Hivi vyote Mbona vinafanyika?
Kwa sasa ukiwekeza nchini na ukasajili mradi wako TIC haulipi corporate tax kwa miaka 10. Pata taarifa hiyo Mkuu.
Si suala la kodi tu ,kuna vitu chungu mzima vinahusika kufanya taifa kuwa maridadi katika sekta ya viwanda , misingi ni mibovu ya hii nchi .
Inconsistencies katika sera pia ni kikwazo , leo yupo samia kesho yupo mwingine naye atakuja na sera zake na kuanza usumbufu ,kiufupi hii nchi ina poor organization .
Taasisi mfu zipo kama picha tu ,useless burecracies .
Na suala la miundombinu pia ,kitu kama umeme , huwezi kuwa na sekta ya viwanda bila umeme wa uhakika tena uwe so cheap , nenda mtandaoni uangalie bei za unit za umeme Vietnam ,Indonesia , Thailand ,Malaysia , China nk
Huwezi kumshawishi mwekezaji aje kufunga na kuendesha kiwanda hapa kuzalisha bidhaa wakati nchi inategemea power grid ya umeme wa Magumashi huu wa TANESCO usio na upatikanaji wa uhakika na pia uzalishaji bado ni mdogo na bei ya umeme bado ni kubwa .
Viwanda ni heavy consumers WA umeme tena inahitajika umeme wa uhakika muda wote .
Tuje kwenye miundombinu ya usafiri kama railways , road networks , bandari viwanja vya ndege na huduma zake , hii nchi bado sana , logistics ni kitu cha muhimu kwenye sekta ya viwanda , wazalishaji wa bidhaa wanaenda na muda si bidhaa ikizalishwa inatakiwa ifikishe sokoni kwa muda mfupi sana
Malighafi pia hivyo hivyo nk
So ukiangalia kuna vitu vingi sana bado tuko nyuma ,la sivyo sekta ya viwanda tutakuwa tunaiota tu kila siku mpaka tushughulikie hayo masuala hapo juu