#COVID19 Kudhibiti maambukizi ya COVID-19: Wasafiri kutoka Tanzania wapigwa marufuku kuingia Uingereza

#COVID19 Kudhibiti maambukizi ya COVID-19: Wasafiri kutoka Tanzania wapigwa marufuku kuingia Uingereza

Japo sijafungua link...Ila sisi tunawapokea wazungu kwa vigezo kuwa wao ni watalii na wanachangia pato la Taifa.

Sio sisi hata Dubai pia wanapokea watalii kwa kua wanategemea Utalii kuendesha Nchi Yao kwa asilimia kubwa,lakini upokeaji wao ni tofauti kidogo na wa kwetu ,mataifa kanjanja kama nchi yetu ukifika Dubai lazima upimwe tena COVID unaonesha majibu ya nchini kwako na pia wanakupima tena na foleni hakuna kuna boots kama 50 with doctors wanachukua sample inside the airport before haujatoka arrival gate wala kwenye mizigo haujatoka kwenda kuchukua majibu ni after 24 hrs unaacha mobile number yako wanakutumia sms kama ukikutwa na covid Emirates in cover insurance cost za wewe kutibiwa, na Pia kwenye passport wanakubandikia steaker ambayo ni barcode ukiscan kwa Simu after 24 hrs itakupa majibu yako kama haukupata sms ya majibu

hapa Tanzania hawaulizi Cheti cha COVID ukitua sana sana unajazishwa form kuulizwa umetoka nchi gani na ulikaa seat no ngapi , sasa hiyo inasaidia? Na ukidanganya nobody cares muhimu uludishe form yao na hawana hata kalamu za kujaza hizo forms , pen ni moja mnashare passengers 100+ Wameshindwa kununua pen Ambazo zipo well sanitized and packed or hizo form zao wangekua wanawapa shirika na ndege usika watu wajaze wakiwa angani kuliko kulundikana pale airport

kwa kifupi mama Gwajima Kafeli kwenye hili, Umi Mwalimu aliweza nina mshauli mama Gwajima atoke kidogo aende hata hapo Dubai aone on how they handle this situation , if we surely needs the tourist
 
H
(Reuters) - Britain is banning all arrivals from Tanzania and Democratic Republic of Congo from Friday to stop the spread of the South Africa COVID-19 variant, transport secretary Grant Shapps said in a tweet on Thursday.

"All passengers from these countries except British & Irish Nationals and third country nationals with residents rights will be denied entry," Shapps wrote in his tweet.

==========

Wasafiri kutoka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo watazuiwa kuingia Uingereza kwenye harakati za kujaribu kuzuia kirusi kipya cha Covid-19 kutoka Afrika ya Kusini.

Lakini marufuku hiyo itakayoanza Ijumaa saa 10 usiku haitawahusu raia wa Uingereza na Irish na wote wenye haki za makazi nchini Uingereza wanaorudi nchini humo, alisema katibu mkuu wa usafiri, Grant Shapps.

Hii imekuja baada ya mshauri mkuu wa kisayansi nchini Uingereza, Sir Patrick Vallance kuonya chanjo ambayo kwa sasa inatolewa inaweza kuwa haina nguvu sana dhini ya kirusi kutoka Afrika ya Kusini.

Kirusi tofauti cha Covid kinachojulikana kama 501Y.V2 kina uwezekano wa kusambaa haraka zaidi kwa asilimia 50 zaidi ya mwanzo.

Soma > UK bans passengers from Tanzania, Democratic Republic of Congo to control spread of COVID variant
Hii siyo njia sahihi ya kuzuia kusambaa kwa Covid. Wangesesema kuwa kila mgeni apime ndiyo aingie Uingeleza.this is the only affordable way ya kuzuia maambukizi bila kuathili uchumi wa nchi.

Lock down haisaidii kiivyo.makampuni yanayotengeneza vifaa vya kupima Covid wafanye iwe gharama nafuu.

Vivyo hivyo na sisi watanzania tusiwe dampo la kupokea wageni ambao Hawana cheti kwamba wamepima Covid.please
 
Kama Wana Nia ya kututawala kupitia magonjwa kwani ugonjwa Ni korona tu? Ni ugonjwa upi ambao sisi tuna uwezo wa kuushughulikia bila wao kwa maana ya Kinga, dawa, tafiti nk? Taja hata mmoja tu ambao hatuwategemei wao.
Corona inakuja na masharti mengi.. Ambao usafirishaji wa watu na mizigo unawekewa masharti basi utaona biashara kati ya mataifa itapungua sana ..Ukishafanya hivyo unaweka masharti ambayo , asiyoyafata anakuwa chini yako..Sasa sisi kama nchi ndio maana, JPM keshawagundua na tutashirikiana na nchi za kiafrika , jirani na ukanda wetu na tukafanya biashara kati yetu.. Kwa nje tutafanya biashara na ambao wana muelekeo kama wetu wa kutotaka kuja kututawala kupitia masharti ya corona... Hayo unayoiita magonjwa mengi si magonjwa , kama ilivyo Corona ,bali ni agenda za mashirika makubwa kwa kupitia WHO, kufanya biashara na washirika wao chini ya nchi na serikali zisizo na uzalendo kwa wananchi wao.. Kwa Tanzania wamenoa , tunaye JPM... Mungu aendelee kumbariki akiwashughulika na hila za mabeberu...
 
Kucheckiwa hapa ??

Hatuwezi kuaminika tena kwenye suala hilo maana ilishaonekana hatuko serious.
Kuna hospital zao ambazo mataifa ya nje yanaziamini, na jambo hilo walilianzisha siku nyingi wakati wa mambo ya aids
 
Unasema je kama tuliokosea ni sisi? Ama kweli "nyani haoni kundule."

Eti tuendelee kujifukiza tusife hadi dawa rasmi ipatikane. Kwa nini kujifukiza kusiwe ndiyo dawa rasmi basi?

Eti tuendelee kutengeneza pesa!

Hii inaitwa, "tamaa mbele, mauti nyuma."

Mawazo duni kabisa.
Kwani umekufa au bado?
kama unaogopa kufa ondoka tz kwanza mpaka siku wakitangaza hao unaowaaamini kuwa hakuna corona ndo urudi.
Unapiga kerere kwenye keyboard huku hujavaa barakoa na wala hunawi mikono na kukaa distance hata kujifungia ndani hutaki ila unataka waseme kuna corona ndo ufurahi.
Jinga kabisa, ungekua na maana kama unge vaa hata barakoa tu.
 
Tatizo Wests are arrogants wanadhani wanachokiwaza wao ndiyo sahihi kwetu bila kujali uhalisi wetu!! They are "superficial"!

Corona siyo mpira wa miguu kiasi kwamba sheria kumi na saba zinazotumika Ligi kuu Uingereza ndiyo hizo hizo zitumike Ligi kuu Tanzania bara m Ligi ya huko Zanzibar!

Corona inashughulikiwa kwa stahili ambayo muhusika amejipanga nayo kulingana na wakati, mahali, na nyenzo alizonazo! Corona haikabiliwi kwa "copy na paste" kila kitu! Tuchanganye na za kwetu jamani!

Tuache ulimbukeni wa "wests are best"! I can assure you, sometimes mind you not always "wests are worst "!
 
Lakini hii sirikali yetu inachekesha sana, ni kweli maambukizi ya korona sio makubwa nchini. Kuna ubaya gani wa kutoa data za hao wagonjwa?

Nchi yetu sio kisiwa ina muingiliano na mataifa mengine yaliyoathirika sana na wala ugonjwa huu sio wa aibu haujaanzia kwetu...kuna tatizo gani kusema hali yetu nchini kuhusu korona ikoje.

Yaani li sirikali lipo kimya japo hata kuendelea kuhamasisha raia wake kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa ambao dhahiri bado ni tishio duniani.
Wewe mkuu umejuaje kuwa Tz maambukizi ya corona sio makubwa hali ya kuwa hskuna takwimu? huko unakosema kumeathirika sana na corona tumejua kupitia takwimu sasa bongo hakuna takwimu tunawezaje kusema maambukizi sio makubwa?
 
Si lazima kuwa na total lockdown lakini ni muhimu kuzuia mikusanyimo ya watu, kama inabidi wakusanyike wawe na barakoa pia kunawa mikono kila mara.
Kama mikusanyiko gani ambayo izuiliwe?
 
Wacha tuendelee kuleta ujinga tuone mwisha wake ni upi, hii Covid itaipeleka hii nchi Eda Aka nusu-mlingoti..
 
Imebaki tu kwa jiwe kuugua na kufa ndio utakuwa mwisho wa kudharau ugonjwa huu.
Ushawahi kujiuliza kwanini Magufuli anaudharau huu ugonjwa? ikiwa rai wa kawaida anaona corona ipo Tz na watu wanakufa sasa iweje mtu ambaye ana taarifa za kujua nini kinaendelea lakini ila bado anadharau corona? Ni kwamba haogopi kufa au ni kipi anachokijua?
 
Swali la kujiuliza ni je wenye total lockdown with "barakoa" every second mbona bado hawajamaliza tatizo tunakaribia mwaka sasa? Kuna nchi zimeua watu wao kwa vipigo vikali na kuwafungia ndani na njaa, wamechukua misaada na mikopo ya covid lakini ndiyo kwanza maambukizi yako juu.

Ninadhani kila mmoja apambane kivyake. Matokeo ndiyo yatasema. Alianza kusema TAL akiwa kwa wakubwa wake na akaja na barakoa mia nane. Alipofika hakuvaa hadi kura zilipomkataa akaondoka na barakoa kwenda kuvalia alikonunulia sijui kupewa.
Mimi nashangaa kuna watu humu wakati wa kampeni walikuwa wanashabikia nyomi za watu kwenye hiyo mikutano ya kampeni,ila baada ya uchaguzi kuisha ndio wanakumbuka kuna corona.
 
Duh🙆🙆J

Hii inatia shaka sana, sasa kama Waingereza wanasema variant mpya ya COVID-19 imeikumba Afrika Kusini,je, Tanzania imeingizwaje kwenye mkumbo? Waingereza wanajuaje kwamba kasi ya maambukizi ya aina hii mpya ya virusi ni mara mbili ya mwanzo na chanjo haziko effective dhidi ya kirusi tajwa hapo juu, au jamaa ndio wanatujia na plan "B" nini?

Hapa viongozi wetu wawe makini wasikubali Watanzania kuchanjwa chanjo za Oxford zinazo zalishwa huko Uingereza pamoja na washirika wake.

Binafsi bado najiuliza maswali mengi - hivi imekuwaje mataifa ya Kiafrika ambayo yameruhusu majaribio ya chanjo za Oxford and partners ndio zinakumbwa na COVID-19 variant mpya ambayo inaelekea ni kali zaidi kuliko ya mwanzo - kama nakumbuka vizuri Mataifa ya Kiafrika yaliyo kubali majaribio ya chanjo za Oxford na mshirika wake, mataifa hayo ni: Kenya, Afrika kusini nadhani pamoja na Nigeria kama sikosei - mwaka jana Bill Gates alitembelea Afrika kusini kakutana na Raisi Ramaphosa na Ramaphosa alikubaliana na William Gates wamba Taifa lake liko tayari kufanyiwa majaribio ya chanjo au kuzitumia kabisa emass.

Juzi hapa niliangalia BBC documentary iliyo kuwa inazungumzia kuhusu kugundulika kwa COVID-19 variant/mpya huko TAVETA yaani mpakani mwa Kenya na Tanzania - now, the question is: why TAVETA and not Nairobi or Mombasa - Kenya kama nilivyo sema tangu mwanzo wanashirikiana kwa karibu sana na kampuni ya Oxford and partners za huko Uingereza katika kuwafanyia baadhi ya raia wa Kenya (blacks) majaribio ya chanjo za Oxford ambazo huko Uingereza walifanya majaribio ya chanjo hizo kwa Sokwe mtu sio binadamu.

Bottom line is: Ninapo toa tahadhari kuhusu chanjo hizi za kutoka Mataifa fulani baadhi ya watu wana anza kunibeza beza eti naendekeza masuala ya conspiracy na kuyasema vibaya mataifa ya magharibi - wanao sema hivyo siwa kweli hata kidogo, kama bado mnafikiri comments za mkewe Bill Gates za kusema kwamba Waafrika ndio watakufa zaidi compared to other races kama bado mnafikiri mama huyo aliyasema hayo kwa bahati mbaya - you better think twice au kama mnafikiri wehu hawa hawawezi kuwapa instruction wana sayansi wa Big Pharma companies zinazo pewa ruzuku kubwa ya fedha kutoka kwenye mfuko wa Bill and Melisa foundation, wana sayansi watafanya lolote Bill Gates atakalo ambia/waomba ,influence ya Bill Gates ni omni potent and omni present kila sekta imeingia mpaka W.H.O si hilo tu, nawakumbusheni tena kwamba karibu makampuni yote ya ketengeneza dawa na Chanjo, maabara za kitafiti - yaani taasisi zote za magharibi zilizo tajwa hapo juu zinapewa hela nyingi kutoka kwenye foundation ya Melisa&Bill Gates i.e hakuna ambapo hakuna mkono wa Bill Gates, sasa hii inatoa taswira gani? Ni wazi kwamba Bill Gates na like mind wenzake wanaweza kuwapa instruction wana sayansi wa fani za kibiolojia ili waweze ku-tinker around na COVID-19 gnome kuzalisha virusi vipya ambavyo ni hatari zaidi kuliko vya mwanzo, wakiwa na lengo la kutekeleza malengo yao ya muda mrefu ya ku-depopulate Dunia ya tatu kwa kiwango kikubwa - kama kuna baadhi ya Watanzania who still don't believe ushauri/maoni yangu - fine, lakini-wakumbuke kwamba ni suala la muda kadri siku zinavyo songa mbele ndio watakuja kutambua undani/ubaya wa Bill Gates na genge lake, hawa si watu wema hata kidogo.
 
Hii inatia shaka sana, sasa kama Waingereza wanasema variant mpya ya COVID-19 imeikumba Afrika Kusini,je, Tanzania imeingizwaje kwenye mkumbo? Waingereza wanajuaje kwamba kasi ya maambukizi ya aina hii mpya ya virusi ni mara mbili ya mwanzo na chanjo haziko effective dhidi ya kirusi tajwa hapo juu.

Hapa viongozi wetu wawe makini wasikubali Watanzania kuchanjwa chanjo za Oxford zinazo zalishwa huko Uingereza, binafsi najiuliza maswali mengi - imekuwaje mataifa ya Kiafrika ambayo yameruhusu majaribio ya chanjo za Oxford ndio zinakumbwa na COVID-19 variant ambayo inaelekea ni kali zaidi kuliko ya mwanzo - kama nakumbuka vizuri Mataifa ya Kiafrika yaliyo kubali majaribio ya chanjo za Oxford na mshirika wake, mataifa husika ni Kenya, Afrika kusini nadhani pamoja na Nigeria kama sikosei - mwaka jana Bill Gates alitembelea Afrika kusini kakutana na Raisi Ramaphosa na yeye akakubali kwamba Taifa lake liko tayari kufanyiwa majaribio ya chanjo au kuzitumia kabisa emass, juzi hapa BBC documentary ilizungumzia kuhusu kuhundulika kwa COVID-19 variant/mpya huko TAVETA mpakani mwa Kenya na Tanzania - the question is why TAVETA and not Nairobi or Mombasa - Kenya kama nilivyo sema tangu mwanzo wameshirikiana kwa karibu na kampuni ya Oxford and partners ya huko Uingereza katika kuwafanyia baadhi raia wa Kenya (blacks) majaribio ya chanjo za Oxford ambazo huko Uingereza walifanya majaribio ya chanjo kwa Sokwe mtu sio binadamu.

Ninapo toa tahadhari kuhusu chanjo hizi kutoka Mataifa fulani baadhi ya watu wana anza kunibeza beza eti naendekeza masuala ya conspiracy na kuzisema vibaya mataifa ya magharibi - hiyo si kweli hata kidogo, kama bado mnafikiri mkewe Bill Gates kusema kwamba Waafrika ndio watakufa zaidi compared to other races na alisema hivyo kwa bahati mbaya - you better think twice, na kama mnafikiri wehu hawa hawawezi kuwapa instruction wana sayansi to tinker around na COVID-19 gnome kuzalisha virusi vipya ambavyo ni hatari zaidi kuliko vya mwanzo wakiwa na lengo la kutekeleza malengo yao ya muda ya depopulate dunia ya tatu kwa kiwango kikubwa - kama you still don't believe ushauri wangu - Up2U.
Shukrani nitakujibu kwa kirefu kesho
 
Sasa mnamlaumu Jiwe kwa sababu ya South Africa covid variant? Ingekuwa Tanzania covid variant ningeelewa mantiki ya hiyo ban. Vinginevyo ni upuuzi na kuchanganyikiwa kwa hao wazungu wa UK.

Ok tumepigwa ban kuingia UK....kwa nchi na mtu anayejielewa hiyo ban should not be our problem, it is UK problem. UK ni paradiso?
Hujui chochote kuhusiana na mutation ya virus. Variant kusemwa ni ya South Africa sio lazima ilianzia huko! Angalau huko wanapima! Sisi huku vipi? Mutations hazina mipaka!!! UK sio wajinga, tuendelea kufurahia yaani. Ni utamu tu yaani.
 
Hii inatia shaka sana, sasa kama Waingereza wanasema variant mpya ya COVID-19 imeikumba Afrika Kusini,je, Tanzania imeingizwaje kwenye mkumbo? Waingereza wanajuaje kwamba kasi ya maambukizi ya aina hii mpya ya virusi ni mara mbili ya mwanzo na chanjo haziko effective dhidi ya kirusi tajwa hapo juu.

Hapa viongozi wetu wawe makini wasikubali Watanzania kuchanjwa chanjo za Oxford zinazo zalishwa huko Uingereza, binafsi najiuliza maswali mengi - imekuwaje mataifa ya Kiafrika ambayo yameruhusu majaribio ya chanjo za Oxford ndio zinakumbwa na COVID-19 variant ambayo inaelekea ni kali zaidi kuliko ya mwanzo - kama nakumbuka vizuri Mataifa ya Kiafrika yaliyo kubali majaribio ya chanjo za Oxford na mshirika wake, mataifa husika ni Kenya, Afrika kusini nadhani pamoja na Nigeria kama sikosei - mwaka jana Bill Gates alitembelea Afrika kusini kakutana na Raisi Ramaphosa na yeye akakubali kwamba Taifa lake liko tayari kufanyiwa majaribio ya chanjo au kuzitumia kabisa emass, juzi hapa BBC documentary ilizungumzia kuhusu kuhundulika kwa COVID-19 variant/mpya huko TAVETA mpakani mwa Kenya na Tanzania - the question is why TAVETA and not Nairobi or Mombasa - Kenya kama nilivyo sema tangu mwanzo wameshirikiana kwa karibu na kampuni ya Oxford and partners ya huko Uingereza katika kuwafanyia baadhi raia wa Kenya (blacks) majaribio ya chanjo za Oxford ambazo huko Uingereza walifanya majaribio ya chanjo kwa Sokwe mtu sio binadamu.

Ninapo toa tahadhari kuhusu chanjo hizi kutoka Mataifa fulani baadhi ya watu wana anza kunibeza beza eti naendekeza masuala ya conspiracy na kuzisema vibaya mataifa ya magharibi - hiyo si kweli hata kidogo, kama bado mnafikiri mkewe Bill Gates kusema kwamba Waafrika ndio watakufa zaidi compared to other races na alisema hivyo kwa bahati mbaya - you better think twice, na kama mnafikiri wehu hawa hawawezi kuwapa instruction wana sayansi to tinker around na COVID-19 gnome kuzalisha virusi vipya ambavyo ni hatari zaidi kuliko vya mwanzo wakiwa na lengo la kutekeleza malengo yao ya muda ya depopulate dunia ya tatu kwa kiwango kikubwa - kama you still don't believe ushauri wangu - Up2U.
Peleka ushamba wako huko! Kwenye immunology hujui chochote! Post ndefu halafu ni uozo tu.
 
Wenye mamlaka ya kutamka juu ya covid19 Tz wanasemaje?
Tanzania does not depend to much from UK, so it was prudent for the UK to add Tanzania and Congo in the list to justify their initial ban to other south of Sahara African countries, as the variant originates from South Africa.
 
Hadi sasa nimepokea nina marafiki 9 toka nchi za ulaya watatu wamefikia mombasa na 6 wako Tanzania.

Wanasema huko Europe kila mtu anapambana kujinasua kwenye huo mtego wa kufa kwa stress ya kufungiwa ndani kwa kutafuta nchi salama duniani akapumzike na wanasema all over the the world Tanzania ni sehemu pekee salama kwa sasa.

Adhabu ya kutofuata taratibu na masharti ya COVID ni faini ambayo minimum ni USD1000 na maximum ni USD5000

Nilicho observe kwa hawa wageni pamoja na mateso yote wanayopata huko kwao sijawasikia kutamka mabaya kuhusu serikali zao wala kuwatukana marais wao. Sijui wenzetu wamefundwaje kuwa wazalendo kiasi hicho ila Kuna cha kujifunza hapa!

Mimi naendelea kujiongeza rais wangu John Pombe Magufuli kwa ushindi mkubwa kwenye mambo mengi ya maendeleo ila najivunia kusema kwa alivyoweza kufanya maamuzi juu ya corona John Pombe Joseph Magufuli atabaki kuwa rais Jasiri zaidi duniani, huyu atabaki kwenye historia kama rais wa karne

Mungu ibariki Tanzania
 
Corona inakuja na masharti mengi.. Ambao usafirishaji wa watu na mizigo unawekewa masharti basi utaona biashara kati ya mataifa itapungua sana ..Ukishafanya hivyo unaweka masharti ambayo , asiyoyafata anakuwa chini yako..Sasa sisi kama nchi ndio maana, JPM keshawagundua na tutashirikiana na nchi za kiafrika , jirani na ukanda wetu na tukafanya biashara kati yetu.. Kwa nje tutafanya biashara na ambao wana muelekeo kama wetu wa kutotaka kuja kututawala kupitia masharti ya corona... Hayo unayoiita magonjwa mengi si magonjwa , kama ilivyo Corona ,bali ni agenda za mashirika makubwa kwa kupitia WHO, kufanya biashara na washirika wao chini ya nchi na serikali zisizo na uzalendo kwa wananchi wao.. Kwa Tanzania wamenoa , tunaye JPM... Mungu aendelee kumbariki akiwashughulika na hila za mabeberu...
Maneno meeengi huhajibu swali.
 
Back
Top Bottom