Kosa la Adolph Hitler la Septemba mosi 1939 linataka kurudiwa na Vladimir Putin

Mkuu unahisi hakuna dunia bila wayahudi...?
Hii mada umeipamba na ushabiki mwingi.
Hizi sio mambo za kushabikia kabisa...
Lipite kwa amani hope watafikia muafaka mzuri kwa pande zote.
 
Mkuu unahisi hakuna dunia bila wayahudi...?
Hii mada umeipamba na ushabiki mwingi.
Hizi sio mambo za kushabikia kabisa...
Lipite kwa amani hope watafikia muafaka mzuri kwa pande zote.
Mungu ni mwema litapita kwa amani.
 
Wote wana makosa na kila mmoja hapo ana justification za kufanya alichofanya. Mfano Putin ni mtu anapenda kutumia ushahidi wa historia, mwaka 1939 kulisainiwa Molotov-Ribbentrop Pact baina ya USSR na Ujerumani kwamba hawatavamiana. Ujerumani ikaanza kusogeza silaha zake kukaribiana na USSR, 1939 hiyo hiyo ikavamia Poland, ikavamia nchi jirani nyingine inazidi kusogea. USSR nao wakavakia Poland kwa pretext kwamba ilichukua majimbo ya Ukraine na Belarus miaka ya nyuma. Ikawa USSR na Ujerumani ziko karibu kabisa.

Britain walikuwa na spy network nzuri wakaiambia USSR kwamba Ujerumani inapanga kuivamia. USSR ikajua ni ulaghai Waingereza wanafanya, mara 1941 Hitler akavunja makubaliano akavamia bila Stalin kuamini mpaka siku moja imepita. Kumbe mbinu zote za Ujerumani kusogea Poland na majirani lengo ni Wasovieti.

Sasa leo NATO wanasogea kuizunguka Russia ila Russia akiamua aizunguke USA watagoma. Russia itaaminije NATO wamekuja kukaa tu. Mimi na wewe tuna ugomvi, umetoka kwako uko umeshika panga ukaketi karibu na kwangu mlangoni alafu nikichungulia kuuliza unasema hamna shida unaangalia mazingira, unadhani nitakubali?
 
Putin sio mwenye tatizo peke yake. Rafiki wa adui yako ni adui yako, hizi sababu za military expansion na alliances ndio zilileta WW1 na WW2. Russia inataka buffer zone na imefanya hivi kila ikiona maslahi yake yanapotea, Nikita Khrushchev alivyoondoa makombora Cuba wale Soviet politburo walimuona mzembe na pacifist. Ni interest za Russians kuwa mbali na NATO, Finland imezingatia hilo, Ukraine ilizingatia hilo ila mwishowe ikataka kuwa member.

Kwanini hujalalamika Israel hao Wayahudi wako wanavyoshambulia miradi ya silaha ya Waarabu na projects za kuwapa mafunzo na silaha makundi kama Hezbollah na Hamas nchini Syria, Palestina na Lebanon. Mbona Israel imeshambulia kinu cha nyuklia cha Iraq mwaka 1980. Mbona imeshambulia cha Syria mwaka 2007. Israel hadi leo si inashambulia Syria au hujui?

Yaani unawakuza Wayahudi kama hawafanyi hivyo alivyofanya Russia. Unataka watu waache uzinzi wawe wasafi, kwenye kutoa mfano kina nani wasafi ukataja makahaba
 

..nilikuwa nazungumzia suala la majimbo yanayotaka / yaliyoamua kujitenga na Ukraine.

..masuala ya NATO nadhani ni ya kizamani mno, dunia ilishapita huko kwenye vita baridi.

..Biden na Putin wana mawazo ya kizamani.
 

..Russia wawekeze Eastern Europe ili kuinua standard of living za raia wa nchi hizo.

..USA iwekeze South America ambako wananchi wake wana hali mbaya kwelikweli na wanalazimika kukimbilia USA.

..dunia imebadilika sasa hivi wakati Biden na Putin bado wanaota ndoto za kizamani za wakati wa cold war. Yaani wanabishania kitu na masuala ambayo hayana manufaa yoyote kwa wananchi wa nchi zao, na dunia kwa ujumla.
 
Mkuu

Kuvamia nchi nyingine kwa sababu zisizoingia kichwani ni ngumu sana. Ni kweli si Saddam lakini udikteta wa Hitler kwa karne hakuna atakayeuvumilia.
Udikteta wa marekani kwa dunia ya leo ni mara 20 zaidi ya ule wa Hitler miaka ile. Si kwamba unavumiliwa, pengine Putin anaionyesha dunia kwamba ipo namna ya kuweza kuuondosha udikteta huo.
 
Udikteta wa marekani kwa dunia ya leo ni mara 20 zaidi ya ule wa Hitler miaka ile. Si kwamba unavumiliwa, pengine Putin anaionyesha dunia kwamba ipo namna ya kuweza kuuondosha udikteta huo.
Putin ameanza kuishambulia Ukraine muda huu tunavyoongea.
 
Jambo jema sana. Russia na China wanasaidia kuweka balance kwenye geopolitics.
Unaongelea geopolitics wakati kuna watu wanakufa na wengine wanageuka mayatima!!?.

Labda ni kwa sababu Tanzania tumeishi kwa amani kwa miaka mingi.
 
Unajua idadi ya waliokufa Iran au Korea kaskazini kutokana na vikwazo walivyowekewa na Marekani?!

Au hiyo haikugusi!
Mkuu kuna watoto wa kitanzania wanaosoma vyuo vikuu vya Ukraine, sasa hivi jiulize wapo katika hali gani.
 
Biden unamsingizia hana ndoto hizo. Hiyo Russia inayozidiwa uchumi na South Korea ndio unasema iwekeze Eastern Europe? Kwa hela ipi waliyonayo
 
Mimi nilikuwa kule na nimeacha watanzania ninaowafahamu. Unaongea North Korea na Iran ukiwa unajenga hoja tu, ni vitu viwili tofauti.
Ukitanguliza utanzania kwenye masuala kama haya unakuwa unaweka mbele ubinafsi. Waone wote wanaoteseka duniani kwa kadhia hizi kama ndugu zako, itakuweka huru.
 
Jumuia ya kimataifa imeishachelewa kuchukua hatua,kama ilivyochelewa kwa Adolf Hitler mpaka akaua wayahudi milioni moja.
Putin aliishambulia Georgia,Dunia ikakaa kimya.
Akaimega Crimea kutoka Ukraine,Dunia ikakalia matamko tu.
Wakaimega Donesk na Luhansk kutoka Ukraine,badala ya vitendo,ni matamko tu.
Sasa wamewasha siraha za moto wanapiga miji mikubwa ndani ya Ukraine,Dunia Bado haijaelewa tu?.
NATO na USA zile nguvu walizotumia kuisambaratisha Libya na Ghadafi,wanashindwa nini kuzitumia sasa hv.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…