Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Habari za uchaguzi Wakuu!
Nafikiri siku ya Leo imeenda kinyuma na lengo lilivyopangwa. Serikali iliiweka siku ya Leo kama siku ya mapumziko ili kutoa fursa kwa watu kupata muda wa kwenda kupiga Kura katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa.
Lengo lilikuwa zuri lakini likapoteza maana baada ya baadhi ya wagombea kuenguliwa. Kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea hasa wagombea wa upinzani kumefifisha umuhimu na maana maana halisi ya mchakato wa uchaguzi.
Hivi kama mgombea ni Mmoja eneo Fulani kuna mtu na akili zake ataenda kupiga Kura? Kuna mtu atasema ndio ataenda kupiga Kura ya Hapana kama hamtaki huyo mgombea.
Serikali iichukue hii kama changamoto na funzo kwa wakati ujao yaani uchaguzi Mkuu ujao kuwa masuala ya kuenguana enguana yaachwe. Ili kuupa umuhimu na maana uchaguzi Mkuu.
Vinginevyo hakuna maana yoyote ya watu kukaa nyumbani alafu hawaendi kupiga Kura.
Nilikuwa najaribu kuuliza baadhi ya watu katika vijiwe kadhaa kuhusu ushiriki wao katika kupiga Kura asilimia kubwa walinijibu kuwa sasa kama mgombea ni Mmoja kuna haja gani ya kujisumbua kupiga Kura?
Watu huenda kupiga Kura kumsapoti mtu wanayemkubali ili asishindwe na Yule wasiyemkubali. Sasa kama wanayemkubali yupo mwenyewe huo umuhimu wa kupoteza Muda kwenda kumchagua mtu aliyemwenyewe unatoka wapi?
Au mtu wanayemkubali kaenguliwa, wataenda kupiga Kura kwa mantiki ipi, hata wakimkataa aliyewekwa haitabadilisha kutokuwepo kwa mtu wao.
Serikali Ione Jambo hili kama sehemu ya kuifanyia maboresho.
Ili tusiwe taifa lililojudharau. Watu na wananchi waenchi hii wasijidharau ikawa nchi ya waliojidharau na kudharauliwa.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam