Kuna tofauti kati ya israeli kuchaguliwa na Mungu kua taifa lake teule lakumwelezea hapa duniani na wayahudi kumkubali yesu.kwasababu yesu aliikuta tayari israeli imeshachaguliwa kua teule.Kwa mujibu wa vitabu vya dini ya kikristo vinaonyesha mahusiano ya wayahudi na Mungu yalikuwepo miaka mingi iliyopita kabla ya yesu kuja na badae kukapita kipindi cha maasi na Mungu akawaacha hadi walipomrudia Mungu nayeye akamtuma yesu kuja kuwakomboa.Yesu alikuja kwa ajili yakukomboa binadamu wote ila wayahudi walitumika kama kielelezo kuwakilisha wanadamu wote.sasa swala la wao kutokumkubali yesu hiyo ni shida yao kwasababu sio lazima wawe wote wanaomkubali ndio ujue Mungu aliwateua.Ila kupitia wao kama kiwakilishi imani ya yesu imeenea dunia nzima na ilo ndilo lilikua lengo la Mungu.Mungu akuwateua ili wawe watakatifu bali wafanye kile ambacho alikusudia na kupitia wachache kazi imefanyika na sasa inafanywa na mataifa mengine ila lengo ni lile lile kuhubiri injili kwa kila taifa na kabila..Ukisoma biblia yako vizuri yote utayaona uko.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mathayo 21
33. Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.
34. Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake.
35. Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe.
36. Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile.
37.
Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu.
38. Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.
39. Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu,
wakamwua.
40. Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima?
41. Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya;
na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.
42. Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,
Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?
43. Kwa sababu hiyo nawaambia,
Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao
watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.
👉Kwa maana waitwao ni wengi, bali
wateule ni wachache. ~Mathayo 22:14