Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Mimi sio daktari lakini nimeona wengi wakianguka bafuni na si chooni. Nadhani watu huwa tunatembea na magonjwa na hatujui ukianza kuoga kujimwagia maji ni kama msukumo wa damu unaongezeka kwa kasi sasa mtu anaweza kuwa na pressure ndio anaanguka. Au jaribu kumaliza kula halafu ukimbie wa speed lazima uzimie so may be supply ya oksijeni kwenye ubongo inakuwa hakuna na msukumo wa damu unaongezeka kwa speed. Ni vizuri tuwe tunacheki afya zetu.

Hata mie naunga mkono. Na itambulike kuwa, hasa wakati wa kuoga, mapigo ya moyo huongeza ama kupunguza usukumaji wa damu japo ambalo hipelekea kwa wagonjwa pressure kujikuta matatzon.
 
ushauri ukiingia chooni kama ww ni mkristo tamka neno hili"kwa jina la Yesu"au kama ww ni muislamu tamka hivi "Bismilah"mpaka hapo utakuwa umekamata mamlaka ya eneo hatarishi .nb.uwe na imani.
 
Wana jf hi post Niliona Jana nikaidharau xna, lakini kweli Leo yamenikuta, rafiki angu wa karibu alikuwa anaoga akateleza na kuanguka. kumuwahisha hospitali akafariki. Hakika bafuni so pa kawaida
 
Wana jf hi post Niliona Jana nikaidharau xna, lakini kweli Leo yamenikuta, rafiki angu wa karibu alikuwa anaoga akateleza na kuanguka. kumuwahisha hospitali akafariki. Hakika bafuni so pa kawaida

Yaandikwayo humu hayatoki mwezini wanaobisha huwa ni asili yao kubisha na wengine ni kufuata mkumbo
 
duh,ila kuna ukweli....hadi naogopa kwenda msalani.
 
Bafu langu lina jacuzzi kubwa sana ambalo linaendeshwa na motor mbili kubwa kuzungusha maji kwa nguvu sana kwenye karai la kuogea na kurusha jets za nguvu kwa muogaji. Kwa muda mrefu huwa silitumii jacuzzi hili ila mara chacahe sana ninapokuwa nimechoka na nina muda wa kupotezea bafuni kuchezea maji, jambo ambalo hutokea labda mara moja kwa miezi mitatu hadi mitano.

Miaka kadhaa nilicheza sana kwenye jacuzzi lile kwa muda mrefu kumbe likawa limerusha maji yenye povu la sabuni kwenye sakafu ya kutokea. Sasa baada ya kuwa nimejiridhisha na mchezo wangu wa maj9 nilipotoka ndani ya jacuzzi nikakanyaga sakafu ambayo ilikuwa inateleza nikaanguka sakafuni na kupata majeraha makubwa sana usoni mabyo yalinigharimu hela nyingi sana kutibiwa baada ya insurance kuwa wamelipa sehemu yao.

Nadhani sakafu za kwenye mabafu huweza kuwa na utelezi wakati wowote na kusababisha ajali; ile ya kwangu ilisababishwa na jacuzzi kutumiwa kwa muda mrefu siku hiyo na kuwa limerusha mapovu ya sabuni sakafuni. Ni muhimu kuwa makini unapokuwa bafuni hasa kwa vile sakafu ile inaweza kuwa na utelezi wakati wowote. Vile vile ni vizuri tujenge utamaduni wa kusafisha sakafu za mabafu yetu kwa sababu utelezi mwingine husababishwa na uchafu wa muda mrefu mabafuni.
 
Upande wa imani ya kiislam huamini bafuni/chooni kuna mashetani wawili waitwao KHUBTHI na KHABAITH,ni hatari sana ambapo mafundisho yetu yanatutaka kabla kuingia sehemu hizi tuombe dua kwa kusema"Allahumma inna nauudhubika minal KHUBTHI wal KHABAITH" tafsiri yake ni kuwa "Ewe Mwenyezi Mungu niepushe/nilinde na KHUBTHI na KHABAITH " Kisha unatanguliza mguu wa kushoto unapoanza kuingia chooni/bafuni,ni mashetani wabaya sana.
Pia tunafundishwa pia tunapoingia tujitahidi kufunika kichwa kwa kitu chochote hata kitambaa tu,tusipendelee kuingia chooni kichwa wazi.
 
ushauri ukiingia chooni kama ww ni mkristo tamka neno hili"kwa jina la Yesu"au kama ww ni muislamu tamka hivi "Bismilah"mpaka hapo utakuwa umekamata mamlaka ya eneo hatarishi .nb.uwe na imani.

Ushauri mzuri saana.Hujabagua dini hapo.
Mimi ndio naingia kuoga naanza,
BISMILLAH RAHMAN RAIHM.
 
Wana jf hi post Niliona Jana nikaidharau xna, lakini kweli Leo yamenikuta, rafiki angu wa karibu alikuwa anaoga akateleza na kuanguka. kumuwahisha hospitali akafariki. Hakika bafuni so pa kawaida
kama hayajakukuta, huwezi kuyajua ! N.B, usidharau usichokijua.
 
hii mada imenivuta kwel, week mbili zilizopita nilivytoka job nikaamua kulala kodogo, baada ya kuamka nikaingia toilet kujisaidia haja ndogo ghafla nikaanza kujikia vibaya, nikajikuta tu nashtuka na kujikuta nimelala chooni huku jacho likinitoka mwil mzma. Nashukuru Mungu niliumia kidogo tu lakin mpaka sasa nawaza hii hali inaashiria nn???
 
wakuu naombeni kuuliza hivi kuna jambo gani na mausihano gani ya watu kuanguka chooni au bafuni na kukutwa na mauti siku kazaa baada ya kutokewa na tukio ilo.
na je kuna walioanguka chooni au bafuni wakaendelea kuishI kwa muda mrefu kama wapo wanisaidie kuondoa wasiwasi wangu

Asanteh
 
hakuna mahusiano yyte kati ya kifo na mtu kuanguka chooni/bafuni ila chooni sio sehemu safi na salama hvyo viumbe wahasio wazuri huishi humo.
 
wakuu naombeni kuuliza hivi kuna jambo gani na mausihano gani ya watu kuanguka chooni au bafuni na kukutwa na mauti siku kazaa baada ya kutokewa na tukio ilo.
na je kuna walioanguka chooni au bafuni wakaendelea kuishI kwa muda mrefu kama wapo wanisaidie kuondoa wasiwasi wangu

Asanteh

hakuna uhusiano wowote. haiwezekani kwa mtu mzima mwenye afya yake akateleza na kuanguka then akafa baada ya siku chache eti sababau ni kuanguka chooni. wengi wanaofariki ni wale ambao tayari walikua wagonjwa na wanapojikongoja kwenda chooni na udhaifu wao ikitokea wakaanguka basi watu huhusisha kifo na kuanguka. hivi unaamini mtu uwe fiti kama tyson uteleze bafuni uanguke halafu baada ya siku mbili eti ufe??... ondoa wasiwasi ndugu hakuna uhusiano wowote
 
Back
Top Bottom