Kuchanganya vihusishi 'na' na 'Kwa' katika matumizi ni kosa kubwa na ni tabia mbaya sana

secretarybird

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
23,984
Reaction score
51,055
Vihusishi 'na' na 'kwa' vinakosewa sana katika matumizi kiasi cha kuleta mkanganyiko katika mawasiliano ya kila siku.

Kwa mfano, mtu anasema "Nilisafiri na gari", badala ya "Nilisafiri kwa gari". Ukisema nisafiri na gari unamaanisha wewe unatembea mwenyewe na gari linatembea mwenyewe, Wala hujapanda kwenye gari.

Yaani ukichanganya matumizi ya vihusishi hivi tajwa mbele yangu nakuweka vibao au ngumi kadhaa kisha nakurekebisha.

Haya!
 
"Nilisafiri na gari" ni kama umelichukua gari ukaliweka katika lori umelibeba halafu ukasafiri nalo.
 
Huwa sipendi kuumiza sana kichwa naulizaga Ai.
Majibu haya hapa mtoa mada .

"Hoja iliyoandikwa kwenye hiyo mada ya JamiiForums ina sehemu iliyo sahihi na sehemu isiyo sahihi kabisa. Hebu tuiangalie kwa utulivu wa kisarufi.
1️⃣ Hoja yake kuu
Mwandishi anasema:
Watu wanapaswa kusema “Nilisafiri kwa gari”
Na kusema “Nilisafiri na gari” ni kosa.
Hapa ndipo panahitaji ufafanuzi.
2️⃣ Ukweli wa kisarufi
Katika Kiswahili sanifu, vihusishi hivi vina kazi tofauti:
“Kwa”
Hutumika kuonyesha njia au chombo kilichotumika kufanya jambo.
Mfano:
Nilisafiri kwa gari
Aliandika kwa kalamu
Walikata mti kwa shoka
Hapa gari ni chombo cha usafiri.
“Na”
Hutumika kuonyesha kuandamana au kuwa pamoja na kitu au mtu.
Mfano:
Nilisafiri na rafiki yangu
Alikuja na mtoto wake
3️⃣ Lakini je “nilisafiri na gari” ni kosa?
Si lazima iwe kosa kabisa.
Kwa matumizi ya kawaida ya mazungumzo ya kila siku, “nilisafiri na gari” inaweza kueleweka vizuri, hasa ikiwa maana ni:
Ulikuwa na gari lako wakati wa safari
Mfano:
Nilienda Dodoma na gari langu.
Hapa maana inaeleweka vizuri.
4️⃣ Kosa lililopo kwenye hoja ya mwandishi
Sehemu hii si sahihi:
“Ukisema nilisafiri na gari maana yake wewe unatembea mwenyewe na gari linatembea lenyewe.”
Hii si tafsiri sahihi ya sarufi ya Kiswahili.
Katika matumizi ya lugha, “na” haimaanishi lazima kila kitu kitende kivyake.
Ni kuonyesha kuandamana au umiliki.
5️⃣ Hitimisho
Kwa hiyo:
“Nilisafiri kwa gari” → sahihi sana (inaonyesha chombo cha usafiri)
“Nilisafiri na gari” → inaweza pia kueleweka, hasa kwenye mazungumzo ya kawaida
Hoja ya kwamba “na gari” ni kosa kabisa → imezidishwa kidogo
✔️ Kwa kifupi:
Hoja ya huyo mwandishi ina msingi wa sarufi, lakini imeelezwa kwa ukali kuliko inavyotakiwa."
 
We ni mvivu jamani😁
 
Lakini je “nilisafiri na gari” ni kosa?
Si lazima iwe kosa kabisa.
Kwa matumizi ya kawaida ya mazungumzo ya kila siku, “nilisafiri na gari” inaweza kueleweka vizuri, hasa ikiwa maana ni:
Ulikuwa na gari lako wakati wa safari
Mfano:
Nilienda Dodoma na gari langu.
Hapa maana inaeleweka vizuri.
Huyu AI wako naye anahitaji kichapo cha mbwa aliyeiba mboga ya jirani.

Mimi sijasema mtu akisema, "Nilisafiri na gari haeleweki", nimesema kuwa si sahihi japo unaweza ukaeleweka ukisema hivyo.

AI ya hovyo kweli yaani.

Seran.
 
Back
Top Bottom