Kubeza maendeleo yaliyoletwa na CCM ndani ya miaka 60 ni kukosa busara. Tulipata uhuru tukiwa nyuma sana kimaendeleo

Mkuu maendeleo ni concept inayochagizwa na time, time ndiyo driving force ya maendeleo, hata kama tungebaki na wakoloni tungekipata tu hiki unachokiita maendeleo. Suala ni kwanini tumetumia miaka 60 kuanza kutambaa wakati wenzetu wenye umri sawa na sisi wanakimbia? Jibu ni Viongozi kukosa maono na kushindwa kuutumia muda (time) katika kujenga taswira ya maendeleo. Leo kila uchwao tunazungumzia kujenga shule na kuchonga madawati as if ni jambo jipya.
 
Ni AIBU kwa NCHI yenye Miaka 60 ya Uhuru na Raslimali za Kutisha Haina Maendeleo na Wananchi wake mnawaita WANYONGE
Jiulize Nchi zilizokuwa Kundi moja na Tanzania kwa Umaskini leo zimekuwa Nchi zenye Maendeleo Makubwa tunawategemea Watupe Misaada wakati sisi tuna
Madini Aina zote
Bahari
Maziwa
Mbuga za Wanyama
Ardhi nzuri kwa Kilimo
Mabonde
GAS
MITO n.k

bila shaka huna ham ya kuona nchi zinzosema zmeendelea zikoje upande wa pili, uchumi sio mrahisi ivo
 
Acha uongo wako, maendeleo ni wananchi kumudu basic needs na sio wingi wa maghorofa mjini.
Kama hadi leo watz wanaishi kwenye nyumba za nyasi kama panya utasema vipi kuna maendeleo
 
Mtoto kazaliwa na kilo 2, baada ya muda miaka 10 ana kilo 5. Ni kweli kaongezeka, swali ni je huo uzito unaendana na umri wake?

Vipi watoto wengine aliozaliwa nao, wana uzito gani sasa hivi?
Huu mfano sio relevant na kuleta maendeleo ya nchi.
 
Acha uongo wako, maendeleo ni wananchi kumudu basic needs na sio wingi wa maghorofa mjini.
Kama hadi leo watz wanaishi kwenye nyumba za nyasi kama panya utasema vipi kuna maendeleo
Compare and contrast wakati tunapata uhuru na leo hii baada ya miaka 60 ndio utajua namaanisha nini.
 
Mkuu maendeleo ni concept inayochagizwa na time, time ndiyo driving force ya maendeleo, hata kama tungebaki na wakoloni tungekipata tu hiki unachokiita maendeleo. Suala ni kwanini tumetumia miaka 60 kuanza kutambaa wakati wenzetu wenye umri sawa na sisi wanakimbia? Jibu ni Viongozi kukosa maono na kushindwa kuutumia muda (time) katika kujenga taswira ya maendeleo. Leo kila uchwao tunazungumzia kujenga shule na kuchonga madawati as if ni jambo jipya.
Shule na madawati ni suala linaloendana na kukua kwa population. Hivyo wakati mwingine sio la kulaumu sana, serikali inajitahidi maana kila miaka watu wanazaliana na population kubadilika.
 
Mtoto kazaliwa na kilo 2, baada ya muda miaka 10 ana kilo 5. Ni kweli kaongezeka, swali ni je huo uzito unaendana na umri wake?
Swali zuri sana hilo bwashee. Chadema ina miaka zaidi ya 25 ya uhai, lakini mpaka sasa haina hata kiwanja cha kujenga ofisi ya makao makuu! Hitimisho: chadema ni kama huyo mtoto 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Inashangaza sana kusikia mtu anakebehi kuwa Ccm imelifanyia nini taifa hili ndani ya miaka sitini.

Pamoja na kuwa tulikuwa chini ya uangalizi wa UN mpaka tutapopata uhuru lakini mwangalizi wetu yaani Mwingireza hakufanya maendeleo ya maana kama katika makoloni yake ya kudumu kama Kenya na Zimbabwe. Hivyo mpaka anatupatia uhuru aliacha taifa letu lipo na hali mbaya ya kiuchumi na maendeleo.

Mw Nyerere alipopata uhuru aliandaa misingi mizuri ili kila mtu aweze kufaidi keki ya taifa hasa kwa kuanzisha siasa ya ujamaa na kujitegemea. Na ilikuwa na nia nzuri tu ila husuda za Mapebari wakamuangusha.

Tuachane na setbacks na mafanikio katika awamu zote tano mpaka hii ya mama Samia
Ukweli ni kuwa kwa taifa lililokuwa halina kitu kimaendeleo, leo hii tunamiundombinu iliyosimama ya barabara, afya,elimu hadi viwanda. Si busara kuibeza Ccm ambayo iliachiwa nchi ikiwa masikini kabisa kwa kila namna. Na leo hii tupo hii stage.

Kwani mnaobeza mlitaka tuwe kama Usa ambao wanamiaka zaidi ya mia mbili tangu wapate uhuru?
Kwanza kigezo kikubwa cha kusema kwamba ccm imefeli ni kwa sababu imeshindwa kutekeleza ahadi zake yenyewe. Nyerere alianza vizuri, pamoja na makosa aliyofanya ya kutaifisha mali mbalimbali na kuegemea ujamaa.

Nyerere alipatia kwa kuwekeza kwenye KILIMO na kuwa very serious na kilimo. Kosa kubwa la ccm ni kuwaacha solemba wananchi na kujitajirisha binafsi, na kukiweka kando kilimo.

Miaka 60 iliyopita tulikuwa sambamba na nchi mbalimbali kama South Korea, na zile za mashariki ya mbali. Leo sisi ni mafukara wa kutupa.

Serikali, kwa mfano, inatakiwa kupima maeneo ambayo watu wanatakiwa kujenga nyumba (residential ), na wapeleke huko huduma zote, umeme, maji safi na taka, nk. Na kama mtanzania anaanza kujenga sehemu isiyotakiwa, basi ni jukumu la serikali kumzuia ili kidogo alichonacho akitumie vizuri na kwa faida ya familia. Serikali sikivu ya ccm imefanya nini? Haikupima viwanja, haikuzuia wananchi kujenga sehemu zisizotakiwa. Ila imeona ni ufahari kuwabomolea nyumba wananchi maskini, bila fidia. Huu ni UJAMBAZI wa Dola dhidi ya raia wake. Ni CANNIBALISM kwa kweli.

Leo tunaongea habari ya machinga. Machinga ni matokeo ya kufeli au kutokuwepo kwa sera muhimu. Kudharau kilimo, kusimamisha ajira, kuwa na tafsiri potovu ya MAENDELEO, na mengineyo. Maendeleo ni ya watu, siyo vitu. Magufuli alisimamisha ajira ili ajenge miundombinu. Wakati idadi ya wanafunzi ikipanda sana kwa sababu ya "elimu bure", yeye haajiri waalimu. Matokeo yake katuachia BOMU.

Ushamba wa Magufuli pia umeigharimu nchi. Ananunua ndege bila plani, tena ananunua keshi, sababu anajua bila kufanya hivyo asingeweza kununua. Nani atakufanyia credit au hata lease, kama huna "sound business plan"?

Of course ukinunua keshi, hata ukiamua kuipaki au kufugia sungura, nobody gives a damn.

Kwa ujinga huu iliotufikisha hapa, mamilioni ya watanzania ni fukara wa kutupa, nani mwenye akili timamu atasifia?

Watu wanasingizia ooh, watanzania wavivu! Wavivu gani wanalima kahawa inanunuliwa sh 5,000 kwa kilo, ilhali Uganda na Kenya wananunua sh. 20,000? Kwa nini mty asipeleke huko?

Bangi ina matumizi ya hospitali, ingeweza kulimwa kwa leseni maalum na watu wangepata ajira. Leo ma DC mazuzu wanaona fahari kutumia fedha ya serikali kuabdaa operesheni za kuchoma moto mashamba ya bangi, tena na kubeba vyombo vya habari kuionesha dunia jinsi "wanavyowajibika". Kuna kitu hapo?

Miaka 60 ya Uhuru ni kuadhimisha Total failure ya ccm, crashing defeat na upumbavu uliokithiri, to say the least
 
Swali zuri sana hilo bwashee. Chadema ina miaka zaidi ya 25 ya uhai, lakini mpaka sasa haina hata kiwanja cha kujenga ofisi ya makao makuu! Hitimisho: chadema ni kama huyo mtoto 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Mtaji wa CHADEMA ni watanzania, ccm wanaiogopa sana kiasi kwamba hawathubutu kuendesha uchaguzi huru. Rais Samia mwanzo alisema atakutana na vyama vya Upinzani , na CHADEMA walimuandikia barua wakutane, akakubali. Weeee! Ccm wakamwambia hivi unajipenda? Ukishaongea na hao jamaa ukaweka uwanja uwe sawa, huna chako. Hapa tunaishi kwa kuwadhibiti tu!

Nyie ccm wezi na mafisasi, jengeni hayo magorofa yenu. CHADEMA ofisi zao ziko kwenye mioyo ya watanzania.

Enzi za Dijitali wala huhitaji maofisi ya ajabu. Kalagabaho
 
Inashangaza sana kusikia mtu anakebehi kuwa Ccm imelifanyia nini taifa hili ndani ya miaka sitini.

Pamoja na kuwa tulikuwa chini ya uangalizi wa UN mpaka tutapopata uhuru lakini mwangalizi wetu yaani Mwingireza hakufanya maendeleo ya maana kama katika makoloni yake ya kudumu kama Kenya na Zimbabwe. Hivyo mpaka anatupatia uhuru aliacha taifa letu lipo na hali mbaya ya kiuchumi na maendeleo.

Mw Nyerere alipopata uhuru aliandaa misingi mizuri ili kila mtu aweze kufaidi keki ya taifa hasa kwa kuanzisha siasa ya ujamaa na kujitegemea. Na ilikuwa na nia nzuri tu ila husuda za Mapebari wakamuangusha.

Tuachane na setbacks na mafanikio katika awamu zote tano mpaka hii ya mama Samia
Ukweli ni kuwa kwa taifa lililokuwa halina kitu kimaendeleo, leo hii tunamiundombinu iliyosimama ya barabara, afya,elimu hadi viwanda. Si busara kuibeza Ccm ambayo iliachiwa nchi ikiwa masikini kabisa kwa kila namna. Na leo hii tupo hii stage.

Kwani mnaobeza mlitaka tuwe kama Usa ambao wanamiaka zaidi ya mia mbili tangu wapate uhuru?
Kati ya watu milioni 60 ni wangapi wanafaidi keki ya taifa? Kuna wachache wanaishi kama wafalme, waliobaki wana umasikini wa kutupa. Wananuka umasikini mpaka wanatia huruma. Yote hayo ni matunda ya siasa za ujamaa alizoanzisha Nyerere.
 
Inashangaza sana kusikia mtu anakebehi kuwa Ccm imelifanyia nini taifa hili ndani ya miaka sitini.

Pamoja na kuwa tulikuwa chini ya uangalizi wa UN mpaka tutapopata uhuru lakini mwangalizi wetu yaani Mwingireza hakufanya maendeleo ya maana kama katika makoloni yake ya kudumu kama Kenya na Zimbabwe. Hivyo mpaka anatupatia uhuru aliacha taifa letu lipo na hali mbaya ya kiuchumi na maendeleo.

Mw Nyerere alipopata uhuru aliandaa misingi mizuri ili kila mtu aweze kufaidi keki ya taifa hasa kwa kuanzisha siasa ya ujamaa na kujitegemea. Na ilikuwa na nia nzuri tu ila husuda za Mapebari wakamuangusha.

Tuachane na setbacks na mafanikio katika awamu zote tano mpaka hii ya mama Samia
Ukweli ni kuwa kwa taifa lililokuwa halina kitu kimaendeleo, leo hii tunamiundombinu iliyosimama ya barabara, afya,elimu hadi viwanda. Si busara kuibeza Ccm ambayo iliachiwa nchi ikiwa masikini kabisa kwa kila namna. Na leo hii tupo hii stage.

Kwani mnaobeza mlitaka tuwe kama Usa ambao wanamiaka zaidi ya mia mbili tangu wapate uhuru?
Utakuwa hujui maendeleo au Hujaona maendeleo wewe. Anyway, Tulitaka tuwe kama Singapore au South Korea.
 
Inashangaza sana kusikia mtu anakebehi kuwa Ccm imelifanyia nini taifa hili ndani ya miaka sitini.

Pamoja na kuwa tulikuwa chini ya uangalizi wa UN mpaka tutapopata uhuru lakini mwangalizi wetu yaani Mwingireza hakufanya maendeleo ya maana kama katika makoloni yake ya kudumu kama Kenya na Zimbabwe. Hivyo mpaka anatupatia uhuru aliacha taifa letu lipo na hali mbaya ya kiuchumi na maendeleo.

Mw Nyerere alipopata uhuru aliandaa misingi mizuri ili kila mtu aweze kufaidi keki ya taifa hasa kwa kuanzisha siasa ya ujamaa na kujitegemea. Na ilikuwa na nia nzuri tu ila husuda za Mapebari wakamuangusha.

Tuachane na setbacks na mafanikio katika awamu zote tano mpaka hii ya mama Samia
Ukweli ni kuwa kwa taifa lililokuwa halina kitu kimaendeleo, leo hii tunamiundombinu iliyosimama ya barabara, afya,elimu hadi viwanda. Si busara kuibeza Ccm ambayo iliachiwa nchi ikiwa masikini kabisa kwa kila namna. Na leo hii tupo hii stage.

Kwani mnaobeza mlitaka tuwe kama Usa ambao wanamiaka zaidi ya mia mbili tangu wapate uhuru?
Naunga mkono hoja.
P
 
Bora kukosa busara kuliko kukosa akili kwa kufikiria maendeleo yameletwa na CCM badala ya WATANZANIA WENYEWE. Mshajiona wenye nchi kiasi kwamba CCM ni muhimu kuliko Tanzania? 😡
Hauhitaji kuwa na ubongo ili uwe CCM. Hata mende anaweza kuwa mwanaCCM
 
Inashangaza sana kusikia mtu anakebehi kuwa Ccm imelifanyia nini taifa hili ndani ya miaka sitini.

Pamoja na kuwa tulikuwa chini ya uangalizi wa UN mpaka tutapopata uhuru lakini mwangalizi wetu yaani Mwingireza hakufanya maendeleo ya maana kama katika makoloni yake ya kudumu kama Kenya na Zimbabwe. Hivyo mpaka anatupatia uhuru aliacha taifa letu lipo na hali mbaya ya kiuchumi na maendeleo.

Mw Nyerere alipopata uhuru aliandaa misingi mizuri ili kila mtu aweze kufaidi keki ya taifa hasa kwa kuanzisha siasa ya ujamaa na kujitegemea. Na ilikuwa na nia nzuri tu ila husuda za Mapebari wakamuangusha.

Tuachane na setbacks na mafanikio katika awamu zote tano mpaka hii ya mama Samia
Ukweli ni kuwa kwa taifa lililokuwa halina kitu kimaendeleo, leo hii tunamiundombinu iliyosimama ya barabara, afya,elimu hadi viwanda. Si busara kuibeza Ccm ambayo iliachiwa nchi ikiwa masikini kabisa kwa kila namna. Na leo hii tupo hii stage.

Kwani mnaobeza mlitaka tuwe kama Usa ambao wanamiaka zaidi ya mia mbili tangu wapate uhuru?
Ndani ya miaka 60 ccm imetufanya masikini zaidi watz huku kikundi kidogo cha wanaccm na ndugu zao na marafik zao wakiishi maisha ya kifahar kwa kodi zetu tunataka katiba mpya na tume huru ya uchaguz
 
Back
Top Bottom