Kubadilisha gia angani kwa NECTA na maajabu Kemobos

Akina Diamond walotoboa ni wangapi ? Acha mzaha
Wengi, asilimia 70 ya matajiri ni la saba, asilimia 3 ya wasomi ndio matajiri, wengi wamo tra, tarura, tanesco, etc maisha yanafahamika, hata akijenga, inafahamika hela ametoa wapi😄🙆‍♀️
 
Cha ajabu sasa, mtaani wanatoboa akina diamond, hamonize, ali kiba, fei toto😂😂,
Huku hao wanaofaulu wakienda kufanya kazi serikalini, na wengi kuishia kuishi kwa kula milungula🤷‍♂️
Hao uliowataja fatilia watoto wao wamewapeleka shule gani utapata majibu kuwa shule Ina umuhimu kiasi gani
 
Necta walisema mapema sana mwaka 2022 kwamba kuanzia mwaka huu matokeo hayatatoa 10 bora. Walisema hivo kabla hata mitihani haijasahishishwa inawezekana hata iuanza ilikuwa haijaanza.
Point waliyotoa NECTA iko sahihi na serikali inatakiwa kuona ukweli huo. Hivi una akili timamua hata wewe unayeandika kunfananisha mtoto wa private na serikali? Mtoto anaamka asubuhi hajui kama atakula mchana, hana nauli, kwenye daladala anasukumwa sukumwa tu, njiani anakoswa koswa na bodaboda, akifika home wazazi wanaoigana au anapewa ubuyu na maandazi akauze, akirudi apike na kufanya kazi za ndani na wakqti huo umeme uneishq haqwzi kujisomea au anaishi nyumba haina uneme, bado hana madaftari na vitabu vya kusoma kwa sababu serikali haijapeleka vitabu mashuleni kwa ratio hata ya 1:2 ubakuta labda ration ni 1:10😐 na haviendi kila mwaka, je kama kuna mtoto kapoteza kitabu kitakuwa replaced vipi? Bado huyo mzazi hawezi afford vitabu kwa mtoto.Mtoro anarudi home anakuta hata chakula hamna. Mtoto wa tandale ubamfabanisha na mtoto wa Masaki uko sawa kichwani au ni USHABIKI NA MIHEMKO????😳🤔.
Na serikali hili waliangalie ndo maana walimu wanakuwa wakali kuoitikoza kwa sababu serikali inalazimisha wakimu wa serikali kufaulisha katika mazingira yasiyowezekana kabisa wanaguka mbogo kwa wanafunzi katika kutekeleza yasiyo wezekana
 
Na hata mitihani hapo baadae iwe tofauti... Kila mtu apimwe sawa na mazingira yake na vile alivyoandiliwa..
 
Shida yetu wa Tz kila kitu kupinga. Mimi niko upande wa NECTA, sababu walizotoa. Ifike sasa shule binafsi zitafute njia ya kujitangaza.
Kuna shule wanawachuja watoto mpaka wanabaki, wale wazuri kabisa.

Huwezi shindanisha na wa Serikali kwa hilo, kinachotakiwa wa Tz tupambane na Serikali, shule za Serikali zipewe kipaumbele. Fedha nyingi zinazopangiwa bajeti ya vitu visivyo vya muhimu, ziende kwenye elimu na zisimamiwe ipasavyo.

Tukajifunze Nairobi hapo, shule za Serikali unapigania kupeleka mtoto, labda sasa iwe imebadilika. Mazingira mazuri ya kusomea, walimu na vitendea kazi vikiwepo, shule za Serikali nazo zitafanya vizuri. Kuna watoto wenye uwezo mkubwa huko, ila sababu ni shule ya kata hawafanyi vizuri.
 
Elimu yetu si inapimwa kwa kufaulisha sasa wakifanya vizuri wakatangazwa si ndo kunachochea shule zingine zijitume zaidi au, nimeshuhudia MUSABE ikipeleka waalimu wake wakafanye masters abroad ili waje wafaulishe zaidi
Musabe wezi tu hao...wamefungiwa mwaka jana
 
Hyo shule naskia ni ya Mzee wetu wa mzoga.....sema wamejipanga haswaa ....skull buses zao ni yutong kama mabasi ya mkoani
 
Serikali hii ya CCM ni janga la kitaifa. Kukimbia tatizo sio suluhisho, Wanapaswa kuboresha shule za kata badala ya kuzifichia udhaifu. Kuficha kilema ni upumbavu wa kiwango cha juu.
 
Wewe ulivyobwabwaja, mbona haujagusia maelezo mengine muhimu ya "mweshimiwa" aliyetoa sababu za maana za kufuta utaratibu wa kutangaza top10?

Tena ile ya muhimu kabisa na yenye mashiko, kwamba hauwezi kuwashindanisha watoto wanaosomea katika mazingira tofauti umeiacha?

Kwa hiyo umeona uipigie Promo Kemobs, huku jambo hilo likiwa tayari limepigwa marufuku?

Kifupi unapimana ubavu na serikali, si ndiyo!

Utovu huu wa nidhamu ni kwa manufaa ya nani?
 
mi nataka kujua hivi miaka ya nyuma ,yaani miaka ya 2000yr kushuka chini walikuwa wakitangaza hizi top 10 !!??au watu mlikuwa mnajuana baada ya ku join form v huko ulikopangiwa!!
 
Knowladge & skills matters more than scoring. Nadhani debate ingeanzia hapo, kwanini tunawasomi wengi ambao hawana msaada?
 
Cha ajabu sasa, mtaani wanatoboa akina diamond, hamonize, ali kiba, fei toto😂😂,
Huku hao wanaofaulu wakienda kufanya kazi serikalini, na wengi kuishia kuishi kwa kula milungula🤷‍♂️
mbona hujawataja kina mwigulu nchemba?makamba,ridhiwani nk
 
Mazoea hujenga tabia. Huu utaratibu wa number ndo unashhusha quality ya elimu. Hauwi problem solving based. Yaani ni banking model inatumika. Pump watoto hadi lieleweke. Ndo maana mtoto wa form One anjifunza mambo ya form 3. Sasa huyo atapataa muda wa kujadili mada viz a viz inavyoweza kumsaidia kubadili mazingira yaliyomzunguka? Mwishowe anabaki facts za kukaririishwa tu. By january sylabus imeisha. Unafanya mitihani tu. Ukifika mtihani wa taifa you have met all possible questions. Hii model ya elimu ni mbaya sana. Inaagalia elimu kama accumulation of facts and not how those facts can change our own situation. Ndio maana katika nchi za wenzetu equivalent graduate na mtanzania ni mbingu na dunia. They are very skilled and competent. We have papers.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…