Kosa la binti huyu mwanachuo lilikuwa nini mpaka atekwe na kuuawa mkoani Mbeya?

Kosa la binti huyu mwanachuo lilikuwa nini mpaka atekwe na kuuawa mkoani Mbeya?

Shyrose alitekwa siku ya Jumamosi na watu wasiojulikana na wakaanza kumpigia Baba yake simu kumuomba Pesa ili wamuachie huru huku wakimtumia Video fupi wakimuonesha wanavyomtesa.

Baada ya kupata Video hizo Baba Mzazi Dkt. Mabula Mahande alituma kiasi kidogo cha pesa ili Mwanae asiumizwe lakini baada ya Muda Mwili wa Shyrose ukapatikana akiwa amechomwa moto lakini pia akiwa amechomwa Visu Mgongoni.

Shyrose alianza Elimu yake ya Chuo cha Tumaini, Arusha ambapo alikuwa anasomea Shahada ya Sheria lakini kutokana na Matatizo ya kiafya ilibidi ahame akasome Chuo karibu na nyumbani ambapo alihamia Chuo kikuu cha Mzumbe Tawi la Mbeya, Hapa alianza Mwaka wa Kwanza na mpaka Umauti unamkuta 😢💔

Shyrose amefariki akiwa na umri wa Miaka 21 tuu, too young 😭

Msiba upo Nyumbani kwao Mbeya, Uzunguni karibu na Desderia Hotel na kwa Taarifa za awali kuzika ni Jumamosi ila Mahali pa Kuzika bado hapajakuwa-confirmed


View attachment 3475619
Hautamsikia Samia akijigusa wala kuchukua hatua.

Damu hizi zitamlilia hadi haki ipatikanike
 
Baba Mzazi Dkt. Mabula Mahande

kuna maswali mengi kuhusu hawa watekaji huko Mbeya nchini Tanzania

TOKA MAKTABA :

JULAI 1, 2025
Mbeya, Tanzania
1758282228568.jpeg

Kushoto Dr. Mabula Mahande daktari bingwa masuala ya moyo (Physician /Cardiologist)akipewa fomu .

Dkt. Mabula Michael Mahande amerejesha rasmi fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu hiyo, Dkt. Mahande amesema kwa sasa anasubiri taratibu za chama kufuatwa, ikiwa ni pamoja na mchakato wa majina kupitiwa na vikao husika.
 
Uchunguzi unapaswa kuanzia kwake.

Siyo kwa ubaya, bali ni ktk kuutafuta ukweli wa mambo.
Absolutely!! Watu wenye pesa chafu, wanafanya kazi chafu. Kwenye kazi chafu ukidhulumiwa huwezi kumpeleka mtu Polisi kumshtaki. Kimjini mjini watu humalizana.

Jiulize tu mtu alitakiws alipe Tsh 200 Million ila kaweza kutoa Tsh 50 Million. Kuna via viashiria vyote vya kudhulumiana
 
Utu sasa nchini Tanzania umetoweka, watu wamekuwa wanyama-binadamu haki ya kuishi haithaminiwi

1758282562021.jpeg
 
Tatizo la kutekwa ni njaa ya hao masela, na chanzo cha kuuwawa ilihali pesa imetumwa huenda hao jamaa walikua wamesha mbaka na anawafahamu kwa sura na majina, angewasahe kumpuna pesa baba yake lakini si kubakwa, wakampoteza...
 
Lakini kwenye matukio yote ya utekaji unakuwa mkali hivi au ndio ikitokea CCM unapandwa na hasira? Nakumbuka Gwajima aligusia hiki kitu kwa kusema, vipi ikitokea kwa watoto wenu?

Mdude alichukuliwa mbele ya mke wake na watoto, kibao alichukuliwa ndani ya usafiri wa umma, matukio ni mengi hivyo tusichukulie kawaida yanapotokea apande mmoja na upande mwingine tikiona ndio muhimu zaidi.
... CLUES!
 
Binadamu wote hatuko tofauti na wanyama tunapokosa hofu ya Mungu na kukosa malezi sahihi.Kwanini wafanye hivyo?
 
Huyo mzee ahojiwe kama kunawatu ashawahi kuwafanyia mabaya anyway watu sio vichaa waamuke asbh wakateke mtu pasipo na sababu za msingi.
 
Kama walimteka ndani ya basi na kumuua Ally Kibao na kumtupa kesho yake, na mpaka leo "hawajapatikana" usitegemee jeshi la polisi litaweza kuwakamata na hawa wengine "wasiojulikana"
 
Wewe ndo kama mimi tu, nitatumia resource zangu na zinazonizunguka kuwapata kisha mmoja mmoja namsababishia maumivu makali sana
Ni sahihi. Hutakiwi kushindana wala kutumia polisi. Unanyamaza tu ila hata kwa miaka 3 mbele lazima walipe gharama.
 
Mwaka wa uchaguzi huu, na baba mtu ni mgombea ubunge.

Kwani haiwezi kuwa viceversa?

Haiwezi ikawa "Sympathy Seeking"?
Nawe bwege nini? Yaani uchaguzi ndio justification ya mauaji?

Hapo ni damu kwa damu kwa namna yoyote na kisasi cha damu lazima kiwepo.
 
Kumbe na chat na nyumbu basi umeshinda.
Sema nimeshindwa kujibu maswali sio "nachat ma nyumbu basi umeshinda".

Kama kuna jambo unajua au unaweza kujibu kuhusu kitu unashindwa wapi kutoa majibu?
 
Huyo mzee akibanwa vizuri atasema kweli kwa nini binti yake atekwe na watekaji wakataka pesa​
 
Back
Top Bottom