Si huyo peke yake, serikali ichukue hatua kwa makanisa yote yanayoitwa ya KIROHO,yakiongozwa na wanaojiita Nabii,Mtume,Kuhani n.k....makanisa yote yanayohubiri uponyaji,utajiri, kufungua nyota, kutabiri n.k.Shalom!
Serikali inayojali raia wake na mali zao ni ile inayochukua hatua za haraka sana pale jambo tatizi linapotokea kwa raia wake.
Ni hapa hapa Jamii Forum nimeandika na kurudia kwamba huyu Raia wa DRC anatumia imani ya Watanzania kutapeli na kujipatia fedha nyingi mno kinyume na taratibu za kiimani.
Hata kama nchi yetu haina dini lakini watu wake wana dini na imani zao, ni sharti Serikali inayojali watu wake kuangalia kama imani hizo zinaistawisha jamii au kuangamiza?
Nabii Dominic Kiboko ya Wachawi ameteua "engo" ya kuwapiga Watanzania masikini bila huruma akitumia staili ya ramli chonganishi. Kuna vifo vimetokea na vinaendelea kutokea kutokana na mahubiri ya Dominic anayevaa "gloves" nyeusi saa zote za ibada yake pamoja wasaidizi wake ambao wote ni wakongo.
Shuhuda za waliopoteza fedha kwa Dominic ni nyingi mno. Wengi wameuza mali zao kusaka maisha bora kwa Mzee wa Buza kwa Lulenge bila mafanikio. Baadhi ya kina mama wamefilisika kwa Dominic maana kukutana name ni Sh 500,000. Kukutana na wasaidizi wake (wakongo) ni kuanzia 100 000 hadi 300,000.
Wengine wameuza samani za ndani, nyumba, mifugo, nakadhalika kuponyeshwa magonjwa ya wazi kama Ukimwi. Presha, Saratani, Minyoo na kaswende. Wizard ya Afya iko wapi ku-clearify mambo haya ya kisayansi?
Kwa nini asiyafanye haya nchini Kongo? Kwamba mahaba yake ni kwa Watanzania pekee? Wajinga waliwao. Rwanda wameweza kudhibiti upumbavu huu. Kenya wamefuata na Burundi nao wameweza. Na sisi tuweze. Huyu tapeli apewe saa 24 kuondoka nchini na mali zake zitaifishwe ili iwe fundisho. Lakini na sisi umma tujiepeshe na hizi ramli chonganishi kupitia madhabahu ya kiimani. Hongera Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
#KaziIendelee!
Haya yote ni janga kwa jamii na kwa Taifa pia.