Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Habarini za mida wakuu, kuna kitu kiukweli huwa sikielewi fresh. Hii huwa inatokea mara nyingi sana, mtu akianguka chooni basi ataugua sana au kufa kabisa. Sasa me naomba kufahamishwa hivi kuna nini haswa nyuma ya pazia? Kwanini ukianguka chooni tu ndo unapata matatizo ila sehemu zingine inakua kawaida? Please let me know?
Kuanguka kwa
chooni ni dalili ya ishara mbaya ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi kupooza kwa upande mmoja. Na Kama utaanguka
chooni kwa bahati mbaya na unaweza usipooze upande mmoja itakuwa ni bahati yako nzuri lakini wengi wao
wanaoanguka chooni huwa wanapatwa na maradhi ya kiharusi yaani Stroke na kama utapona basi utakuwa umepooza
upande mmoja kwa wanawake hupooza upande wa kulia kwa wanaume hupooza upande wa kushoto na ikitokea
umepoza upande mmoja basi kupona inakuwa tabu sana. Kwa imani zetu watu wa Miji ya Pwani yaani Bwagamoyo Dar,Tanga,Zanzibar,Pemba, Mtwara na Mombasa chooni kuna Shetani mbaya
unachotakiwa kwenda chooni utangulize mguu wa kushoto na usome dua fulani kwa kiswahili unaweza kusema hivi
(Ewe Mwenyeezi Mungu ninajikinga kwako kutokana na uchafu wa shetani).Ndio unaingia kwa kutumia mguu wako kushoto na wakati wa
kutoka unatoka na mguu wa kulia ndio unaotanguliza kwa kumuomba Mungu pia, kwa kumshukuru unasema hivi
(Ninakushukuru kwako Mwenyeezi Mungu) ndio unatanguliza mguu wa kulia wakati wa kutoka hayo ndio ninavyojuwa mimi sijuwi
wenzangu wengine mnajuaje tuelewesheni jamani.
Ni yapi makazi ya Majini?
Majini wanaishi katika mgongo wa ardhi, na wanapatikana kwa wingi katika majangwa na sehemu za takataka, sehemu zenye najisi, chooni na makaburini. Na hii ndio sababu hasa ya wale waganga ambao wana uhusiano na mashetani kupenda kuwashauri wateja wao kupeleka vitu vyao na uchawi wao katika maeneo hayo.
Shetani huyu ndio hupenda kukaa chooni au sehemu chafu chafu na pia hukaa majalalani.Na hupenda kunyonya Damu za watu. chanzo. [h=1]Topic: Kuanguka chooni/bafuni na kufa,kuna uhusiano gani?[/h]