#COVID19 Kudhibiti maambukizi ya COVID-19: Wasafiri kutoka Tanzania wapigwa marufuku kuingia Uingereza

Wala sichoki kuwaelimisha
Mmesikia kuna Corona maalum imegundulika South Africa ambayo ni COVID19 lakini imebadilika na ni kali ? Inaitwa South African variant au strain? Sasa hii Corona ya Sauzi haitibiki na antibiotics etc walizotumia kupunguza makali ya Corona, pia chanjo inaonekana kutosaidia! So ni kitu kipya na inaua sana! Sasa UK wanasema Tanzania tunasambaza hiki so hawataki tuwapelekee - Nchi zilizoendelea zimelipa gharama kubwa kupata chanjo na kuwafungia raia wao wasiambukizwe - wanajiandaa kuwachanja wote warudi kwenye shughuli zao! Nyie bado mnazurura bila kujikinga mnataka kuzua balaa nyingine - hawataki masihara!
Wameanza Uingereza lakini tukiendelea kupuuza na kutochukua hatua tutafungiwa na nchi zingine pia! MATAGA waache uongo eti nchi zingine zimepigwa ban - Kenya, Rwanda, Uganda wanaruhusiwa kuingia UK bila shida! Why Tanzania na DRC? Acheni kupotosha umma!
Pili sisi wenyewe tujue Corona hii ya Sauzi ni hatari kuliko ile ya mwanzo na Afrika inaonekana kupigwa nayo ndo maana mnaona mawaziri huko Zimbabwe, South Afrika wanakwenda!
Narudia tuchukue hatua madhubuti kama Taifa dhidi ya Corona na tufanye mapema kabla hatujatengwa!
Wewe binafsi JIKINGE
#TutaelewanaTu #ChangeTanzania
Hivi Mkuu wa nchi na wataalamu wetu wana ona shida gani kutuambia tujikinge? Kama ipo isitupate. Kama haipo hatuta kuwa tume poteza chochote.
Ni heri kinga kuliko tiba..
 
Wakati mnatengeneza pesa wao watakuwa wamelala tu?The answer is this: Every country must be integrated well in the world.
Sasa Hivi tujikite kutengeneza fedha, baadaye dawa rasmi ikipatikana tutaenda. Waache waje tupate pesa, sie tujifukize tusife ili siku za usoni waone kuwa wao walikosea.
 
Tatizo hata Kama Aga Khan wanatibu Ni Watanzania wangapi wanaweza kumudu gharama zao?!
 
Ndugu achana na propaganda, ugonjwa wa COVID-19 na kujigawa kwake kwa virusi vingine vya Afrika kusini, Nigeria na Brazil upo kila nchi na kila nchi itambana nao kwa uwezo walio nao.

Hizi variants za ugonjwa pia zimegundulika Ujerumani na baadhi ya nchi zinazitokeza kusema zimegundua hizi variants.

Variants ni jinsi kirusi kinavyojibadili kulingana na mazingira ya sehemu na aina ya watu waliopo hapo.

Hivyo hata umoja wa Ulaya nao wanapanga kuwazuia raia na wakazi wa Uingereza kuingia kwenye hizo nchi kama Ujerumani.

Kama hufahamu mwezi December mwaka jana nchi nyingi za jumuiya ya Ulaya zilizuia ndege za kutoka UK kuingia katika nchi hizo.

Hivi sasa wanapanga hatua zaidi na wanawalenga Uingereza.

Soma hapa:

Individual EU countries could temporarily ban all UK residents - the new proposal explained (msn.com)

Tusiwe wajinga wa kukumbatia kila propaganda.
 
Yule balozi wao aliyeambiwa na jiwe awaonye wale wengine badala yake naye kawa mshirika wa kutufungia mlango?

Kama shere dunia kweli imetupata.

Twachezwa shere kila upande.
JPM anafikiria wazungu ni watu wa mchezo....na bado..huwezi kumdanganya mtu mwenye akili...aendelee kutoa watanzania sadaka tu.
 
Kwenu kuna Nimonia tu
 
Kama hukwenda darasani huwezi kujua umuhumu wa data.
ulienda darasani na unatizama data kama mkombozi wa ugonjwa wa mlipuko usio na tiba!!!

tofauti yako na tofali la kukalia ni nini????
 
Baki kwenu kwani ni lazima uende kwa mabeberu?
 
ulienda darasani na unatizama data kama mkombozi wa ugonjwa wa mlipuko usio na tiba!!!

tofauti yako na tofali la kukalia ni nini????
Unafikiri dawa zinapatikana kwa kuokotwa barabarani watu wamefanya research nyingi kabla na huwezi kufanya research bila data.
 
Kirusi kimegunduliwa Afrika Kusini lakini wanaozuiwa ni Watanzania na Wakongo,,,,,,sielewi.
 
Japo sijafungua link...Ila sisi tunawapokea wazungu kwa vigezo kuwa wao ni watalii na wanachangia pato la Taifa.
Sasa watakuwa hawaji maana watakuwa hawaruhusiwi kurudi Uingereza ikiwa wametokea tanzania. This is to block even litle tourists who used ti believe Tz is safe
 
Kuna wakati tuseme ukweli zaidi kuliko kusema siasa zaid,laiti kama Corona ingekuwepo kama inavyoonekana kuwepo katika mataifa mengine,na laiti kama wazee tungekuwa tunaishi kama tunavyoishi sasa na Corona ikawa kama ilivyo kwingine,basi Tanzania nzima hadi sasa maiti zingekuwa zikiliwa na kunguru barabarani,itoshe tu kusema Corona ipo na tahadhari zichukuliwe.
Kama watanzania watakataliwa kwenda sehemu nyingine kwa sababu kuna Corona,kwanini tung'ang'ani nchi za watu,hata bila COorna tungezuiana tu kuingia kwenye za watu maana yapo mengi ya kusababisha tuzuiane ila siyo kuja na kusingizia Corona,ajabu sana kuona watu wanadanganyika kwa kugeuzwa uongo kuwa ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…