Kufanana na watu wengi hii imekaaje?

Ila yaweza kuwa kweli mkuu maana hata ndevu sina🙌😂😂😂
ingawa nina karibia 30 hv sasa.
 
Naweza kutana na mtu akawa ananiangalia sana. Atatafuta namna tupige story kidogo. Then ataniuliza unajua bana umefanana sana na mtu mmoja hv yaani kila kitu hadi kuongea.
Mama mwingine nilikuwa tu napita akaniita yaani anasema nikajua ww ni mwanangu maana mmefanana kila kitu.🙌😂😂
 
Wewe ni kibonge afu mfupi?
 
Mmmh pengine mna undugu....hisia hazidanganyi
 
Mimi pia ilikuwa hivyo watu ndio waliniambia. Eti kumbe una mdogo wako anasoma hapa. Hee kuja kumuona ni mimi kabisa. Dogo hata akawa anapenda sana kuja class kwetu.😄
 
Same to me, hakuna sehemu naenda nikose kuambiwa nina twin huko...
Kama hadi kuongea...
Kuna msanii wa bongo movie naambiwa nafanana naye, kuna mtu wake wa karibu kila tukikutana anataka anipeleke namtolea nje...

Ila sasa nikiwa sehemu ya watu wengi wanaitana, fulani huyo hapo muigizaji. Basi wananiangalia, wanaongea miye hata najali basi? Nimeshazoea..
The Boss ushahisi ni msanii gani? 😜 usimtajeee...
 
Ungemsalimia mkajenga urafiki usikute baba yako alichepuka
 
Mara nyingi hua nafananishwa na wapenzi wa watu. Utasikia umefanana na Ex wangu fulani. Hii kufananishwa ilikua inaniletea sana zali kipindi nasoma 😅

Niligundua ukiwa mtulivu/decent kimuonekano basi utafanishwa na wengi wenye muonekano kama wako
 
Njia pekee ya kuondokana na tatizo hilo ni kubadilisha muonekano kama unapenda kunyoa vipara anza kufuga nywele na ndevu kama unapenda kufuga nywele anza kunyoa style tofauti tofauti ili kupata upekee wako.. ni hatari sana kufananishwa fananishwa na watu inaweza kukuletea matatizo huko baadae niliwahi kosa mchongo fulani 2010 kwa kufananishwa na mtu fulani nisiyemjua..
 
Kwa upande mwingine ni hatari. Mtu anakuja fanya tukio akakimbia ukashikwa ww. Mpaka waje kujua si ww, huenda ukawa ushateseka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…