Kufungua kiwanda Tanzania ni gharama kuliko kuagiza nje, sera ya Tanzania haisapoti viwanda vya ndani

Kufungua kiwanda Tanzania ni gharama kuliko kuagiza nje, sera ya Tanzania haisapoti viwanda vya ndani

balozi wa Uingereza nchini Tanzania anayemaliza muda wake David Concur anasema wazalishaji wengi wa Tanzania wanashindwa kulihudumia soko la ndani kwa sababu bidhaa za kuagiza ni nafuu zaid
Kitu ambacho Balozi amekisahau ni kuwa, mikakati yote yakuidhalimu Afrika ilipangwa EXETER Hall-Ikiwemo ya Kuua, Kubaka, Kubadilisha dini, mila na desturi za Watanzania na mambo mengine mengi tu kuhusu mustakabhali wa Uingereza na makoloni yake kwa kile walichokiita kuchochea maendeleo. Rongo sana.

EXETER hall ipo Uingereza na ndipo mikutano ya kupanga mikakati mingi ya Ubeberu Duniani ilipofanyika.

Balozi katoka Uingereza. Asituzuge.
===
Marehemu Rais Mkapa alikuwa sawa. Tuachane na mambo ya EPA na Waingereza. Watatunyonya na kuviacha viwanda vyetu kuwa makanisa.

Mungu awalaani wazugaji
 
Mzungu kuondoka toka 1961 ,Ukoloni uliobaki ni vichwani mwa wananchi na viongozi wao
 
Nimemsikiliza balozi wa Uingereza nchini Tanzania anayemaliza muda wake David Concur anasema wazalishaji wengi wa Tanzania wanashindwa kulihudumia soko la ndani kwa sababu bidhaa za kuagiza ni nafuu zaidi. Hii inasababisha viwanda vichache kufunguliwa na kupelekea upungufu wa ajira.

Mfano mzuri, ni vitenge vinavyozalishwa hapa nchini bei yake ni juu kuliko vinavyoagizwa nje hii inamaanisha gharama za uzalishaji Tanzania ni kubwa kupitiliza.

Ukienda kariakoo, na masoko yote makubwa utagundua bidhaa nyingi zinatengenezwa China. Hata vifaa Kama furniture vinatokea China ilhali mazao ya misitu yanatoka huku Africa.

Tunashindwa nini kuongeza uzalishaji? Sera mbovu!, nini kifanyike tuwajengee uwezo wazawa na wageni kuweka viwanda nchini.

TIC inajitahidi kuhamasisha uwekezaji lakini ni lazma ziwepo jitihada za makusudi kurekebisha Sera zetu. Nchini China, Taiwan, India au Korea uchumi wa viwanda unachangia Sana pato la taifa.

4R HOYEE

Watanzania hatuendelei kwa sababu mabilionea wengi utajiri wao unatokana na ruzuku za serikali. Kuanzia Mo Dewji, Bakhressa, Asasi hadi wahindi wa upanga. Huu inatokana na wao kutoa gawio wagawane na watoa Ruzuku.
 
Imagine miaka 60+ imepita bado tumekwama kwenye giza nene kama hilo ambalo sisiem kwa makusudi wamegoma kuwasha taa.
 
Mkuu nimesema wizara iweke sera ya kuvutia viwanda mfano ukiajiri watanzania 5000 haulipi kodi (corporate tax) kwa miaka 2,halafu unachukua kodi zingine PAYE etc
Hivi vyote Mbona vinafanyika?

Kwa sasa ukiwekeza nchini na ukasajili mradi wako TIC haulipi corporate tax kwa miaka 10. Pata taarifa hiyo Mkuu.
 
Sio rahisi kuwepo kwa sera za ku support viwanda, ajira za ndani.
Ni mpaka ziwepo machaduko ya wenyewe kwa wenyewe mwisho watu Wana Kaa mezani na kufanya maamuzi ya pamoja ya maslai kwa wote.
Nchi zote zilizo endelea duniani zimepitia hatua hii, lazima zipigwe wenyewe kwa wenyewe kwanza.
Ngumu sana watu kuweka maslai ya wote mbele.
 
Ajabu viongozi wenye dhamana wanajisifu kuwa mazingira ya uwekezaji ni mazuri.Sijui akili zao zikoje tu.Mfano mwingine kunakiwanda Cha marumaru(tiles)hapo pwani lakini bei zake ni kubwa kuliko zinazotoka china na ulaya ambazo ndiyo imara zaidi kuliko hizo za mkoa wa pwani.mfano mwingine unaagiza gari kutoka ulaya inauzwa milioni kumi lakini ikifika hapa Tanganyika unakadiriwa Kodi inazidi bei ya ununuzi wa gari.kiujumla Tanzania inaongozwa na Wendawazimu

Something need to be done hii nchi iendelee. Hata mtandao wa kupokelea pesa kutoka ughaibuni (PAY PAL) wamezuia. Means wewe ni mtu wa kulipa na kununua tu si kupokea. Najiuliza nia ya huyo kibopa aliepo BOT ni nini hasa kwa vijana wanaotaka kuuza bidhaa zao kwenye masoko ya kimataifa online, Kama si uchawi ni nini? Ccm must go!
 
Naona Kila mtu ana lalamika, tupendekeze suluhisho..unaposema sera irekibishwe be specific sera ipi

Binafsi naona production cost ni kubwa kuwa sababu ya bei ya umeme, umeme Tanzania ni ghali sana,

Pili, Kodi ziondolewe kwa mashine za kuongeza thamani za bidhaa

Na mwisho Mazingira ya kuagiza mashine za kati pamoja na malighafi uboreshwe, uwe na uwazi na rahisi, kusiwe na monopoly au mtu kati,
Ni machine zipi zenye kodi nchi hii? Machines kwa asilimia zaidi ya 90 hazing import duty. Nafikiri wengi tunaozungumza mtandaoni hatuna uelewa wa masuala ya uwekezaji mkubwa.

Mfano, sasa uzalishaji wetu wa tiles ni mkubwa kuliko mahitaji na tunauza nje kwa wingi, Cement halikadhalika tuko vizuri, bidhaa za chuma kwa maana ya mabati na nondo tuko vizuri sana, nk

Watanzania tunatabia ya kujidharau sana kısa kasema mzungu, na hatuna taarifa sahihi kuhusu nchi yeti
 
Ajabu viongozi wenye dhamana wanajisifu kuwa mazingira ya uwekezaji ni mazuri.Sijui akili zao zikoje tu.Mfano mwingine kunakiwanda Cha marumaru(tiles)hapo pwani lakini bei zake ni kubwa kuliko zinazotoka china na ulaya ambazo ndiyo imara zaidi kuliko hizo za mkoa wa pwani.mfano mwingine unaagiza gari kutoka ulaya inauzwa milioni kumi lakini ikifika hapa Tanganyika unakadiriwa Kodi inazidi bei ya ununuzi wa gari.kiujumla Tanzania inaongozwa na Wendawazimu
Mimi hapo kwenye magari tena haya used sitokuja kuielewa serikali kwa nini inaweka kodi kubwa kiasi kile.
 
Ni machine zipi zenye kodi nchi hii? Machines kwa asilimia zaidi ya 90 hazing import duty. Nafikiri wengi tunaozungumza mtandaoni hatuna uelewa wa masuala ya uwekezaji mkubwa.

Mfano, sasa uzalishaji wetu wa tiles ni mkubwa kuliko mahitaji na tunauza nje kwa wingi, Cement halikadhalika tuko vizuri, bidhaa za chuma kwa maana ya mabati na nondo tuko vizuri sana, nk

Watanzania tunatabia ya kujidharau sana kısa kasema mzungu, na hatuna taarifa sahihi kuhusu nchi yeti
Nchi hii kuna tatizo kubwa sana la kodi na tozo. Mpaka ninapoandika hapa, sukari ni bei ya chini hapo Malawi na Zambia ukilinganisha na Tanzania, kodi za kuagiza magari vile vile. Nchi hii kuna utitiri wa kodi na tozo mpaka kero.
 
Nimemsikiliza balozi wa Uingereza nchini Tanzania anayemaliza muda wake David Concur anasema wazalishaji wengi wa Tanzania wanashindwa kulihudumia soko la ndani kwa sababu bidhaa za kuagiza ni nafuu zaidi. Hii inasababisha viwanda vichache kufunguliwa na kupelekea upungufu wa ajira.

Mfano mzuri, ni vitenge vinavyozalishwa hapa nchini bei yake ni juu kuliko vinavyoagizwa nje hii inamaanisha gharama za uzalishaji Tanzania ni kubwa kupitiliza.

Ukienda kariakoo, na masoko yote makubwa utagundua bidhaa nyingi zinatengenezwa China. Hata vifaa Kama furniture vinatokea China ilhali mazao ya misitu yanatoka huku Africa.

Tunashindwa nini kuongeza uzalishaji? Sera mbovu!, nini kifanyike tuwajengee uwezo wazawa na wageni kuweka viwanda nchini.

TIC inajitahidi kuhamasisha uwekezaji lakini ni lazma ziwepo jitihada za makusudi kurekebisha Sera zetu. Nchini China, Taiwan, India au Korea uchumi wa viwanda unachangia Sana pato la taifa.

4R HOYEE

Mkuu, asante kwa kuleta hii mada.

ila nadhani haupo sahihi kwa asilimia kubwa kusema, "Hata vifaa Kama furniture vinatokea China ilhali mazao ya misitu yanatoka huku Africa". China ni number moja duniani kwa ku export mazao ya misitu ikiwemo "Mbao". Na imekuwa namba moja kwa kipindi cha mda mrefu kidogo. Pili, hakuna nchi yeyote ya Africa ambayo ipo kwenye top 10 kwenye nyanja ya ku export mbao.

Juu ya hapo, china wanalipa mishahara mikubwa kulinganisha na hapa Tanzania kwa watu wa viwandani. inamaana bei za china zilitakiwa kuwa kubwa, kwasababu wanalipa mishahara mikubwa,pia kuongeza ushuru na usafirishaji. ila, lakini bado bei zao ni chini kwasababu ya "faida ya kuzalisha kwa wingi au wanaita economy of scale". Hii inasababishwa na kutumia machine au kuwa na miundo mbinu ya kisasa.

Viwanda haviwezi kuja tu kwasababu watu wana pesa, pia inategemea kama kuna experts au upatikanaji wa watu ambao wanauwezo wa kuendesha kiwanda,hii ikiwemo wafanyakazi. Nadhani serikali inatakiwa kuwekeza sana kwenye elimu, haswa kwenye eneo la "technical skills",kuwa na vitu kama VETA. hivi ndio vitu vitavyo chochea viwanda.

Mwekezaji anaweza kuwa na pesa ya kuwekeza, ila kama ataona hakuna watu wa kuweza kuendesha hicho kiwanda kwenye nchi, anaweza hasiweze kuwekeza.
 
Nchi hii kuna tatizo kubwa sana la kodi na tozo. Mpaka ninapoandika hapa, sukari ni bei ya chini hapo Malawi na Zambia ukilinganisha na Tanzania, kodi za kuagiza magari vile vile. Nchi hii kuna utitiri wa kodi na tozo mpaka kero.
Hiyo Sukari ya Malawi au Zambia yenye bei nafuu imezalishwa kwenye hizo nchi? Jitahidi uwe na taarifa sahihi
 
Hivi vyote Mbona vinafanyika?

Kwa sasa ukiwekeza nchini na ukasajili mradi wako TIC haulipi corporate tax kwa miaka 10. Pata taarifa hiyo Mkuu.
Si suala la kodi tu ,kuna vitu chungu mzima vinahusika kufanya taifa kuwa maridadi katika sekta ya viwanda , misingi ni mibovu ya hii nchi .
Inconsistencies katika sera pia ni kikwazo , leo yupo samia kesho yupo mwingine naye atakuja na sera zake na kuanza usumbufu ,kiufupi hii nchi ina poor organization .
Taasisi mfu zipo kama picha tu ,useless burecracies .
Na suala la miundombinu pia ,kitu kama umeme , huwezi kuwa na sekta ya viwanda bila umeme wa uhakika tena uwe so cheap , nenda mtandaoni uangalie bei za unit za umeme Vietnam ,Indonesia , Thailand ,Malaysia , China nk
Huwezi kumshawishi mwekezaji aje kufunga na kuendesha kiwanda hapa kuzalisha bidhaa wakati nchi inategemea power grid ya umeme wa Magumashi huu wa TANESCO usio na upatikanaji wa uhakika na pia uzalishaji bado ni mdogo na bei ya umeme bado ni kubwa .
Viwanda ni heavy consumers WA umeme tena inahitajika umeme wa uhakika muda wote .
Tuje kwenye miundombinu ya usafiri kama railways , road networks , bandari viwanja vya ndege na huduma zake , hii nchi bado sana , logistics ni kitu cha muhimu kwenye sekta ya viwanda , wazalishaji wa bidhaa wanaenda na muda si bidhaa ikizalishwa inatakiwa ifikishe sokoni kwa muda mfupi sana
Malighafi pia hivyo hivyo nk
So ukiangalia kuna vitu vingi sana bado tuko nyuma ,la sivyo sekta ya viwanda tutakuwa tunaiota tu kila siku mpaka tushughulikie hayo masuala hapo juu
 
Back
Top Bottom