Kudorora kwa muhimili wa familia na wimbi la kukataa ndoa ni ishara ya ushindi kwa shetani

Kudorora kwa muhimili wa familia na wimbi la kukataa ndoa ni ishara ya ushindi kwa shetani

Ndoa ni mpango wa Mungu kwa mwanadamu. aliianzishaYeye mwenyewe pale bustani ya Edeni.
mume ni mfano wa Kristo
mke ni mfano wa kanisa

kanisa ni bi arusi, na Kristo ni Bwana arusi. Biblia imeayaongea haya mambo kwa namna ya ajabu sana.

Waefeso 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³¹ Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
³² Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa.

“Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi."
— 2 Wakorintho 11:2 (Biblia Takatifu)

hapo kinachosemwa hapo ni ndoa kati ya Kristo na kanisa
 
“Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi."
— 2 Wakorintho 11:2 (Biblia Takatifu)

hapo kinachosemwa hapo ni ndoa kati ya Kristo na kanisa
Kama ndoa ni kati ya kanisa na kristo, kuna andiko linasema kristo aliwahi kwenda au kuingia kanisani?
 
kuingia ka
Kama ndoa ni kati ya kanisa na kristo, kuna andiko linasema kristo aliwahi kwenda au kuingia kanisani?

kuingia kanisani kivipi. kanisa sio jengo. kanisa ni watu waliookolewa na Kristo. MATENDO 2:47.

“wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.

— Matendo ya Mitume 2:47 (Biblia Takatifu)
 
Taasisi za dini na serikali inabidi kuingilia kati kunusuru hili jambo.

Pale kutuo jumuishi temeke wanavunja ndoa Mia moja kila mwezi.

Hivyo ni wastani wa ndoa elfu moja na miambili kwa mwaka.

Familia za kitanzania kwa sasa zina wastani wa watoto wawili hivyo ni zaidi ya watu 4800 wanaathirika na kuvunjika kwa ndoa kwa mkoa wa Dar pekee kwa mwaka.
 
Sawa mkuu, hapo nimeelewa, lakini tukirudi kwenye mada, ndoa ni jambo muhimu na lazima, kukataa ni kupingana na maamrisho ya MUNGU
 
Taasisi za dini na serikali inabidi kuingilia kati kunusuru hili jambo.

Pale kutuo jumuishi temeke wanavunja ndoa Mia moja kila mwezi.

Hivyo ni wastani wa ndoa elfu moja na miambili kwa mwaka.

Familia za kitanzania kwa sasa zina wastani wa watoto wawili hivyo ni zaidi ya watu 4800 wanaathirika na kuvunjika kwa ndoa kwa mkoa wa Dar pekee kwa mwaka.
Sahihi mkuu, hali ya ndoa ni mbaya sana kwa sasa, watu wanaoana haipiti hata miezi wanaachana, hii ni ishara kwamba itafika wakati ndoa itakuwa ni jambo ambalo watu hawalizingatii na kutolipa umuhimu
 
Huo ni utani tu wa mitandaoni, wabongo bado ni watu wanaothamini sana ndoa. Ukitaka kuthibitisha hilo angalia kadi za michango ya harusi unazopokea
Upo sahihi ,mwezi wa tano niketoa mchanho zaidi ya 300k , hapo nimeigawa kwa 50k kwa kila harusi
 
Habari za wakati huu wadau na wana familia wote.....

Moja ya nguzo muhimu katika maisha ya mwanadamu ni familia, hata Mungu alipo muumba Adam aliona amekuwa mpweke na akamletea mwenza, pia mwisho akawaamuru waende wakaijaze dunia.

Hivyo basi, njama au lengo kuu la shetani ni kusambaratisha na kuvuruga nguzo ya familia, na njia mojawapo ni kuhakikisha hakuna ndoa wala malezi ya pamoja.

Ifuatayo ni mifano au mambo ambayo yanaashiria ushindi huu ambao shetani anaupata.....

Mfano 1. Kumeibuka wimbi kubwa la vijana kudai na kuhamasisha wengine kupinga na kukataa swala la ndoa, hii ni ishara ya juhudi na ushindi wa shetani katika kuharibu Muhimili wa familia.

Mfano 2. Malezi ya pamoja yamepungua, single mothers wameongezeka na watoto wengi wanapata malezi ya upande mmoja.

Mfano 3. Watoto kutumia muda mwingi mashuleni, asubuhi mpaka jioni mtoto anashinda nje ya nyumbani, malezi ya wazazi atayapata sangapi au mpaka weekend?

Mfano 4. Wimbi la mapenzi ya jinsia moja, kama watu wakishiriki aina hii ya mahusiano basi tayari hapatakuwa na familia tena kwani hakuna uwezekano wa kuzaa watoto.

Mfano 5. Wanawake kutoka nyumbani, Muhimili wa familia unategemea sana uwepo wa mwanamke, kama anatoka kutwa nzima na kuwaacha watoto, hapo tayari familia inakosa uimara wa malezi ya upande wa mama.

Mfano 6. Ongezeko la talaka au ndoa kuvunjika, tunashuhudia namba kubwa ya ndoa ambazo zinavunjika baada ya muda mfupi tu kufungwa, hii ni ishara kwamba Muhimili wa familia upo hatarini kupotea au kusambaratika kabisa.

Haya yote yamo katika kitabu ambacho kiliandikwa mnamo mwaka 1990 kabla mifano tajwa hapo juu kuenea kwa kasi kama ilivyo sasa.

View attachment 3063649

ANGALIZO : Kwa wale wote ambao wanapinga na kukataa kuwa na familia, mnapaswa kujua kwamba mnamsaidia shetani kutimiza lengo lake.
Kurudi ktk asili ya maumbile ni ushindi wa muumba uliokua umeporwa na shetani aitwae ndoa
 
Kama unajitambua utajua umuhimu wa ndoa
kila kitu kina umuhimu kwa nafasi yake, ile kwamba ndoa ina umuhimu haina maana kwamba kutokuoa/kuolewa ni kutokujitambua, hata biblia haija mlazimisha mtu kuwa kwenye ndoa imempa mtu uhuru wa kuchagua nini afanye
 
Biblia imempa mtu uhuru wa kuzini maisha yake yote?
 
hapana .
kwani kutokua kwenye ndoa ni kuzini?
Labda nikukumbushe jambo

“Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako”. ( MK 10:19)
 
Back
Top Bottom