Mwaka 2011 kuna jamaa aliendaga Mwanza hotel saa 12 alfajiri akasema kaagizwa na meneja aje achukue sound system kwa ajili ya kuifanyia matengenezo, meneja akaelezewa na mlinzi muonekano wa huyo aliyekuja kuchukua vitu vyao.......moja kwa moja akajua ni mimi, akaniita pale ile kufika mlinzi akakazia kuwa ni mimi, ilibaki kidogo sana Gachuma aniweke ndani kwa ishu hiyo.
Wiki mbili baadae yule jamaa akataka kufanya jaribio la ivo sehemu nyingine akadakwa tukaitana wadau wote kwenda kumuona, nilienda na hasira huku nimepanga kwenda kumfanyia kitu mbaya sana......lakini kufika eneo la tukio mwili ulinisisimka na damu yote mwilini ikajikusanya sehemu moja, yani nilikuwa najiangalia mimi halisi kupitia kwa yule jamaa mwizi, yule mwizi alikuwa ni mimi copy kabisa