Sasa tushike lipi na tuache lipi mkuu, maana wengine wanasema maji ya baridi ndio yanasababisha madhara na wewe umesema hapa kwamba maji ya moto yanasababisha mishipia kutanuka hivyo pressure kushuka na mtu kuanguka, sasa tumuamini nani katika hili?Kuna kitu inaitwa postural hypotension. Hii inatokea mtu anaposimama ghafla, pressure inashuka ghafla, mtu anapata kizunguzungu na kuanguka. Hii hutokea anapoamka na kwenda kujisaidia. Hasa wale wanaotumia dawa za pressure, au dawa kama viagra. Ndiyo maana kama unatumia dawa za presuure inashauriwa kukojoa umekaa.
Kitu kingine ni ukioga maji ya moto. Haya yanafanya mishipa itanuke(vasodilation) hili linashusha pressure na mtu anaweza anguka kwa kizunguzungu.
Jambo lingine ni utelezi sababu ya sabuni. Hakuna majini wala mapepo.