Kosa la Adolph Hitler la Septemba mosi 1939 linataka kurudiwa na Vladimir Putin

Kosa la Adolph Hitler la Septemba mosi 1939 linataka kurudiwa na Vladimir Putin

Mkuu unahisi hakuna dunia bila wayahudi...?
Hii mada umeipamba na ushabiki mwingi.
Hizi sio mambo za kushabikia kabisa...
Lipite kwa amani hope watafikia muafaka mzuri kwa pande zote.
 
Wote wana makosa na kila mmoja hapo ana justification za kufanya alichofanya. Mfano Putin ni mtu anapenda kutumia ushahidi wa historia, mwaka 1939 kulisainiwa Molotov-Ribbentrop Pact baina ya USSR na Ujerumani kwamba hawatavamiana. Ujerumani ikaanza kusogeza silaha zake kukaribiana na USSR, 1939 hiyo hiyo ikavamia Poland, ikavamia nchi jirani nyingine inazidi kusogea. USSR nao wakavakia Poland kwa pretext kwamba ilichukua majimbo ya Ukraine na Belarus miaka ya nyuma. Ikawa USSR na Ujerumani ziko karibu kabisa.

Britain walikuwa na spy network nzuri wakaiambia USSR kwamba Ujerumani inapanga kuivamia. USSR ikajua ni ulaghai Waingereza wanafanya, mara 1941 Hitler akavunja makubaliano akavamia bila Stalin kuamini mpaka siku moja imepita. Kumbe mbinu zote za Ujerumani kusogea Poland na majirani lengo ni Wasovieti.

Sasa leo NATO wanasogea kuizunguka Russia ila Russia akiamua aizunguke USA watagoma. Russia itaaminije NATO wamekuja kukaa tu. Mimi na wewe tuna ugomvi, umetoka kwako uko umeshika panga ukaketi karibu na kwangu mlangoni alafu nikichungulia kuuliza unasema hamna shida unaangalia mazingira, unadhani nitakubali?
 
Putin ndio tatizo lenyewe. Mbona Ukraine iliyoongozwa na kina Kuchma au Yanukovich ilikuwa na uhusiano mwema na Russia?.

USA kuikaribia Ukraine haijaanza jana wala juzi, lakini hatukuwahi kuona Kremlin wakifikia maamuzi ya kuipiga nchi na kutangaza majimbo yake kuwa ni sehemu ya Russia.

Enzi za Yeltsin hatukuwahi kusikia hizi habari za kibabe zikiongelewa, waliijua diplomasia na ujanja wake.

Hamna ubunifu miongoni mwa wenye kufanya diplomasia ndani ya serikali ya Russia.
Putin sio mwenye tatizo peke yake. Rafiki wa adui yako ni adui yako, hizi sababu za military expansion na alliances ndio zilileta WW1 na WW2. Russia inataka buffer zone na imefanya hivi kila ikiona maslahi yake yanapotea, Nikita Khrushchev alivyoondoa makombora Cuba wale Soviet politburo walimuona mzembe na pacifist. Ni interest za Russians kuwa mbali na NATO, Finland imezingatia hilo, Ukraine ilizingatia hilo ila mwishowe ikataka kuwa member.

Kwanini hujalalamika Israel hao Wayahudi wako wanavyoshambulia miradi ya silaha ya Waarabu na projects za kuwapa mafunzo na silaha makundi kama Hezbollah na Hamas nchini Syria, Palestina na Lebanon. Mbona Israel imeshambulia kinu cha nyuklia cha Iraq mwaka 1980. Mbona imeshambulia cha Syria mwaka 2007. Israel hadi leo si inashambulia Syria au hujui?

Yaani unawakuza Wayahudi kama hawafanyi hivyo alivyofanya Russia. Unataka watu waache uzinzi wawe wasafi, kwenye kutoa mfano kina nani wasafi ukataja makahaba
 
Wajue mustakabali wa nchi yao unapoishia ndipo mstakabali wa nchi nyingine unapoanzia.

Hitaji lao kubwa wajiunge na NATO. Hii Atlantic organization mpaka mpakani mwa Russia haina hata mantiki.

Fikiria Russia leo akisema anapeleka zana za kijeshi zikiwemo za nyuklia kwa rafiki yake Venezuela au Cuba, patakalika?!

Tatizo ni US kujifanya yeye ndie mmiliki wa hii dunia.

..nilikuwa nazungumzia suala la majimbo yanayotaka / yaliyoamua kujitenga na Ukraine.

..masuala ya NATO nadhani ni ya kizamani mno, dunia ilishapita huko kwenye vita baridi.

..Biden na Putin wana mawazo ya kizamani.
 
Sasa masuala ya kimataifa kutofautiana yana uzito. Southern Ossetia na Abkhazia ilikuwa hivi, Crimea imekuwa annexed Russia wakawekewa vikwazo. Bado ukirudi kwenye chanzo chenyewe Ukraine haikufanya vizuri calculations za kuwa karibu na NATO, kina Poland waliwahi kipindi Russia haijatengamaa. Finland waliochelewa tena ambao USSR ilishawahi kuwavamia wakaamua kuwa neutral kwa sababu wanapakana na Russia. Ukraine ndio doorstep ya kuingia Russia alafu anataka NATO waweke bases zake. Mbona US hawezi kukubali bases za Russia kuwepo Venezuela au Cuba.

Ushasema mambo ya kimataifa hutofautiana. Ndio tofauti zenyewe hizi

..Russia wawekeze Eastern Europe ili kuinua standard of living za raia wa nchi hizo.

..USA iwekeze South America ambako wananchi wake wana hali mbaya kwelikweli na wanalazimika kukimbilia USA.

..dunia imebadilika sasa hivi wakati Biden na Putin bado wanaota ndoto za kizamani za wakati wa cold war. Yaani wanabishania kitu na masuala ambayo hayana manufaa yoyote kwa wananchi wa nchi zao, na dunia kwa ujumla.
 
Mkuu

Kuvamia nchi nyingine kwa sababu zisizoingia kichwani ni ngumu sana. Ni kweli si Saddam lakini udikteta wa Hitler kwa karne hakuna atakayeuvumilia.
Udikteta wa marekani kwa dunia ya leo ni mara 20 zaidi ya ule wa Hitler miaka ile. Si kwamba unavumiliwa, pengine Putin anaionyesha dunia kwamba ipo namna ya kuweza kuuondosha udikteta huo.
 
Udikteta wa marekani kwa dunia ya leo ni mara 20 zaidi ya ule wa Hitler miaka ile. Si kwamba unavumiliwa, pengine Putin anaionyesha dunia kwamba ipo namna ya kuweza kuuondosha udikteta huo.
Putin ameanza kuishambulia Ukraine muda huu tunavyoongea.
 
Jambo jema sana. Russia na China wanasaidia kuweka balance kwenye geopolitics.
Unaongelea geopolitics wakati kuna watu wanakufa na wengine wanageuka mayatima!!?.

Labda ni kwa sababu Tanzania tumeishi kwa amani kwa miaka mingi.
 
Unajua idadi ya waliokufa Iran au Korea kaskazini kutokana na vikwazo walivyowekewa na Marekani?!

Au hiyo haikugusi!
Mkuu kuna watoto wa kitanzania wanaosoma vyuo vikuu vya Ukraine, sasa hivi jiulize wapo katika hali gani.
 
..Russia wawekeze Eastern Europe ili kuinua standard of living za raia wa nchi hizo.

..USA iwekeze South America ambako wananchi wake wana hali mbaya kwelikweli na wanalazimika kukimbilia USA.

..dunia imebadilika sasa hivi wakati Biden na Putin bado wanaota ndoto za kizamani za wakati wa cold war. Yaani wanabishania kitu na masuala ambayo hayana manufaa yoyote kwa wananchi wa nchi zao, na dunia kwa ujumla.
Biden unamsingizia hana ndoto hizo. Hiyo Russia inayozidiwa uchumi na South Korea ndio unasema iwekeze Eastern Europe? Kwa hela ipi waliyonayo
 
Mimi nilikuwa kule na nimeacha watanzania ninaowafahamu. Unaongea North Korea na Iran ukiwa unajenga hoja tu, ni vitu viwili tofauti.
Ukitanguliza utanzania kwenye masuala kama haya unakuwa unaweka mbele ubinafsi. Waone wote wanaoteseka duniani kwa kadhia hizi kama ndugu zako, itakuweka huru.
 
Wanasiasa hufanya makosa mengi sana wakiwa madarakani. Wanapoyafanya huwa hawana uwezo wa kupima ukubwa na madhara ya wanachokusudia kukifanya. Ni pale wanapokuwa wanapokea lawama nyingi ndio hujisumbua kuangalia kwa kina namna ambavyo wangeweza kuzuia kile walichokifanya, wangefanya hivi na wakafanya vile ndio huwa ni wazo lililochelewa wakati wake. Wanapokuwa wakiamua kufanya maamuzi yanayoongozwa na upofu au ulevi wa madaraka huwa wamezungukwa na wapambe wanaosema kitu wanachotaka kukisikia. Wao kuwa na maamuzi ya mwisho wakati mwingine huwanyima ile busara ya kuwa mawazo yao sio kila wakati huwa ndio ya kutekelezwa na yakaja na jibu lililokusudiwa na lenye faida.

Rais wa Russia Vladmir Putin anataka kufanya kosa litakalompa umaarufu mbovu kama ule aliokuwa nao Adolph Hitler mwaka 1939. Putin anataka kufanya kosa kama lile alilolifanya Idd Amin mwaka 1978 kwa kuivamia sehemu ya mkoa wa Kagera, kipigo alichokipata kilimpoteza kabisa miongoni mwa viongozi wa mataifa waliostahili heshima kila walipokatiza. Putin ameiangalia Ukraine katika udogo wake kwa kuilinganisha na Russia hivyo anaamini kwamba anaweza kufanya lolote na dunia ya sasa ikatulia tu na kumtazama. Kitakachompata kitakuwa ni fedheha kama ile iliyomkuta Hitler ambaye aliishia kujinyonga baada ya vita kumalizika akiwa ameshindwa vibaya.

Anatakiwa kukumbushwa kuwa Volodymyr Zelensky licha ya kuwa ni rais wa Ukraine taifa huru lenye maamuzi huru kama ilivyo Russia pia ni myahudi. Kwa asili ya wayahudi huwa ni watu wenye mtandao ulio hai na makini siku zote. Wayahudi wanajuana popote walipo, na mwanasiasa ambaye hata kama upande wa Mama ndio wayahudi huwa wanamchukulia kama ni mtoto wao. Wayahudi wanalinda ushawishi walionao duniani kote. Na ni rahisi kwao kumpachika jina la 'anti semitic' yoyote yule anayekwenda kinyume na falsafa zao au anayewakejeli.

Sembuse maamuzi ya Putin kuivamia nchi huru ya Ukraine inayoongozwa na myahudi mwenzao!!. Putin anakosa washauri wenye kutazama mbali, wenye ushawishi wa kidunia. Atumie busara sana kwani anachofikiria dhidi ya Ukraine kinaweza kumpoteza kabisa na yale yote aliyokwisha kuyafanya tangu 1999 alipoanza kuongoza Russia yakafunikwa na huu 'ujinga' anaouwazia kwa sauti ya juu.

Ulimwengu wa 1939 wakati Hitler akiivamia Austria sio huu wa 2022. Zimetungwa sheria nyingi za kimataifa zinazolinda uhuru wa kila taifa. Wamezaliwa wanasiasa wenye maarifa mazito ya kuongoza. Sayansi haijabaki nyuma zimeundwa silaha za hatari zenye kuweza kuangamiza kila kilichopo juu ya uso wa dunia ndani ya saa chache tu. Anaumizwa sana na ushawishi wa USA kwa jirani yake wa karibu, lakini nguvu nyingi hutumiwa na mwenye maarifa madogo ya uongozi.
Jumuia ya kimataifa imeishachelewa kuchukua hatua,kama ilivyochelewa kwa Adolf Hitler mpaka akaua wayahudi milioni moja.
Putin aliishambulia Georgia,Dunia ikakaa kimya.
Akaimega Crimea kutoka Ukraine,Dunia ikakalia matamko tu.
Wakaimega Donesk na Luhansk kutoka Ukraine,badala ya vitendo,ni matamko tu.
Sasa wamewasha siraha za moto wanapiga miji mikubwa ndani ya Ukraine,Dunia Bado haijaelewa tu?.
NATO na USA zile nguvu walizotumia kuisambaratisha Libya na Ghadafi,wanashindwa nini kuzitumia sasa hv.
 
Back
Top Bottom