Kosa la binti huyu mwanachuo lilikuwa nini mpaka atekwe na kuuawa mkoani Mbeya?

Kosa la binti huyu mwanachuo lilikuwa nini mpaka atekwe na kuuawa mkoani Mbeya?

Haya mambo sio ya kuyatetea uwe unajifanya hupendi siasa, unapenda, umepata kaijira chako serikalini au uko mtaa.

Tumia akili yako ya kawaida uliyozaliwa nayo, wewe kama binadamu huwezi tetea ujinga kama huu.

Huyu binti ni vile tu anajulikana ila mitaani watu wanapotezwa kila siku.
 
Huko mbeya bana kuna majitu bado ni maprimitive sana.
Kuna binti mdogo tu hapo uyole stand ya tukuyu,alikua na stationery yake,nilikua mara nyingi nikiwa mbeya naenda hapo kwake kufanya shughuli zangu.
Sasa siku moja ilikua ijumaa nakumbuka nimeenda hapo nikamwachia kazi yangu flani anifanyie kwa makubaliano kuwa jtatu asubuhi nitaipitia.
Dah,inafika jtatu nafika hapo uyole hajafungua ofisi, kupiga simu haipatikani,nilivyouliza majirani wakaniambia amefariki,alivamiwa nyumbani kwake na wahuni wakampiga visu kisha wakachukua chupa ya soda wakamuingizia ukeni.
Yani mbeya sio sehemu salama kabisa huko.
 
Wakiendelea kuchekea utekaji haya mambo yatazidi kushamiri sadly. Mama Abdul hatoi pole wala tamko ila kwenye Simba/yanga anajiongelesha mwenyewe kwa lazima.
 
Shyrose alitekwa siku ya Jumamosi na watu wasiojulikana na wakaanza kumpigia Baba yake simu kumuomba Pesa ili wamuachie huru huku wakimtumia Video fupi wakimuonesha wanavyomtesa.

Baada ya kupata Video hizo Baba Mzazi Dkt. Mabula Mahande alituma kiasi kidogo cha pesa ili Mwanae asiumizwe lakini baada ya Muda Mwili wa Shyrose ukapatikana akiwa amechomwa moto lakini pia akiwa amechomwa Visu Mgongoni.

Shyrose alianza Elimu yake ya Chuo cha Tumaini, Arusha ambapo alikuwa anasomea Shahada ya Sheria lakini kutokana na Matatizo ya kiafya ilibidi ahame akasome Chuo karibu na nyumbani ambapo alihamia Chuo kikuu cha Mzumbe Tawi la Mbeya, Hapa alianza Mwaka wa Kwanza na mpaka Umauti unamkuta 😢💔

Shyrose amefariki akiwa na umri wa Miaka 21 tuu, too young 😭

Msiba upo Nyumbani kwao Mbeya, Uzunguni karibu na Desderia Hotel na kwa Taarifa za awali kuzika ni Jumamosi ila Mahali pa Kuzika bado hapajakuwa-confirmed


View attachment 3475619
Nilisoma sehemu kwamba walihitaji 200m , cha kujiuliza yule mzee alikuwa na uwezo gani , adui wa mtu huwa hatoki mbali.
Pole kwa familia , binti ameuawa kikatili sana
 
Ila binadamu😢.
Unamchoma mtu visu hujaridhika unaamua uutie na mwili wake kiberiti. Kama walikuwa na tatizo na mzee wake si wangemalizana wao kwa wao!
Kuchoma moto ni kujaribu kuficha baadhi ya ushahidi unaoweza kujitokeza mfano fingerprint,ushahidi wa vinasaba pia sometime wanajua itachelewesha uchunguzi hivyo watapata muda wa kutoroka
 
Sio kila kitu kutekwa, kwani alikuwa mwanaharakati mitandaoni?
Hapa nadhani ni kuna mpumbavu wa mapenzi kahusika....
Mbona watekaji wenyewe wamemzika......

1758489157499.png
 
Back
Top Bottom