nyboma
JF-Expert Member
- Aug 29, 2021
- 2,308
- 7,366
Kwa tafasiri yako HAKAINDE HICHILEMA alikuwa Mwanamme wa Shoka hakuwahi kumpigia magoti Edgar Lungu, pamoja na mateso na kifungo cha muda mfupi hadi anaachiwa huru na leo ndio Raisi wa Zambia.1. Ni Majuha
2. Ni Wanafiki
3. Ni Waongo
4. Ni Waoga
5. Ni Wapenda Maslahi Binafsi
6. Wana Uwendawazimu wasioujua
7. Hawajiamini na ni Wachuuza Watu
Kuanzia leo naiombea CCM kwa Mwenyezi Mungu iendelee Kutawala nchini Tanzania mpaka pake Dunia itakapobadilika na nawaombeni Laana mbaya Wapinzani wote Tanzania.
Yaani Wewe Umeteswa, Umehangaishwa, Umesingiziwa, Umetishwa, Umefilisiwa na Umechafuliwa vya kutosha halafu unatoka Matesoni hata Kwako hujaenda haraka haraka unaenda Kujipendekeza kwa Waliokuchafua na Kukuumiza huku kila mara ukiongea kwa Kukunja mikono yako Kiuwoga na Ukitukenelia tu mimeno na kuahidi Ushirikiano.
Kuna Mtu nilimheshimu ila Kanikera!!!!
Uwongo mbaya Mbowe alikosea sana leo usiku kwenda kupiga picha za kificho na Rais Samia Suluhu Hassan