Inashangaza sana kusikia mtu anakebehi kuwa Ccm imelifanyia nini taifa hili ndani ya miaka sitini.
Pamoja na kuwa tulikuwa chini ya uangalizi wa UN mpaka tutapopata uhuru lakini mwangalizi wetu yaani Mwingireza hakufanya maendeleo ya maana kama katika makoloni yake ya kudumu kama Kenya na Zimbabwe. Hivyo mpaka anatupatia uhuru aliacha taifa letu lipo na hali mbaya ya kiuchumi na maendeleo.
Mw Nyerere alipopata uhuru aliandaa misingi mizuri ili kila mtu aweze kufaidi keki ya taifa hasa kwa kuanzisha siasa ya ujamaa na kujitegemea. Na ilikuwa na nia nzuri tu ila husuda za Mapebari wakamuangusha.
Tuachane na setbacks na mafanikio katika awamu zote tano mpaka hii ya mama Samia
Ukweli ni kuwa kwa taifa lililokuwa halina kitu kimaendeleo, leo hii tunamiundombinu iliyosimama ya barabara, afya,elimu hadi viwanda. Si busara kuibeza Ccm ambayo iliachiwa nchi ikiwa masikini kabisa kwa kila namna. Na leo hii tupo hii stage.
Kwani mnaobeza mlitaka tuwe kama Usa ambao wanamiaka zaidi ya mia mbili tangu wapate uhuru?
Kwanza kigezo kikubwa cha kusema kwamba ccm imefeli ni kwa sababu imeshindwa kutekeleza ahadi zake yenyewe. Nyerere alianza vizuri, pamoja na makosa aliyofanya ya kutaifisha mali mbalimbali na kuegemea ujamaa.
Nyerere alipatia kwa kuwekeza kwenye KILIMO na kuwa very serious na kilimo. Kosa kubwa la ccm ni kuwaacha solemba wananchi na kujitajirisha binafsi, na kukiweka kando kilimo.
Miaka 60 iliyopita tulikuwa sambamba na nchi mbalimbali kama South Korea, na zile za mashariki ya mbali. Leo sisi ni mafukara wa kutupa.
Serikali, kwa mfano, inatakiwa kupima maeneo ambayo watu wanatakiwa kujenga nyumba (residential ), na wapeleke huko huduma zote, umeme, maji safi na taka, nk. Na kama mtanzania anaanza kujenga sehemu isiyotakiwa, basi ni jukumu la serikali kumzuia ili kidogo alichonacho akitumie vizuri na kwa faida ya familia. Serikali sikivu ya ccm imefanya nini? Haikupima viwanja, haikuzuia wananchi kujenga sehemu zisizotakiwa. Ila imeona ni ufahari kuwabomolea nyumba wananchi maskini, bila fidia. Huu ni UJAMBAZI wa Dola dhidi ya raia wake. Ni CANNIBALISM kwa kweli.
Leo tunaongea habari ya machinga. Machinga ni matokeo ya kufeli au kutokuwepo kwa sera muhimu. Kudharau kilimo, kusimamisha ajira, kuwa na tafsiri potovu ya MAENDELEO, na mengineyo. Maendeleo ni ya watu, siyo vitu. Magufuli alisimamisha ajira ili ajenge miundombinu. Wakati idadi ya wanafunzi ikipanda sana kwa sababu ya "elimu bure", yeye haajiri waalimu. Matokeo yake katuachia BOMU.
Ushamba wa Magufuli pia umeigharimu nchi. Ananunua ndege bila plani, tena ananunua keshi, sababu anajua bila kufanya hivyo asingeweza kununua. Nani atakufanyia credit au hata lease, kama huna "sound business plan"?
Of course ukinunua keshi, hata ukiamua kuipaki au kufugia sungura, nobody gives a damn.
Kwa ujinga huu iliotufikisha hapa, mamilioni ya watanzania ni fukara wa kutupa, nani mwenye akili timamu atasifia?
Watu wanasingizia ooh, watanzania wavivu! Wavivu gani wanalima kahawa inanunuliwa sh 5,000 kwa kilo, ilhali Uganda na Kenya wananunua sh. 20,000? Kwa nini mty asipeleke huko?
Bangi ina matumizi ya hospitali, ingeweza kulimwa kwa leseni maalum na watu wangepata ajira. Leo ma DC mazuzu wanaona fahari kutumia fedha ya serikali kuabdaa operesheni za kuchoma moto mashamba ya bangi, tena na kubeba vyombo vya habari kuionesha dunia jinsi "wanavyowajibika". Kuna kitu hapo?
Miaka 60 ya Uhuru ni kuadhimisha Total failure ya ccm, crashing defeat na upumbavu uliokithiri, to say the least