Kufanana na watu wengi hii imekaaje?

Kufanana na watu wengi hii imekaaje?

Wakati mwingine ni ndugu bila wewe kujua!
Mimi Kuna mtu alinifananisha na mtu mwingine, nilipochimba na kufuatilia sana nikaona naye kumbe ni ndugu yangu Mtoto wa inje ya ndoa wa baba yangu mkubwa,
Msiwe mapotezea jaribuni kufuatilia Kwa karibu
 
Hello JF

Nimejikuta nalazimika kuleta uzi sasa maana hii imeanza kunishangaza.

Tangu nakuwa ni kawaida kukutana na watu then wananiambia nimefanana na either ndugu yao fulani au jamaa zao. Imefika hatua now nimekuwa wengine mpaka hunipiga picha. Wakawaonyeshe wahusika. Ikafika muda nikawa nahesabu na kunote mahali, mpaka sasa ni zaidi ya watu 15 ambao nishakutana nao kisha wakanifananisha na jamaa zao.

Ingawa binafsi kihalisi nishakutana na watu watatu ukitutazama ni kama mapacha au ndugu wa tumbo moja. Uzuri mwingine nilikuwa nimemtangulia kidato shule moja.

Kiukweli inashangaza sana.
Mambo ya Mungu Ni ya ajabu kabisa....sura za binadamu Zina mafungu mafungu mafungu,zingine zipo common Sana zingine sio Sana...we utakuwa umeangukia kwenye group common
 
Mi nilifananishwa na watu watatu afu wa NNE nikaja onana nae mi mwenyewe airport.... Mwanamke mwenzangu ....aisee nilishtuka hata kumsimamisha niliogopa....ila tulipogongana macho tulitazamana kwa muda mrefu afu kila MTU hamwambii kitu mwenzie....Mimi mwili ulisisimka...nilijihisi upendo wa hali ya juu usioelezeka(ni kama mshtuko ulikuwa wa furaha..hata sielewi) ...njia nzima tangu tupishane ni full kugeukiana.Daaa,kumbukumbu isiyosahaulika
Kwa nini hamkusalimiana Sasa?
 
Mimi nahisi wakati Mungu ananiumba, nilikuwa kwenye toleo la watu wengi sana...
Kuanzia shule mpaka maisha ya kawaida nafananishwa kila leo...
Nimeshazoea, sielewi hao watu ni kina nani niliofanana nao hivyo!!!

Kuna mmoja niliona kwenye tangazo la nywele, yaani yule nimimi kabisa, ni kama nilikuwa najiangalia kwenye kioo...
We utakuwa Ni karembo Sana,Kama inafanana na vile vidada vya darling uko vizuri 👍
 
Kitu cha kawaida tu, Tanzania ina watu 61mil...Afrika ina watu 1.4bil...

Binafsi nimeshafananishwa na watu wengi mno maarufu na wasio maarufu...

Kuna mabinti fulani church walikuwa wananifananisha na mjomba wao sijui gani huko, ningekuwa kiwembe ningeshawanyoa kwa kutumia huo mwanya maana ilikuwa lazima kila wakati wa kutoka wanitafute ili wanione tu...

Kuna dada mmoja alikuwa cashier duka kubwa tu la vifaa vya ujenzi, alikuwa kila nikienda anashtuka na kudai nafanana na mumewe kiasi akiniona anaona kama kamuona mumewe, ningekuwa kiwembe naye ningemnyoa kupitia huo mwanya...
 
Mi nilifananishwa na watu watatu afu wa NNE nikaja onana nae mi mwenyewe airport.... Mwanamke mwenzangu ....aisee nilishtuka hata kumsimamisha niliogopa....ila tulipogongana macho tulitazamana kwa muda mrefu afu kila MTU hamwambii kitu mwenzie....Mimi mwili ulisisimka...nilijihisi upendo wa hali ya juu usioelezeka(ni kama mshtuko ulikuwa wa furaha..hata sielewi) ...njia nzima tangu tupishane ni full kugeukiana.Daaa,kumbukumbu isiyosahaulika
Watakwambia huyo ni wewe umetoka kwenye Future ndio maana mlishindwa kuongea

Mambo ya Time Travel hayo [emoji1787]
 
Mimi pia nimekutana na hiyo hali mara nyingi sana na wengine walinifananisha na waigiza filamu maarufu.

Ila cha ajabu binafsi nikiwaangalia hao ninaofananishwa nao sijioni mimi kabisa kwani mimi cha kwanza huanza kulinganisha macho kwanza na hapo najikuta ni tofauti na sijawahi kujiona kwa hao watu kwa kweli labda tuna mifanano tofauti lakini si macho.
 
Back
Top Bottom