Kufunua siri za maendeleo ya miaka hii kumi: Zaidi ya watu milioni 9.6 waliohamishwa katika maeneo maskini waanza maisha mapya

Kufunua siri za maendeleo ya miaka hii kumi: Zaidi ya watu milioni 9.6 waliohamishwa katika maeneo maskini waanza maisha mapya

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
INTRO: Katika vita dhidi ya umaskini, jumla ya watu maskini milioni 98.99 nchini China wameondolewa kwenye umaskini uliokithiri. Miongoni mwao, zaidi ya watu milioni 9.6 wameondolewa kwenye umaskini kupitia kuhamishwa kwenye maeneo maskini na kupelekwa maeneo yenye huduma zote. Utaratibu huu wa kuwahamisha watu kwenye maeneo maskini hadi sasa umeleta mabadiliko makubwa.

微信图片_20220816113021.png


Katika mpaka wa kusini-magharibi mwa China, Kaunti ya Fugong, Mkoa wa Yunnan una maeneo 15 ya kuwahamishia watu na makazi mapya. Kwa msaada wa satilaiti, mabadiliko ya miaka kumi ya vijiji kadhaa maskini katika Kaunti ya Fugong yalirekodiwa.

Kati ya mlima mmoja na mwingine, je, uhamisho huu ni wa aina gani?

Milima na mito imezibwa na safari za magari zimezuiwa, jambo ambalo limekuwa likiwasumbua watu wa Nujiang kwa vizazi vingi. Usumbufu huu uliendelea kuwepo hadi pale kazi ya kuondoa umaskini na kuwahamisha watu kwenye eneo hilo ilipoanza miaka minne iliyopita, na familia ya watu 7 ya Lao Luo, mwanakijiji wa Kijiji cha Tuoping, hatimaye iliondoka kwenye nyumba ya nyasi iliyokuwa ikivuja kila mahali, na kukata kiu ya muda mrefu ya vizazi kadhaa ya kutoka milimani na kuondokana na umaskini.

Sasa Luo mwenye umri wa miaka 58 anafanya kazi kama "mjomba anayesambaza vifurushi" wakati wa msimu wa kilimo usio na shughuli nyingi. Lao Luo alikuwa hajawahi kusafiri kwa kasi ya makumi ya kilomita kwa saa. Zamani nyumbani kwake kulikuwa mlimani, na alipotoka ilimchukua siku nzima kwenda na kurudi.

Vijiji vyote hivi vya Kaunti ya Fugong viko kwenye mwinuko wa mita 1,600, na vingine vimefikia hadi mita 2,500. Mwaka 2018, wanakijiji walifuata njia hii ya kuhama na kuishi chini ya mlima. Maeneo makubwa na madogo ya makazi mapya yametapakaa katika kaunti nzima, kando ya Mto Nujiang. Jumla ya watu 22,000 wamehamishiwa kwenye maeneo 15 ya makazi mapya, sawa na moja ya tano ya idadi ya wakazi wa kaunti hiyo.

Katika muongo mmoja uliopita, China imezindua mpango mkubwa wa kupunguza umaskini na kuwahamisha watu sio tu katika pande mbili za Mto Nu, bali hata katika maeneo kama vile mikoa ya kati na magharibi yenye milima mirefu, jangwa kali, na nyanda za juu.

Kijiji cha Utamaduni wa Ando kipo katika Kaunti ya Xinghai, Mkoani Qinghai, kaskazini magharibi mwa China. Nyumba mpya zilijengwa kwenye eneo la ardhi tupu lenye ukubwa wa hekta 100, na vijiji 48 maskini vya jirani vilihamia hapa.

Hili ni eneo la makazi mapya la Bijie Boyanglin kusini magharibi mwa Mkoa wa Guizhou nchini China. Nyumba 7,265 za makazi mapya zilijengwa kuanzia hatua ya msingi, na watu 29,000 walihamia kwenye nyumba mpya.

Hili ni eneo kuu la makazi mapya katika Kaunti ya Zhaojue, Mkoa wa Sichuan, Kusini-magharibi mwa China, ambapo watu maskini 18,000 walihama mlimani na kuhamia mjini.

Kutokana na utaratibu huu wa kuhamisha watu, takriban maeneo 35,000 ya makazi mapya yamejengwa kote nchini, ambapo zaidi ya watu maskini milioni 9.6 wamehamishwa, ikiwa ni sawa na kuhamisha watu katika nchi yenye idadi ya saizi ya kati.

Katika miaka kumi iliyopita, vizazi vingi vya watu maskini vimeagana na vibanda vya udongo, kilimo cha jadi cha kufyeka na kuchoma moto, na kuingia moja kwa moja katika maisha ya kisasa na mazuri.

Katika miaka kumi iliyopita, uhamiaji huu wa kipekee, ambao haujawahi kutokea katika historia ya binadamu, umeleta muujiza mkubwa duniani.
 

Attachments

  • 微信图片_20220816113030.png
    微信图片_20220816113030.png
    375.8 KB · Views: 4
Back
Top Bottom