Uchaguzi 2020 Kuelekelea Uchaguzi mkuu 2020: Tupe tetesi na maoni yako, unapendekeza nani agombee wapi na nafasi gani?

Tarime sio ukonga chapombe ataleta maendeleo gani sasa alishindwa kuleta akiwa cdm kashindwa pia akiwa ccm.Jimbo la ukonga ndilo lenyewe mahandaki kuliko majimbo yote dar msimu Wa mvua hunapesa ujafika au kutoka kwako barabara hazipitiki
 
Hao wahamiaji haramu watakatwa na wenye ccm yao jengo la bunge atalionea kwenye tv
 
Kwahiyo wananchi wa Ukonga hawamhitaji tena au ni yeye hawahitaji tena wa Ukonga? Waitara ameichoka Ukonga mara hii? Mbona anawafanyia watu wa ukonga kama wahuni wanavyowafanyia machangu, kwamba akishatokwa na kilichomleta basi anasepa anatafuta mwingine!
 
ahaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfanyabiashara mwenye Asili ya Kihindi maarufu "Mwanza Huduma Ltd" amemwaga noti kwa Wajumbe wa CCM Katika kunyemelea Ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini. Kufuru hiyo imefanyika nyumbani kwa Mwenyekiti wa CCM aliyekuwa akiongoza kikao cha Wajumbe hao nyumbani kwake.

Katika Mkakati huo wa siri inadaiwa Katibu Mwenezi wa Wilaya ameachiwa fungu 'nono' ili kusambaza kwa wajumbe ambao wako Vijijini. Mtoa taarifa anasema baadhi ya Wajumbe wamelalamika kupewa Laki Moja na wengine kupewa Laki mbili na Mifuko ya saruji.

Baadhi ya Wajumbe ambao hawakuhudhuria vikao hivyo wameelekezwa kumuona Ndugu Nasoro Suleiman ambaye ni Wakala maarufu wa Mpesa ili kupata 'Mgao' wao. Walipoulizwa kwanini wanatoa rushwa bila kuogopa, wamedai kuwa TAKUKURU Bunda wamewekwa 'sawa'.

Uongozi wa CCM Wilaya ya Bunda utazamwe kwa jicho la Tatu kwani wanapenda Hela mpaka ya 'kutolea'
 
Tangu lini CCM ikashida bila kutoa hela? CCM inatumia UJINGA, UMASIKINI, NA UELEWA MDOGO wa watanzania kuchukua mamlaka, na hii ndio sababu kubwa ccm haiwezi taka watz wapate elimu bora ndio waweze kujua jinsi ya kuchagua viongozi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…