Kosa kubwa alilolifanya Hayati Magufuli ni kutokuelewa utofauti wa adui na mpinzani

Kosa kubwa alilolifanya Hayati Magufuli ni kutokuelewa utofauti wa adui na mpinzani

Haya wengi tuliyasema wakati akiwa hai, kwenye kilele cha urais wake. Tulimwambia aangalie sana, wapinzani wake kama kina Lissu, ni watu wanaompenda sana na wanaanika upungufu wake ili arekebishe. Tukamwambia maadui wake wakubwa wako CCM na wengi ni wale wanaomwimbia mapambio ya kumtukuza. Hakusikia sauti zetu.
Hata Mama tunamwambia Katiba Mpya pekee ndio itakayompa mafanikio. Akishupaza Shingo atamaliza hivi hivi ataishia kutengua na kuteua tu.
 
Ulichokiona wewe siyo tulichokiona sie.

Sie tulimwona matendo yake na maneno tukajua alimaanisha alichosema.
Kupora fedha za mfuko wa korosho na korosho za wakulima ndio ulichokiona, ama ni tofauti na Mimi nilichoona?
 
Alikuwa hana akili
Uroho wa madaraka huondoa akili; ukianza tu ugonjwa huu akili inakufa. Embu tujiulize huu ni muhula wa pili au wa kwanza kwa uongozi huu.
Kupata jibu la swali hili kama ugonjwa umekuathiri, hutaweza jibu kwa usahihi mana akili yako itakuwa imeharibika pamoja na kuwepo miongozo yote ya katiba na kanuni za uongozi nchini. Eeh mwenyezi Mungi linusuru taifa letu.
Wachache sana wasioathirika na virus huyu hatari watanielewa. Kusaidia tu, hii ni awamu ya 5 inamalizika ya Magufuri, anayebisha aniambie rais huyu kachaguliwa lini nukta
 
Katika MAISHA ya siasa unabidi kuelewa ubora wako unategemea na ubora wa mpinzani wako.

Unapomgeuza mpinzani kuwa adui unabidi kujua unaenda kujiua na kujiangamiza.

Adui -ni yule anayepambana kukuondoa usiwepo

Mpinzani-ni yule anayetazama weakness zako na kuzi-expose ili uzifanyie kazi.

Ukichanganya hizo falsafa utaumia Sana katika siasa.
Bora aliachana nao tu, wanakula pesa zetu wanaenda ulaya kila kukicha kula pesa zetu. Zile pesa zingeanzisha barabara nyingi sana.

Matokeo yake sasa hivi miradi inayoendelea ni ile tu iliyoachwa na Marehemu, tena kwa kujikongoja. Huku maBi na maBii.. wakilipwa wanaitwa wapianzani.
 
Back
Top Bottom