Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Habarini za mida wakuu, kuna kitu kiukweli huwa sikielewi fresh. Hii huwa inatokea mara nyingi sana, mtu akianguka chooni basi ataugua sana au kufa kabisa. Sasa me naomba kufahamishwa hivi kuna nini haswa nyuma ya pazia? Kwanini ukianguka chooni tu ndo unapata matatizo ila sehemu zingine inakua kawaida? Please let me know?

Kuanguka kwa

chooni ni dalili ya ishara mbaya ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi kupooza kwa upande mmoja. Na Kama utaanguka

chooni kwa bahati mbaya na unaweza usipooze upande mmoja itakuwa ni bahati yako nzuri lakini wengi wao

wanaoanguka chooni huwa wanapatwa na maradhi ya kiharusi yaani Stroke na kama utapona basi utakuwa umepooza

upande mmoja kwa wanawake hupooza upande wa kulia kwa wanaume hupooza upande wa kushoto na ikitokea

umepoza upande mmoja basi kupona inakuwa tabu sana. Kwa imani zetu watu wa Miji ya Pwani yaani Bwagamoyo Dar,Tanga,Zanzibar,Pemba, Mtwara na Mombasa chooni kuna Shetani mbaya

unachotakiwa kwenda chooni utangulize mguu wa kushoto na usome dua fulani kwa kiswahili unaweza kusema hivi

(Ewe Mwenyeezi Mungu ninajikinga kwako kutokana na uchafu wa shetani).Ndio unaingia kwa kutumia mguu wako kushoto na wakati wa

kutoka unatoka na mguu wa kulia ndio unaotanguliza kwa kumuomba Mungu pia, kwa kumshukuru unasema hivi

(Ninakushukuru kwako Mwenyeezi Mungu) ndio unatanguliza mguu wa kulia wakati wa kutoka hayo ndio ninavyojuwa mimi sijuwi

wenzangu wengine mnajuaje tuelewesheni jamani.

Ni yapi makazi ya Majini?

Majini wanaishi katika mgongo wa ardhi, na wanapatikana kwa wingi katika majangwa na sehemu za takataka, sehemu zenye najisi, chooni na makaburini. Na hii ndio sababu hasa ya wale waganga ambao wana uhusiano na mashetani kupenda kuwashauri wateja wao kupeleka vitu vyao na uchawi wao katika maeneo hayo.

images

Shetani huyu ndio hupenda kukaa chooni au sehemu chafu chafu na pia hukaa majalalani.Na hupenda kunyonya Damu za watu. chanzo.
[h=1]Topic: Kuanguka chooni/bafuni na kufa,kuna uhusiano gani?[/h]
 
KWA IMANI YA KI -HOSPITALI:

Kuanguka chooni itategemea utaitafsiri vipi, mfano kishirikina/kiimani/Kimila/ Kisayansi n.k.

Kishirikina watu huamini, mtu 'amemchawia' mwingine na hivyo kumuadhibu kwa njia hiyo.Hii ipo hadi leo katika jamii yetu.

Kiimani, wengine huamini ni aina ya adhabu kutokana na uovu mtu aliowahi kuufanya na hivyo Mungu kumuadhibu kwa nia hiyo. Au uwepo wa "Majini" kwa wenye kuamini hivyo.

Kisayansi, hali hii inaweza kutokea kwa watu wa aina nyingi lakini Mtu kudondoka Chooni (specifically), hutegemea Jinsia, umri, Kazi, aina ya ugonjwa n.k

Jinsia:
Wanaume- hasa kuanzia umri wa miaka ya 55 kuendelea, zaidi ikiwa kuanzia miaka 65 hadi 70 huwa na ongezeko la ukuaji wa tezi dume (Prostate), hii hufanya kugandamizwa kwa njia ya mkojo na hivyo wakati wa kujisaidia haja ndogo (kukojoa) hutumia nguvu nyingi 'Straining' na kusababisha kuongezeka kwa pressure tumboni ilihali kushuka ghafla kwa msukumo wa damu) na hivyo kuleta kizunguzungu na mtu kudondoka.(same scenario mtu akienda haja kubwa na ku-strain)

Wanawake- Kufikia umri wa miaka 55 na kuendelea(kwa wanawake) hasa ule muda ambao ukomo wa mzunguko/hedhi kukoma wanawake wengi hupatwa na tatizo hili, hasa kutokana na mifupa yako kutokuwa imara.

Pia wanawake wengi waliotunia vidonge vya uzazi wa mpango.

Kazi:
Pili aina ya kazi, wengi wa watu wenye kazi za kuinama...mfano kubeba mizigo, wapishi (hasa migahawa n.k), hupata shida ya pingili za uti wa mgongo, hii huweza kusababisha miguu kukosa nguvu, na mru awapo katika sehemu unayoteleza ni rahisi kuanguka na kuvunjika

Aina ya ugonjwa:
Magonjwa mfano Shinikizo kubwa la damu (Hypertension), na magonjwa mbali mbali ya kifua hutegemea sana uwiano mzuri wa msukumo wa damu na mgandamizo wa hewa, viashiria vya mgandamizo mkubwa (Baroreceptors ) mwilini hutambua endapo kunakuwa na shida hiyo.

Pili, magonjwa ya mifupa kwa aina zake hufanya miguu kutokuwa imara hivyo kazi za kuinama, kuchuchumaa kwa muda mrefu huweza kuwa katika hatari ya kudondoka na kuvunjika .

Hivyo basi the bottomline ni STRAINING activity yeyote yenye kusababisha kubadilika kwa pressure, pamoja na matatizo ya mifupa...na inakuwa chooni, kwa sababu tu ya slippery floor/tiles, straining wakati wa kujisaidia (haja kubwa na haja ndogo).

kazı kwenu wenye imani mutachaguwa imani ya Kidini au imani hii ya Ki-HOSPITALI?
 
Harufu kali ya mikojo ya viroba inafanya ubongo upate ustuko ndo maana watu wanaanguka
 
Kuanguka kwa

chooni ni dalili ya ishara mbaya ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi kupooza kwa upande mmoja. Na Kama utaanguka

chooni kwa bahati mbaya na unaweza usipooze upande mmoja itakuwa ni bahati yako nzuri lakini wengi wao

wanaoanguka chooni huwa wanapatwa na maradhi ya kiharusi yaani Stroke na kama utapona basi utakuwa umepooza

upande mmoja kwa wanawake hupooza upande wa kulia kwa wanaume hupooza upande wa kushoto na ikitokea

umepoza upande mmoja basi kupona inakuwa tabu sana. Kwa imani zetu watu wa Miji ya Pwani yaani Bwagamoyo Dar,Tanga,Zanzibar,Pemba, Mtwara na Mombasa chooni kuna Shetani mbaya

unachotakiwa kwenda chooni utangulize mguu wa kushoto na usome dua fulani kwa kiswahili unaweza kusema hivi

(Ewe Mwenyeezi Mungu ninajikinga kwako kutokana na uchafu wa shetani).Ndio unaingia kwa kutumia mguu wako kushoto na wakati wa

kutoka unatoka na mguu wa kulia ndio unaotanguliza kwa kumuomba Mungu pia, kwa kumshukuru unasema hivi

(Ninakushukuru kwako Mwenyeezi Mungu) ndio unatanguliza mguu wa kulia wakati wa kutoka hayo ndio ninavyojuwa mimi sijuwi

wenzangu wengine mnajuaje tuelewesheni jamani.

Ni yapi makazi ya Majini?

Majini wanaishi katika mgongo wa ardhi, na wanapatikana kwa wingi katika majangwa na sehemu za takataka, sehemu zenye najisi, chooni na makaburini. Na hii ndio sababu hasa ya wale waganga ambao wana uhusiano na mashetani kupenda kuwashauri wateja wao kupeleka vitu vyao na uchawi wao katika maeneo hayo.

images

Shetani huyu ndio hupenda kukaa chooni au sehemu chafu chafu na pia hukaa majalalani.Na hupenda kunyonya Damu za watu. chanzo.
[h=1]Topic: Kuanguka chooni/bafuni na kufa,kuna uhusiano gani?[/h]

Aiseee hii nayo ni ya auna yake
 
Kuna tatizo la kiafya ambalo huwakumba watu wengi hasa wakiwa chooni katika haja kubwa. Mjongeo wa Utumbo mpana (bowel movement) unahitaji damu nyingi ili kufanikisha zoezi na hili uhusisha mishipa mikubwa ya damu moja kwa moja kutoka maeneo ya juu ya mwili wa binadamu. Kumbuka kupungua kwa oxygen katika ubongo husababisha kuzimia na pale damu inapozuiwa kwenda kichwani kwa kiwango cha kawaida, fainting is inevitable.

Kwa wale wenye tatizo hili huwa pia wana ugumu wa kupata choo (constipation) hivyo katika kujikamua zaidi (over straining) damu nyingi zaidi husukumwa katika utumbo mpana na kupungua kichwani hivyo kuleta kizungu-zungu na hata kuzimia. Si damu pekee kupungua kichwani bali pia katika over straining, biggest nerve (vagus nerve) katika uti wa mgongo hutuma ujumbe katika ubongo juu ya mtiririko wa ghafa wa damu hivyo shinikizo la damu (blood pressure) na mapigo ya moyo (heart beat rate) pia huongezeka maradufu hivyo damu nyingi hubaki katika maeneo ya chini ya mwili.

Katika hali ya hii kizunguzungu na mtu huyu anaweza kujaribu kusimama au kujitoa katika hali hiyo ya ajabu na hapa ndipo madhara zaidi yanaweza kutokea maana anaweza kuanguka kwa vibaya na kugonga kichwa hali ambayo itamletea madhara makubwa. Vyoo vingi vimejengwa katika muundo wa kuta nne, kunaweza kuwa sink na pia tiles. Katika hali hii uwezekano wa kugonga kichwa katika ukuta,sink au sakafu unakuwa mkubwa. Pia choo ni faragha hivyo mtu anayeanguka chooni anaweza kuchelewa kupata huduma ya haraka hivyo madhara huongezeka katika hali ile kulinganisha na maeneo mengine ambayo angeweza kuonekana haraka na kupewa huduma ya kwanza au kukimbizwa hospitali.
 
Mpige deki bafuni Mara kwa Mara sio bafu Lina utelezi wa uchafu! Mkianguka mnasema majini.
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Duh!! kumbe ukiingia toi unaingia na shoto then unatoka na lia..
 
nadhani MziziMkavu kamaliza kla kitu, mi naungana nae sema kwenye sayansi pale... kuhusu majini sina uelewa huo, Mungu kafanya kaazi ya kunilinda vyema sana toka nazaliwa sijawahi sumbuliwa na vitu kama hivo... Mi chooni naingia kivyovyote natoka vyovyote, tena hakuna kuomba dua wala nini... so itakua ngumu kuamini
 
A na B yote ni majibu.inasababishwa na ushirikina au ugonjwa.
 
Chooni kunahusishwa na nguvu za giza,nikisikia wanashauri km mtu akianguka chooni msimchome sindano bali maombi kama mnaamini katika maombi km mimi
 
R i P.
Mzee Small.
Hatimae MCHEKESHAJI maarufu nchini Tanzania Mzee Small,Kazikwa leo katika Makaburi ya kinyerezi.
Inasemekana alianguka bafuni,na baadae akaugua kiharusi,na ndicho kilicho sababisha Kifo chake.
Poleni wafiwa woote:
 
Kwa hiyo mtu kamloga small ili apate kile kibarakashia chake

cool down Mkuu😡
Kigogo unaanza kufika mbaali,tunahabarishana tu mkuu.
Ya ngoswe mwachie ngoswe sisi hayo ya mzee wa watu kurogwa,hakuna mtu alotoa/thibitisha kauli
 
Last edited by a moderator:
Kuna tatizo la kiafya ambalo huwakumba watu wengi hasa wakiwa chooni katika haja kubwa. Mjongeo wa Utumbo mpana (bowel movement) unahitaji damu nyingi ili kufanikisha zoezi na hili uhusisha mishipa mikubwa ya damu moja kwa moja kutoka maeneo ya juu ya mwili wa binadamu. Kumbuka kupungua kwa oxygen katika ubongo husababisha kuzimia na pale damu inapozuiwa kwenda kichwani kwa kiwango cha kawaida, fainting is inevitable.

Kwa wale wenye tatizo hili huwa pia wana ugumu wa kupata choo (constipation) hivyo katika kujikamua zaidi (over straining) damu nyingi zaidi husukumwa katika utumbo mpana na kupungua kichwani hivyo kuleta kizungu-zungu na hata kuzimia. Si damu pekee kupungua kichwani bali pia katika over straining, biggest nerve (vagus nerve) katika uti wa mgongo hutuma ujumbe katika ubongo juu ya mtiririko wa ghafa wa damu hivyo shinikizo la damu (blood pressure) na mapigo ya moyo (heart beat rate) pia huongezeka maradufu hivyo damu nyingi hubaki katika maeneo ya chini ya mwili.

Katika hali ya hii kizunguzungu na mtu huyu anaweza kujaribu kusimama au kujitoa katika hali hiyo ya ajabu na hapa ndipo madhara zaidi yanaweza kutokea maana anaweza kuanguka kwa vibaya na kugonga kichwa hali ambayo itamletea madhara makubwa. Vyoo vingi vimejengwa katika muundo wa kuta nne, kunaweza kuwa sink na pia tiles. Katika hali hii uwezekano wa kugonga kichwa katika ukuta,sink au sakafu unakuwa mkubwa. Pia choo ni faragha hivyo mtu anayeanguka chooni anaweza kuchelewa kupata huduma ya haraka hivyo madhara huongezeka katika hali ile kulinganisha na maeneo mengine ambayo angeweza kuonekana haraka na kupewa huduma ya kwanza au kukimbizwa hospitali.
 
Mkuu Mgalanjuka
hivi hii kitu na nchi za wenzetu;Uzunguni,uarabuni,uhindini n.k kuna tatizo hili la kuumwa kiharusi mara baada ya kupatwa na tatzo la kujikamua choon?
Nafaham wazi kuwa na wao wanaumwa kiharusi,ila kwa vyanzo vya taarifa,vikidai muhusika aliugua mara baada ya kuachwa/kuachana na mumewe/mkewe na matatizo mengne ya mahusiano ya kijamii.lkn khs chooni sio siri kwa ulaya sijwahiskia,labda walobahatika kukaa nchi za wenzetu waje watufafanulie hapo,
sasa jee?kinachotuponza tujikamue sana tukiwa chooni inatokana na nn/sabab gani?
Uzee,kupungukiwa nguvu,milo ya kibongo bongo,Au uswahili?
Na mara nyingi wahanga ni adult age,adolecence age haiwatokei hii kitu ijapokuwa wanakula milo ile ile wanayokula mature/adult age.Hii ni kwa nn mkuu?
 
Last edited by a moderator:
kama ishu ya ya dr slaa nae alidondoka chooni, na kulemaa mkono.
kwangu mimi naona labda ni.kutokana ma kuteleza kwa tailizi kukichanganyka na sabuni

ndio maana mkono wake mpaka leo hajapona
 
Back
Top Bottom