Uchaguzi 2020 Kufungiwa Lissu kwa siku 7 ni ‘advantage’ kubwa sana kwake

Kweli tupu. Pia anaweza kufanya mambo mengine yatakoyoweza kumpaisha kuliko hata kama angefanya kampeni. Aitumie fursa hii vizuri mpaka hao vibaraka wa CCM wajute ni kwanini walichukuwa hatua hii.
 
Hakuna cha kupumzika, msibadili gia bana, huyo kafungiwa na NEC siku saba kama kweli yeye jeuri aendelee na msimamo wake kufanya kampeni
 
Kuna wakati najiuliza hii mitego ya TL huwa hawaioni au wanafanya makusudi tu kumridhisha Mkuu wakati wakijua kuwa wanamtengenezea njia TL? siamini kuwa hiyo huwa ni bahati mbaya
Tatizo amejua anaepambana nae ni mtu wa jazba,Hata kwenye karate tunaelekezwa ni rahisi sana kumdunda mtu aliepanic au kupandwa na jazba.JPM kaonywa sana juu ya ujio wa LISU kuwa aachane nae kaja kumuharibia image ya kitaifa na kimataifa juu ya udikteta wake uchwara.SO HILI LA KUMFUNGIA SIKU 7 LITAMPAISHA SANA TUNDU LISU.
 
Nashauri TL na kamati yake watumie muda huu wa kusimamishwa kwa kampeni zao kuandaa mikakati ya kupata mawakala wasomi, wenye nguvu, waaminifu,na wahakikishe kila kituo kinakuwa na mawakala zaidi ya mmoja kwa kutumia uwakilishi wa vyama rafiki hasa ACT wazalendo.

Kumbuka kivumbi, patashika nguo kuchanika, figisu, vitimbwi, mazingaombwe, vituko na kila aina ya mihemko, kura kupotea, mabox kunyakuliwa, mawakala kushambuliwa na kunyimwa nakala za matokeo, kunyimwa fomu za malalamiko, kukataa kusaini matokeo, kubadili matokeo kwa maana ya kura za A kumpa B na za B kumpa A, yote hayo muda wake ni kuanzia saa1 jioni ya tarehe 28/10/2020.

Uzoefu wangu unanionyesha kuwa hicho ndio kitakachokuwa kipindi kigumu na cha kutisha sana huenda kuliko nyakati nyingine zote katika historia ya uchaguzi wa nchi hii.

Ndio kipindi pekee cha kuhakikisha chungwa linabaki kuwa chungwa, au kwa nguvu ya ajabu, chungwa litabadilishwa kuwa limau.

Ndio kipindi cha kuamua hatima ya amani ya nchi hii.
 
Natumaini kamati ya utendaji ya Chadema itazingatia ushauri makini!
Kudos!
 
Lisu ana jitutumua Ila hana uwezo wa kupambana na JPM katika sanduku la kura, na anajua anakwenda kushindwa sasa anatengeneza mazingira ionekane ana nyanyaswa Ila haita zuia kuchezea kichapo kwenye sanduku la kura.
 

Kama nimemsikiliza vizuri amesema kama kamati kuu itasema asubiri siku 7 atasuburi ila yeye binafsi anaendelea kujinoa kwa kuendelea na kampeni kesho, inawezekana kamati kuu ikasema akate kwa kamati ya rufaa ya maadili. Lakini hili litakuwa ni gumu sama kamati ya maadili itachelewesha muhutasari wa maamuzi ili siku ziishe kabla kama ya rufaa ya maadili haijakaa na hivyo shauri kuwa limepitwa na wakati.
 
Kesho lissu yupo kazini muda sio rafiki .Awe anafanya kampeni kama mjumbe wa nec wa chadema au makamu mwenyekiti .Kesho
yupo road .Asipofanya kampeni siku 7 ni zaidi ya majimbo 30 au mikoa 4 hataweza kufika kucover.
Muda haupo.
 
Nasapoti hili wazo mkuu

Hata yeye amesema kama chama kitamtaka apumzike basi atafanya hivyo.
 
Chadema mnaaongoza kwa kujidanganya tena mchana kweupe, nyie lisu anajulikana mtandaoni tu wananzengo hawajui
 
Bravo. To every cause there is a reason.
 
Pole sana
Huu ni wakati wenu kupiga poyoyo na kubwabwaja, kwanza lisu anakesi ya kumshtumu rais kwamba ameagiza apigwe guni,tutaleta ripoti ya uchunguzi siku si nyingi ,watanzania hawawezi mchagua mtu wa ajabu kama lisu hatupendi watu wasingiziaji na wasaliti watakao iuza nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…