Kuelekea Mei Mosi 2022. Yanayotarajiwa, yatakayojiri. Je, Rais Samia atatimiza alichoahidi mwaka 2021?

Mimi siko kwenye halmashauri yoyote na ofisi yetu haifungamani na halmashauri .
Naripoti kwa chief executive naye anaripoti kwa waziri
Basi hiyo ndio sababu. Lakini hata huko pia Ni suala la muda tu.

Maana Sheria ya ajira na mahusiano kazini in loophole hizo. Ikitokea zaidi ya nusu ya wafanyakazi wa eneo husika wamejiunga kwenye chama Cha wafanyakazi, basi wanaweza kuanza kuwakata wote ambao hampo chama chochote
 
Watumishi tujitahidi kuwa na plan B za kupambana na hali zetu! Lakini tukiendelea kutegemea kupandishwa madaraja na kuongezwa mishahara tutaendelea kulia.
 
Kwani huyu mama analipwa kiasi gani?

Wasilete kasumba eti mshahara wake ni siri hayo ni mambo ya kizamani yasiyo na msaada.

Mtu anayelipiwa chakula bure, malazi bure, matibabu bure , mavazi bure na bado anavuta mshahara msifikiri atakua na fikra kama zenu.
 
Subiri royo tua iishe tutajua mbivu na mbichi
 
Wafanyakazi watumie fursa hii kutoa maoni yao kwenye mabango ya kumuunga mkono Mh Rais sera yake ya uhuru wa kutoa maoni.
 
Kila mbuzi atakula kulingana na huruma ya mchungaji.
 
Yupo marekani kutafuta chochote kitu ili atimize ahadi yake aliyoitoa mwaka jana...wafanyakazi jiandaeni kwa neema.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mgeni rasmi atatumwa Dr Bilal,ataahidi kwaniaba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…