Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mlioko huko ni msaada kwetu wa bushSijui wanamzunguziaje, labda utuhabarishe wewe
Isaya 5:13-14Haha basi ulichopost hakina maana sababu ni cha kufikirika. Fanya utafiti ndio uandike 😆😆
Pesa lazima utoe Wala usiweke uume wako rehani mkuu, they are money huntersKama kuna mtu yuko tayari twende nimpeleke aombe kuonana na Kuhani asipolipishwa pesa Mimi nitaukata uume wangu
Kama kuna mtu yuko tayari twende nimpeleke aombe kuonana na Kuhani asipolipishwa pesa Mimi nitaukata uume wangu
sawasawaFanya tumkamate Kuhani Musa tuje kushuhudia uongo wake hapa
Huwa anachaji hela kumuona hata mimi nina uhakika na hilo, kuna wa 20,000, kuna wa 50,000, kuna wa 100,000 na kuendeleaKama kuna mtu yuko tayari twende nimpeleke aombe kuonana na Kuhani asipolipishwa pesa Mimi nitaukata uume wangu
Ni kweli ukienda kanisani kwake utamwona tu na utasikiliza mahubiri, ila kamq inahitaji huduma ya maombi ni lazima ulipie na uoangiwe muda wa kumwona,Ukitaka kumuona si unaenda tuu kanisani kwake utamuona? Hayo mambo ya kiingilio inakuaje
Hiyo sadaka anatumia nani?Chakula cha Mungu ni sala na maombi, funga na sadaka
Daaaahhh, halafu wapambe wake wanahalalisha huo utapeli kwa Stori za kwenye kitabu Cha Samweli.Pesa lazima utoe Wala usiweke uume wako rehani mkuu, they are money hunters
Wametekwa hawawez kujinasua Kutoka hapo ni ngumuDaaaahhh, halafu wapambe wake wanahalalisha huo utapeli kwa Stori za kwenye kitabu Cha Samweli.
Analipwa kwa kazi hiyo hahahahahaHuyu Bwana ana mpambe wake uitikia kibwagizo kuongeza mbwembe . KILA aongeacho mtumishi utasikia " ndipo," amiiina" kama utoto fulani hivi si amuache mtumishi anene mwenyewe bila kibwagizo. Anaboa Sana yule mpambe, imenifanya hata nisimfatilie kwa kukerwa na vibwagizo vya injili nyepesi.
Binafsi anakera ni kama comedy sasa.Analipwa kwa kazi hiyo hahahahaha
Yale ya semaaa fayaaaaaaa, mwambie huyo anayelala Mimi ni kondoooo mtu anatoka kanisani na ujumbe wa kondoo kuwa kaambiwa yeye ni kondooooBinafsi anakera ni kama comedy sasa.
Watu wafundishwe kwa utulivu kama Mwalimu Mwakasege Ili yawaingie na sio kupayuka payuka.Mahubiri ya mwendokasi uingia na kutoka kichwani ayambadilishi mtu.
Ukihitaji huduma ya ziada yaani mnakuwa wenyewe. Mie sijawahi Onana nae privately na nimepona. Ni Sawa anaepanda ndege kwenda Arusha na basi wote wanafika Sema mmoja ni special mwingine mwenzangu na Mimi.Ukitaka kumuona si unaenda tuu kanisani kwake utamuona? Hayo mambo ya kiingilio inakuaje mama kubwa?
Nimekumbuka vile Sauli alienda kwa nabii Samuel akawa hana sadaka akalipiwa shekeli ili aweze kumwona
1Samweli 9
1 Basi, kulikuwa na mtu mmoja wa Benyamini, jina lake akiitwa Kishi, mwana wa Abieli, mwana wa Serori, mwana wa Bekorathi, mwana wa Afia, mwana wa Mbenyamini, mtu shujaa, mwenye nguvu.
2 Naye alikuwa na mwana, aliyeitwa jina lake Sauli, kijana, tena mzuri; wala katika wana wa Israeli hakuwako mtu mzuri kuliko yeye; tangu mabega yake kwenda juu alikuwa mrefu kuliko watu wote.
3 Na punda za Kishi, baba yake Sauli, walikuwa wamepotea. Kishi akamwambia Sauli mwanawe, Haya basi, twaa mtumishi mmoja pamoja nawe, uondoke, uende ukawatafute punda hao.
4 Naye akapita kati ya nchi ya milima milima ya Efraimu, akapita na kati ya nchi ya Shalisha, lakini hawakuwaona; kisha wakapita kati ya nchi ya Shaalimu, wala huko hawakuwako; wakapita kati ya nchi ya Wabenyamini, lakini hawakuwapata.
5 Hata walipofika nchi ya Sufu, Sauli akamwambia yule mtumishi aliyefuatana naye, Haya, na turudi, baba yangu asije akaacha kufikiri habari za punda akatufikiri sisi.
6 Naye akamwambia, Tazama, katika mji huu mna mtu wa Mungu, naye ni mtu mwenye kuheshimiwa; yote asemayo hutukia kweli kweli; basi, twende huko; labda yeye aweza kutuambia habari ya safari yetu tunayoiendea.
7 Ndipo Sauli akamwambia mtumishi wake, Lakini angalia, kama tukienda, tumpelekee mtu huyo kitu gani? Maana chakula kimekwisha vyomboni mwetu, wala hapana zawadi ya kumpelekea mtu wa Mungu; tuna nini sisi?
8 Yule mtumishi akamjibu Sauli, akasema, Tazama, mkononi mwangu nina robo ya shekeli ya fedha; nitampa huyo mtu wa Mungu fedha hiyo, atuambie njia yetu.
9 (Hapo zamani katika Israeli, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa Mwonaji.)
10 Basi Sauli akamwambia mtumishi wake, Umesema vema; haya! Twende. Wakaenda mpaka mji ule aliokuwamo mtu wa Mungu.
11 Hata walipokwea kwenda mjini, wakakutana na wasichana, wanatoka kwenda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko?
12 Nao wakawajibu, wakasema, Yuko; tazama, yuko huko mbele yako; fanyeni haraka sasa, maana hivi leo amekuja mjini; kwa sababu watu wana dhabihu leo katika mahali pa juu;
13 mkiingia mjini tu, mara mtamwona, kabla hajakwea kwenda mahali pa juu ale chakula; maana, watu hawatakula hata yeye atakapokuja; kwa sababu yeye ndiye anayeibarikia dhabihu; kisha hao watu walioalikwa hula. Basi, kweeni sasa; maana wakati huu ndio mtakapomwona.
14 Nao wakakwea kwenda mjini; nao walipokuwa wakiingia mjini, tazama, Samweli akawatokea, kwenda mahali pa juu.
15 Basi Bwana alikuwa amemfunulia Samweli, siku moja kabla Sauli hajamwendea, akisema,
16 Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia.
17 Hata Samweli alipomwona Sauli, Bwana akamwambia, Huyu ndiye niliyekuambia habari zake; huyu ndiye atakayewamiliki watu wangu.
18 Ndipo Sauli akamkaribia Samweli langoni, akasema, Tafadhali, uniambie, nyumba ya mwonaji iko wapi?
19 Samweli akamjibu Sauli, akasema, Mimi ndimi mwonaji; tangulia mbele yangu ukwee mpaka mahali pa juu, kwa maana mtakula pamoja nami leo; kisha, asubuhi nitakuacha uende zako, nami nitakuambia yote uliyo nayo moyoni mwako.
20 Na wale punda zako waliopotea siku hizi tatu, usijiudhi kwa ajili yao; maana wameonekana. Na yote yaliyotamanika katika Israeli amewekewa nani? Si wewe, na nyumba yote ya baba yako?
21 Basi Sauli akajibu, akasema, Je! Mimi si Mbenyamini, mtu wa kabila iliyo ndogo kuliko kabila zote za Israeli? Na jamaa yangu nayo si ndogo kuliko jamaa zote za kabila ya Benyamini? Kwa nini basi, kuniambia hivyo?
22 Naye Samweli akamtwaa Sauli na mtumishi wake, akawaleta ndani sebuleni, akawaketisha mahali pa heshima kati ya watu walioalikwa, nao jumla yao walikuwa kama watu thelathini.
23 Samweli akamwambia mpishi, Lete ile sehemu niliyokupa, hiyo niliyokuambia, Iweke akiba.
24 Basi mpishi akatwaa paja, na nyama iliyokuwa juu yake, akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, Iliyowekwa akiba ndiyo hiyo! Iweke mbele yako ule, kwa sababu umewekewa hiyo wewe hata wakati uliokusudiwa, maana nalisema, Nimewaalika watu. Basi Sauli akala pamoja na Samweli siku hiyo.
25 Hata waliposhuka kutoka mahali pa juu na kufika mjini, akaongea na Sauli darini.
26 Nao wakaamka alfajiri; kisha ikawa, kulipopambazuka, Samweli akamwita Sauli darini, akisema, Inuka, nikupeleke kwenu. Basi Sauli akainuka, nao wakatoka wote wawili, yeye na Samweli.
27 Hata walipokuwa wakishuka mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atangulie, (naye akatangulia), bali wewe simama hapa sasa, ili nikuambie neno la Mungu.