#COVID19 Kudhibiti maambukizi ya COVID-19: Wasafiri kutoka Tanzania wapigwa marufuku kuingia Uingereza

#COVID19 Kudhibiti maambukizi ya COVID-19: Wasafiri kutoka Tanzania wapigwa marufuku kuingia Uingereza

Wewe ulitakaje mkuu .. ukae ndani usifanye kazi? Kampeni zimepita kina lissu walikuwa wanakusanya watu alipata hiyo corona ?!

Haya ni mafua makali na tuna njia zetu wenyewe za kudhibiti
Virus havina mipaka kwamba utajifungia kwenye nchi yako ujitibu huku ukitarajia kwenda nje au kupokea wageni toka nje.

Kuna vyombo kama WHO vyenye mamlaka ya ku control yanapotokea magonjwa kama hayo duniani.
 
Mwisho wa tamaa ni aibu...hii serikali haiko makini na afya za watu...muda utaongea na siku zote ukweli una tabia ya kutokupuuzwa.
 
]
Hapa tusiongee habari eti wewe ni mpinzani.Ni suala la kuchekecha mawazo kuona tunatokaje na janga hili lililoanza upya.
Mm binafsi kwa hali halisi na uzoefu tulio nao km Watanzania, lockdown haifai kwa hali zetu za kiuchumi,na staili yetu ya maisha tutakufa njaa.Fikiria mtu yuko DAR kapanga chumba kimoja unamwambia asitoke.
Pili,kumfungia mtu ndani maana yake unaifanya kinga yake ya mwili kushuka na hivyo kuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa na kufa kirahisi.Na hili ndilo wanataka walioitengeneza hii korona.
USHAURI:
Haihitaji kulumbana au kusubiri kuambiwa na mwanasiasa kuwa korona ipo,ni wewe na wale unaowapenda kuchukua tahadhari muda wote,kunawa na maji tiririka na sabuni,kuvaa barakoa,kuepuka misongamano isyo lazima nk Huhitaji kuambiwa.
Pili, Ni kuendelea kupiga nyungu, kwelikweli,kutumia mchanganyiko wa limao,tangawiz,kitunguu nk hivi vitu ukatae ukubali sisi km Watanzania vilituvusha dhidi ya korona.Vita haichagui silaha.
Tatu,Ondoa hofu,sababu imeonekana hofu ni zaidi ya korona.hofu inaua.
 
Ufipa inaingiaje kwa maamuzi ya Uingereza? Kama huna cha maana cha kuandika ficha ujinga wako.
Naona mnashabikia ujinga wa kutokuelewa kinachohabarishwa.

Hatua hiyo ya UK itawahusu raia wote khasa wale walogundulika wanapitia Tanzania lakini wanatokea Afrika Kusini.

Mbona hata UK nao wanaelekea kuzuiwa kuingia nchi za Jumuiya ya Ulaya?
 
Virus havina mipaka kwamba utajifungia kwenye nchi yako ujitibu huku ukitarajia kwenda nje au kupokea wageni toka nje.

Kuna vyombo kama WHO vyenye mamlaka ya ku control yanapotokea magonjwa kama hayo dunia.
Sasa mpaka sasa WHO wamedhibiti kwa namna gani huu ugonjwa?

Mpaka sasa hakuna nchi ambayo iko immune na COVID -19.

Stay Safe.
 
Tumechoka kutishwa na taarifa zenu za vifo vya corona, hata kabla ya corona vifo vilikwepo vingi vya ghafla, vya kupumua kwa shida, ko vifo ni vilevile toka kuumbwa kwa dunia. Hivyo mtuambia dunia inataka report ya vifo vinavuotokea kwa siku msihusishe na corona mnayoisingizia kwa wa Africa
 
Unasema je kama tuliokosea ni sisi? Ama kweli "nyani haoni kundule."

Eti tuendelee kujifukiza tusife hadi dawa rasmi ipatikane. Kwa nini kujifukiza kusiwe ndiyo dawa rasmi basi?

Eti tuendelee kutengeneza pesa!

Hii inaitwa, "tamaa mbele, mauti nyuma."

Mawazo duni kabisa.
kwani kuna dawa ya corona ambayo wanayo UK na wengine peke yao,kasoro tz!!!!!

mnaacha wapi akili!!
 
Richard ni vigumu kulinganisha madhara yako na ya jirani hujui mwenzako kajiandaa vipi kuisaidia familia yake, kusema Tanzania itaathirika kama nchi nyingine sio sahihi sana.

Kwenye sakata la covid19 nchi nyingi hasa za ulaya zimejiandaa kusaidia makampuni yatakayoathirika kwa kutoa mikopo nafuu, kuna nchi zenye lockdown zinasambaza hadi vyakula majumbani, chanjo ya covid19 ni bure kwa wananchi wake Tanzania hakuna mipango kama hiyo.

UK kwa mfano kuna Coronavirus Bailout Scheme inayosaidia ku stimulate uchumi wakati huu wa korona na zaidi ya £100bn zimetengwa, Tanzania tumetenga ngapi.

Kwahiyo hata kama wote tutaadhirika kiuchumi lkn inategemea na nchi imejiandaaje kukabiriana na mdororo wa uchumi.
 
Lakini hii sirikali yetu inachekesha sana, ni kweli maambukizi ya korona sio makubwa nchini...kuna ubaya gani wa kutoa data za hao wagonjwa?!.

Nchi yetu sio kisiwa ina muingiliano na mataifa mengine yaliyoathirika sana na wala ugonjwa huu sio wa aibu haujaanzia kwetu...kuna tatizo gani kusema hali yetu nchini kuhusu korona ikoje.

Yaani li sirikali lipo kimya japo hata kuendelea kuhamasisha raia wake kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa ambao dhahiri bado ni tishio duniani
data zinaondoa corona!!!
 
Si lazima kuwa na total lockdown lakini ni muhimu kuzuia mikusanyimo ya watu, kama inabidi wakusanyike wawe na barakoa pia kunawa mikono kila mara.
hilo ni jambo la mtu au ofisi na maamuzi yake.

ofisi nyingi kama bank na taasisi kuna sanityzer bado.
 
kwani kuna dawa ya corona ambayo wanayo UK na wengine peke yao,kasoro tz!!!!!

mnaacha wapi akili!!
Kuna chanjo inasambazwa kwenye nchi mbalimbali duniani Tanzania bado hatujaruhusu chanjo hiyo kuingia.
 
Imebaki tu kwa jiwe kuugua na kufa ndio utakuwa mwisho wa kudharau ugonjwa huu.
utakufa wewe,uende unalia kaburini kwa kumuacha anadunda.

hapo ulipo hata barakoa huvai,wala mikono hunawi tena,unamuwaza jiwe afe badala yako!!!!
 
Ni muhimu kuwa na takwimu kuthibitisha haya. Idadi ya maambukizi na idadi ya vifo kwa siku, wiki na mwezi.
wewe unajua wangapi wanakufa kwa HIV kwa siku!!!

lakini jukumu la kutembea kwa usalama hujawahi kumuachia mtu mwingine.
 
Basi serikali itoe data kwa kusema watanzania wote tuna corona hivyo hakuna maambukizi mapya
 
Sasa mpaka sasa WHO wamedhibiti kwa namna gani huu ugonjwa?

Mpaka sasa hakuna nchi ambayo iko immune na COVID -19.

Stay Safe.
WHO hawalali wanahangaika usiku na mchana kupata dawa hawajakaa wakitegemea maombi, sisi (Tz) wala hatujishughulishi hata kujaribu chanjo zilizopo tunasubiri rehema za Mungu.
 
KWA hili SERIKALI imekwama Sana, KWA Hili hatufiki mbali, tukitaka kujifanya tunaweza kila kitu na hatupangiwi hata kwenye afya za watu ,the gov is too long
corona imetangazwa rasmi 2020 mwezi wa kwanza.

miezi 3 baadae jiwe akatoa matamko yake,mliyoanza kuhubiri kwamba ni kujimaliza kwetu,miezi 9 leo,mnatamani mawazo yenu yatimie.

hao UK wana uzito kuliko dunia nzima iliyojifungia wakati wa lockdown???sisi hatutoi data congo nao hawatoi data!!!
 
Back
Top Bottom