battery life life ndogo.

Siwezi sema Xiaomi moja kwa moja anamzidi Pixel kwa kulinganisha brands, ila kwa kulinganisha simu ni kweli Mi 15 Ultra inaizidi 9 Pro XL.
 
GSMArena iko kalikooo sahivi, pixels linanganisha na jamii ya tecno, infinix huko
 
We UNAFKIRI kwanini Pixel AI zinakuwa processed online? Sababu Tensor NPU yake ni ndogo.
Hapo unadanganya, simu zote zinafanya mchanganyiko wa on device na cloud AI..
Kwenye on device AI samsung anapigwa chini...
Call screening kujibu simu inafanyika live bila internet...

Voice typing unapotamka maneno, yanabadilishwa kuwa maandishi kwa kasi na usahihi..

Now Playing,kutambua muziki background , hii inafanyika kabisa offline...

Photo Unblur / Magic Eraser, inategemea on device AI..

Live Translate....

Hap unasemaje pixel inakuwa processed online ? kwa hivyo vitu hapo juu kufanya offline si mchezo, imagine ina recognize nyimbo ikiwa offline...

Kiufupi samsung amezidiwa kwenye on device AI..
 
Si mpenzi wa iPhone lakini kwenye designing Samsung S series ni kama wanafeli, S series haipewi heshima yake inayo stahili kama flagship, yaani ni kawaida kuikuta A series ina design ambayo itamfanya mteja aone S series ni ya kawaida akiilinganisha na A series...

Designing ya S series haistui kabisa.. haileti ule utofauti na upekee wa simu ambayo ni flagship ya kampuni..
 
Na mimi naomba nikuulize. S24 Ultra inafanana na Tecno gani hiyo, au Infinix gani????
Samsung kwa sasa hawazipi S series designs za kipekee na kuvutia, ni kawaida kwa mtu asiyejua simu akadhani A series ndio S series..

Tazama hapa chini..



Hapo juu kuna A55 na S24 sasa zitazame halafu jiulize ipi s24 ipi A55.. huku bei ya s24 ipo juu..

Hii hapa chini ni S25..


Jamaa wapo hovyo sana...
Walau s24 ultra walijitahidi kuitofautisha kwa ile square design.. japo na yenyewe imekaaa kama tofali yaani hovyo kabisa..
 
Ulichoandika hapo ni kitu kimoja ambacho ni urongo... Samsung hana uwezo wa kumzidi Google kwenye AI hata miaka buku ijayo ...Acha uongo.

Google is a today's deal ,imejengwa kwenye misingi ya kisasa na iko strong kwenye upande wa software ,hakuna simu ya Android inagusa ...Anauza brand moja yenye toleo moja sio jamaa yako anatoa simu kila siku kama nguo mpaka zinarudishwa dukani.

Unaongelea customization za kulazimishwa na apps za uchafu nyingi.
 
Mkuu una elimu ya Simu au umesimuliwa tu?

Pole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…