Kufanana na watu wengi hii imekaaje?

Wakati mwingine ni ndugu bila wewe kujua!
Mimi Kuna mtu alinifananisha na mtu mwingine, nilipochimba na kufuatilia sana nikaona naye kumbe ni ndugu yangu Mtoto wa inje ya ndoa wa baba yangu mkubwa,
Msiwe mapotezea jaribuni kufuatilia Kwa karibu
 
Mambo ya Mungu Ni ya ajabu kabisa....sura za binadamu Zina mafungu mafungu mafungu,zingine zipo common Sana zingine sio Sana...we utakuwa umeangukia kwenye group common
 
Kwa nini hamkusalimiana Sasa?
 
We utakuwa Ni karembo Sana,Kama inafanana na vile vidada vya darling uko vizuri πŸ‘
 
Kitu cha kawaida tu, Tanzania ina watu 61mil...Afrika ina watu 1.4bil...

Binafsi nimeshafananishwa na watu wengi mno maarufu na wasio maarufu...

Kuna mabinti fulani church walikuwa wananifananisha na mjomba wao sijui gani huko, ningekuwa kiwembe ningeshawanyoa kwa kutumia huo mwanya maana ilikuwa lazima kila wakati wa kutoka wanitafute ili wanione tu...

Kuna dada mmoja alikuwa cashier duka kubwa tu la vifaa vya ujenzi, alikuwa kila nikienda anashtuka na kudai nafanana na mumewe kiasi akiniona anaona kama kamuona mumewe, ningekuwa kiwembe naye ningemnyoa kupitia huo mwanya...
 
Watakwambia huyo ni wewe umetoka kwenye Future ndio maana mlishindwa kuongea

Mambo ya Time Travel hayo [emoji1787]
 
Mimi pia nimekutana na hiyo hali mara nyingi sana na wengine walinifananisha na waigiza filamu maarufu.

Ila cha ajabu binafsi nikiwaangalia hao ninaofananishwa nao sijioni mimi kabisa kwani mimi cha kwanza huanza kulinganisha macho kwanza na hapo najikuta ni tofauti na sijawahi kujiona kwa hao watu kwa kweli labda tuna mifanano tofauti lakini si macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…