Kudorora kwa muhimili wa familia na wimbi la kukataa ndoa ni ishara ya ushindi kwa shetani

Kudorora kwa muhimili wa familia na wimbi la kukataa ndoa ni ishara ya ushindi kwa shetani

Labda nikukumbushe jambo


“Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako”. ( MK 10:19)
bado jibu halijitoshelezi.
swali langu linasema kuto kuwa na ndoa ni kuzini?
 
bado jibu halijitoshelezi.
swali langu linasema kuto kuwa na ndoa ni kuzini?
Majibu ya Biblia hayatoshelezi?

Ndyomaana nimesema ni lazima uwe unajitambua ili uweze kutofautisha hivyo vitu viwili.
 
Habari za wakati huu wadau na wana familia wote.....

Moja ya nguzo muhimu katika maisha ya mwanadamu ni familia, hata Mungu alipo muumba Adam aliona amekuwa mpweke na akamletea mwenza, pia mwisho akawaamuru waende wakaijaze dunia.
Huyo Mungu mbona hakujiumbia Mke wake aishi nae pamoja?

Kama kuishi mume na mke ni jambo jema, Huyo Mungu kwa nini hana Mke?

Au huyo Mungu wenu anaogopa kuishi na mwanamke?
Hivyo basi, njama au lengo kuu la shetani ni kusambaratisha na kuvuruga nguzo ya familia, na njia mojawapo ni kuhakikisha hakuna ndoa wala malezi ya pamoja.

Ifuatayo ni mifano au mambo ambayo yanaashiria ushindi huu ambao shetani anaupata.....

Mfano 1. Kumeibuka wimbi kubwa la vijana kudai na kuhamasisha wengine kupinga na kukataa swala la ndoa, hii ni ishara ya juhudi na ushindi wa shetani katika kuharibu Muhimili wa familia.

Mfano 2. Malezi ya pamoja yamepungua, single mothers wameongezeka na watoto wengi wanapata malezi ya upande mmoja.

Mfano 3. Watoto kutumia muda mwingi mashuleni, asubuhi mpaka jioni mtoto anashinda nje ya nyumbani, malezi ya wazazi atayapata sangapi au mpaka weekend?

Mfano 4. Wimbi la mapenzi ya jinsia moja, kama watu wakishiriki aina hii ya mahusiano basi tayari hapatakuwa na familia tena kwani hakuna uwezekano wa kuzaa watoto.

Mfano 5. Wanawake kutoka nyumbani, Muhimili wa familia unategemea sana uwepo wa mwanamke, kama anatoka kutwa nzima na kuwaacha watoto, hapo tayari familia inakosa uimara wa malezi ya upande wa mama.

Mfano 6. Ongezeko la talaka au ndoa kuvunjika, tunashuhudia namba kubwa ya ndoa ambazo zinavunjika baada ya muda mfupi tu kufungwa, hii ni ishara kwamba Muhimili wa familia upo hatarini kupotea au kusambaratika kabisa.

Haya yote yamo katika kitabu ambacho kiliandikwa mnamo mwaka 1990 kabla mifano tajwa hapo juu kuenea kwa kasi kama ilivyo sasa.

View attachment 3063649

ANGALIZO : Kwa wale wote ambao wanapinga na kukataa kuwa na familia, mnapaswa kujua kwamba mnamsaidia shetani kutimiza lengo lake.
 
Pia shetani hana kazi na watu ambao tayari amewapoteza, ana deal na hao viongozi wa dini kwani wao ndyo wabishi na wana uelewa na imani kubwa, hao ndyo anawawinda kwa nguvu zote
Ndiyo hiyo sasa, dini zimekuwa sehemu ya kutafuta watu wa kuja kujaa kaburini unapozikwa, kwingine huko dini inabaki ya mtu mwenyewe!.
 
Lakini nashangaa kuona wengine wanasema dini ni mpango wa shetani
Kwanza Mungu hakuleta dini, ndipo hapo unaweza kutaka kujua nani kaleta dini na kwa makusudi gani.

Mfano, Ayubu 4:6 (inasema),
Je! Dini yako siyo mataraja yako, Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako?
 
Kwanza Mungu hakuleta dini, ndipo hapo unaweza kutaka kujua nani kaleta dini na kwa makusudi gani.

Mfano, Ayubu 4:6 (inasema),
Je! Dini yako siyo mataraja yako, Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako?
Dini ni mfumo wa Kumtukuza na kumuabudu Mungu, Huwezi kutenganisha Dini na Mungu
 
Back
Top Bottom