DOKEZO Kuhani Musa Richard Mwacha ashitakiwe kwa kuwadhalilisha watoto wadogo

DOKEZO Kuhani Musa Richard Mwacha ashitakiwe kwa kuwadhalilisha watoto wadogo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Na majira ya usiku katikati ya ibada kinawekwa kipindi cha shuhuda. Ukifuatilia kwa undani utaona ni kama anawapanga watoto wadogo wakajisalimishe kwake yaani wanakwenda kwa Kuhani kukiri kuwa ni wachawi na walikuwa wanakula nyama za watu.
Kwa tunaomfahamu huyu mtu ni muhuni kweli kweli! hana cha dini wala Mungu.
Nikiona wanaokwenda nawaona ni wagonjwa wa akili na wapuuzi wakubwa!
 
MWANZO 17:15-21
Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara.
Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake.

Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.

Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.

Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.

Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao.



YAKOBO 1:27
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ

[ AL I'MRAN - 67 ]
Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.
 
مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ

[ AL I'MRAN - 67 ]
Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.

Umeelewa maana ya kukuwekea hizo verse hapo?

Kwa kifupi
Ishmael na Isaka wote ni watoto wa Ibrahim na wote wana baraka za mwenyezi Mungu katika utofauti wao

Na dini iliyo bora ni matendo mema na kushika amri za mwenyezi Mungu

Hayo mengine yote ni ushirikina wa kiimani
 
Magufuli alizibidi kila aina ya utapeli. Kwanini awamu hii wamelipuka kila kona ya nchi?
 
Ukishakuwa mlokole tayari kunakuwa kuna sehemu ya akili yako umeipoteza.
Mathayo 16:25
"Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. "

Mathayo 16:26
"Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?"
 
Dini yangu : Mkristo
Dhehebu : Lutheran kila ijumapili najua ndio Sala masaa kadhaa eh Mungu nisaidie tofauti na hapo sijui dhehebu lingine Asanteni
 
Ni shuhuda za uchonganishi na mafarakano na huo sio msingi wa Kikristo. Watu wengi hamjui na mnaulaumu sana Ukristo kwa ajili ya uhuni wa wazi wachache. Uhuni wa watu wachache ni wao wenyewe na hauhusiani na Ukristo. Hii ni sawa na Shehe kubaka, hakuhusiani na Uislamu bali ni mtu mwenyewe.

Msingi wa Ukristo ni imara na umejengwa juu ya Kristo mwenyewe ambaye ndiye jiwe la msingi. Mi ninatumika kanisani huku kwetu na wapo watumishi wenye weledi na maadili mazuri ya kiroho na sio hao wahuni wasiojitambua wala kujua nini wanafanya. Maadili ya Kikristo hayaruhusu shuhuda za namna hiyo wala kuuliza mapepo wala kuwa na visaidizi kama Mafuta, maji, chumvi, udongo, leso, keki n.k.

Sisi tumeachiwa Jina la Yesu. Hilo ndilo liponyalo, liokoalo, litakasalo, lifungualo vifungo, linalotushindia kwa maana hapana wokovu katika mwingine zaidi ya Jina la Yesu. Na katika Jina hilo kila Goti litapigwa likiwepo goti la Kuhani Mussa na la Mkureshi Muddy(56) mme wa Bi. Aisha(9)🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣😜😆
Uzuri ni kuwa na yeye kuhani Musa anajiamini kuwa yuko sahihi tena kwa kutumia biblia hiyo hiyo na yesu huyo huyo kama unavyojiona wewe uko sahihi so Huna cha kumwambia 🤣🤣🤣. Habari za Muhammad (SAW) achana nazo kuziingiza kwenye mada hii. We pambana na kuhani 🤣🤣🤣 na ukitaka vifungu vya biblia vinavyosapoti anayoyafanya atakupa.
 
مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ

[ AL I'MRAN - 67 ]
Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.
Ibrahim alikuwa muislamu how?
 
[emoji419]hivi mamlaka kwa nini hazichukui hatua Kwa hawa jamaa..!? inafikirisha sana... uo ukuhani alipewa na nani... zindukeni na hawa matapeli wa kiroho
 
Back
Top Bottom