Kubezwa kwangu kulinipunguzia presha nikawa mshindi vipindi vyote

Kubezwa kwangu kulinipunguzia presha nikawa mshindi vipindi vyote

Tuendeleee........

Nilipokuwa skul nilikuwa nasujuda sana dancing ya music kwenye matamasha na mashindano nilikuwa nashiriki sana.

Ilikuwa form three mwishoni yan likizo ya mwez wa 12 ambapo mwaka mpya nilikuwa naanza form 4.

Siku hiyo ilikuwa ni mkesha wa mwaka mpya nilienda disco vumbi huko kwetu kijijini. Kwasababu nilikuwa mahili katika kudance basi washkaji zangu walinichukua tukaenda disco. Nilifanya yangu huko disco mpka mishale ya saa5 usiku ndo nikarudi home.

Nilipofika home geto letu na bro wangu lilikuwa limejitenga na nyumba kubwa kwahiyo haikuwa rahisi wazaz kuniskia wakati niliporudi kulala.

Nilipoingia magetoni nilimkuta bro akiwa na rafkiake anayeitwa Atanazi. Bro alinifokea kwasababu ya kwenda disco alisema ni uhuni.
Atanazi akadakia akasema "wewe form four utafeli akili huna" yale maneno yaliniuma lakini kikaitikia tu "oky'

Atanazi alikuwa kamaliza form four mwaka ule kwahiyo alikuwa anasubiri matokeo.

Siku zikaenda nikaanza form four na matokeo ya akina Atanazi yakatoka. Atananzi aliyeniambia nitafeli akaanza kufeli yeye kwani matokeo yalivotoka alipata four ya 29 na alikuwa anaaminika sana kwani primary alikuwa kichwa sana alikuwa anaongoza.

Nilivokuwa nikirud likizo home nikikutana na Atanazi barabarani ananambia mdogo wangu matokeo yamekuja ndivo sivyo yani sikutarajia kabisa. Nikawa naona huyu anajikomba komba anajiskukia nikawa namuitikia tu.

Ilipofika mwez wa 9 nipo form four hiyo, idad kubwa ya wanafunzi tulianza kuwa watukutu yani tulikuwa na uhuni wa kirimbukeni kujiona miamba ya skul.

Headmaster akaanza operation ya kuondoa watukutu na kuwahamishia day kuwatoa bweni.
Namkumbuka sana na namshukuru madam mmoja anaitwa madam Zaudyati alinifata akanambia "nikuibie siri staff miongoni mwa majina ya wanafunzi ambao wanafatiliwa kwa ukaribu ili waondoshwe bweni nawewe umo kwahyo nakuomba ubadirike ili usifukuzwe bweni".

Nilimshukuru sana madam, kiukweli nilibadirika na walifukuzwa wengine ila mimi sikufukuzwa.
Tulifanya necta na bahati mbaya ile wiki ya kumaliza practicals nikapata taarifa bro angu mkubwa ukiachana na yule tulokuwa ote form four amefariki nilipata stress lakini nilimshukuru nilimaliza practicals vizuri.

Matokeo yalitoka na Mungu anasaidia tulipasi wote mimi na bro na home wote walifurahi.

Bro alinikumbusha maneno ya Atanazi nikabaki najichekea mwenyewe kwani atana6baada ya kuskia nimefaulu alibak anawaza yani yeye kichwa kadunda halafu mimi kilaza kilaza tu pangu pakavu nimepasi yani alikosa raha kabisa.


See you...........
 
Jikite kwenye mada wewe acha tabia za ki adriz
adriz Mwambie Maghayo mpepe sio kitu kizuri😄😂
FB_IMG_17092921407334428.jpg
 
Kwaio ndugu yangu ulitaka watu wote mlingane umri? Italeta vipi maana halisi ya maisha na kuishi? Haina maana yoyote kwako kuwahi kuzaliwa na yeye kuchelewa.....Generation zitaendelea kuwepo
Mwaka 2000 umezalisha generation nyingine kabisa, Mimi hapa nilipo sina utofauti na Sokwe Mzee alieikwepa Mishale mingi wajukuu zangu mna mengi ya kujifunza
 
Mwaka niliograduate University ,ndo dogo anamaliza la7🤣🤣sisomi Tena nyuzi zake,ndo anabalehe,hapo aliko shawaha bado zinanuka ule uchangah

Kumbe kalisoma diploma,manake kamejisifu kalisoma chuo,kumbe chuo Cha kata mamaeeh 🤧🤧🤧
Nakaweka ignore list asap,sitaki kusoma story za teeneger,it's rubbish.
Kaka naona umemkosea heshima sana member mwenzetu hapa jukwaani, huyu atakuwa ni mtu mzima regardless of his age. Hapa jukwaani tukisema sote tuwe na msimamo kama wako hakika jukwaa litakufa kabisaaa.
Naamini kuna watu wanakuzidi sana umri pengine ni kama baba zako ila kutwa kucha mnapishana na kufarakana kwa hoja na kwa heshima kabisa. By the way kuwa na umri mkubwa siyo sifa ya kujifanya ujikweze na kuwadharau uliowazidi umri.
 
Kaka naona umemkosea heshima sana member mwenzetu hapa jukwaani, huyu atakuwa ni mtu mzima regardless of his age. Hapa jukwaani tukisema sote tuwe na msimamo kama wako hakika jukwaa litakufa kabisaaa.
Naamini kuna watu wanakuzidi sana umri pengine ni kama baba zako ila kutwa kucha mnapishana na kufarakana kwa hoja na kwa heshima kabisa. By the way kuwa na umri mkubwa siyo sifa ya kujifanya ujikweze na kuwadharau uliowazidi umri.
Ana ka ujinga fulani kichwani,licha ya kupata elimu yake ya chuo lakini bado haikumsaidia
 
Back
Top Bottom