Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Hoja za kipuuzi unataka asifiwe ila kumtaja kwa mabaya hapana acha uzwazwa wewe yule alikuwa binadamu so mazuri na mabaya yote lazima yasemwe, UKIWA MCHOYO USIWE MROHO
 
Kwa mara ya kwanza nimenote mambo mawili kwako Robert Heriel la kwanza aidha wewe ni mpumbavu na la pili mabandiko Yako humu jf yamekufanya uvimbe kichwa na tembo kasifiwa Sasa mgema kapata kazi yake!
 
Yule mzee alikuwa Muuaji na halitapingika hilo,,, shetani kabisa Yule tutamlaani kila siku na kuanika mabaya yake hadi vizazi vijavyo vijue kweli tuliwahi kuwa na Shetani Ikulu
Shetani ana wafuasi wengi sana kuliko hata wachamungu, sasa ingekuwa kweli mnachukia maovu tungeona mkiwa mnakemea huyo shetani kama mnavyofanya kwa Magufuli.
 
Ingekuwa wewe ndiye uliyepigwa Risasi thealthini,Mtoto wako alipotezwa, Ndugu zako waliuawa(Baba au mama yako) ulibomolewa nyumba yako Morogoro Road bila kulipwa hata mia nazani ungekuwa unamlaani milele hata kama amekufa
Mpuuzi sana huyo jamaa halafu anajiita taikon wa fasihi na kina Shaban Robert tuwaiteje?
 
Niujinga uliotukuka mtu kujifanya anatangaza na kulialia eti marehemu amenifanyia ABC wakati huyo marehemu hawezi kujitetea.

Uwongo mwingi sana unasemwa kuhusu Magu kwamba alikuwa mbaya nk.
Uwongo ambao hao mawakala wa walamba asali hawawezi kuudhibitisha.

Wanao sema mazuri ya Magufuli angalau wana fact, kwamba mtu akikuambia Magufuli alikuwa mzalendo unaweza kumuelewa kutokana na mambo makubwa ambayo ameyafanya kwa muda mchache sana.

Mambo ambayo yanaonekana wazi na mpaka sasa Nchi inatekeleza mawazoyake kwa kuendekeza plan zake.

Kumlilia marehemu eti alikuumiza ni ujingatu, mtu amesha kufa sasa hatakama ukilialia ndio unataka iweje, akafukuliwe apelekwe mahakamani?.
 
Marehemu anakuwaje na ushawishi Mkuu au wewe anakushawishi nini
Hapa nilipo mie,watanzania wengi wanaoishi hapa uingereza wanamkubali sana jpm,huwa tuna club yetu ya kukutana kila jmos ya mwezi,huwez amin,wanammiss sn jpm,japo wanakili kuwa alifanya makosa kubinya upinzani,
 
Wayahudi wanaomlaani Hitler mpaka Leo unadhani niwajinga wewe ndio mwerevu! Mjinga kabisa wewe!
 
kwani hujui kwamba yule mzee ni Jamii hiyo hiyo ya shetani
Kwa imani yangu mie ni kwamba Mungu hakuumba kiumbe shetani, maovu ya kiumbe ndio hufanya kuitwa shetani, na sio lazima uwe kiongozi dikteta au uwe unauwa watu na kutesa ndio uwe shetani.
 
Hapa nilipo mie,watanzania wengi wanaoishi hapa uingereza wanamkubali sana jpm,huwa tuna club yetu ya kukutana kila jmos ya mwezi,huwez amin,wanammiss sn jpm,japo wanakili kuwa alifanya makosa kubinya upinzani,
Sasa usilinganishe watu walioko UK na Hawa wakina Ben Saanane ambao hata makaburi Yao hayajulikani yalipo! Kuna bandiko liko humu Ben Saanane alimezwa na chatu kisiwa Fulani Cha bahari ya Hindi kwa usiamizi wa vyombo unalijua Hilo?
 
Kila anayemsema katendwa namna moja au nyingine. Cha muhimu ni wanayosema kama yana ukweli, na mengi kama sio yote yanasomwa yana ukweli. Magufuli alikuwa mwendawazimu asiye na utu.
Sasa mbona kila siku tunasikia yaleyale tu ya Lissu mara Mo mara maiti kwenye viroba? Wasemaji ni wengi ila yanayosema ndio hayo hayo tu.
Wapo waliyoguswa na Magufuli katika mambo ambayo hawezi kuyasema ila unakuta hasira zake anaishia kueleza habari za kupigwa risasi Lissu tu.
 
Reactions: nao
Shetani ndio Uovu wenyewe,lakini binadamu hata awe muovu kiaje hakosi jema moja.

Tofautisha Shetani na binadamu.
Mashetani ni wafuasi wa Ibilisi ambaye ni malaika lakini hao wafuasi wake wapo binadamu na majini.
 
Wayahudi wanaomlaani Hitler mpaka Leo unadhani niwajinga wewe ndio mwerevu! Mjinga kabisa wewe!
Kwamba Hitler anazungumziwa na Wayahudi huko sawa au zaidi wanavyozungumzia changamoto zao walizonazo sasa?
 
Umemjibu Kwa usahihi huyo mpuuzi!
 
1). Dikteta Benito Mussolini alianza kutawala Italy tarehe 31/10/1922, karne nzima iliyopita, akapinduliwa tarehe 25/July/1943..
Hatimaye akanyongwa Kwa sababu ya uovu wake dhidi ya umma mwaka 1945.
2). Dikteta Joseph Stalin, alitawala Urusi Kwa mkono wa chuma kati ya 1924 na 1953.
3). Dikteta Vladimir Lenin alitawala kuanzia 1917 hadi 1924..
Nk..
Na kuna orodha ndeeefu ya madikteta wa Afrika ambao ni marehemu na wanaendelea kusemwa..

Wote hao wanasemwa na wataendelea kusemwa ingawa majority ya wahanga wa utawala wao mbovu hawapo hai kwa sasa..
Ndo wewe uje uzibe watu midomo kumsema dikteta wa juzi hapa?!!!

Moja ya manufaa ya kuwasema waovu wa zamani ni kukumbushana na kuelimishana ili kupunguza uwezekano wa kuibuka muovu mwingine upyaaa!

KAZI unayojaribu kujitwisha ya kupulizia pafyumu uovu na uonevu wa watawala dhidi ya umma ni ngumu na ya kuchosha sana. Nadhani huwezi kutoboa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…