Turudi pale Rau Madukani
JF-Expert Member
- Jan 16, 2016
- 2,339
- 5,112
Wakati nipo mdogo mwaka 1995 au 1994 niliwahi kumfananisha mama wa watu na mama yangu.
Tulikuwa tumetoka kanisani na dada zangu wakati huo mama tulimwacha nyumbani alikuwa na safari.
Wakati tunarudi tupo njiani nikamwona huyo mama, nikamkimbilia nikamkumbatia asitembee huku nasema mama mama mama! Ikabidi na yeye anikumbatie tu. Ndio dada zangu wakamwambia amekufananisha huyu, umefanana na mama yetu.
Nilivyogundua nimeingia cha kike nikatoka nduki
Kule nyuma dada zangu wakamwelekeza nyumbani ili akamwone huyo mama wanaofana. Walivyoonana walicheka wenyewe akajisemea kuwa ni halali mwanao atufananishe. Ila mama ni mama tu, hata nilivyomkumbatia ni kama nilihisi mbona kama kuna utofauti hivi!